Sheikh Ponda sasa njia panda

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
ponda+clip.jpg

Dar es Salaam. Maombi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda ya kuomba ufutiwa shtaka la kukiuka uamuzi wa mahakama, yamebaki njiapanda baada ya Jamhuri kuyawekea pingamizi la kisheria, ikiiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iyatupilie mbali.

Sheikh Ponda, kupitia kwa Wakili wake Juma Nassoro, aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya marejeo, akiiomba mahakama hiyo ifanye marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Maombi hayo yalitarajiwa kuanza kusikilizwa jana lakini, Serikali iliwasilisha pingamizi hilo la awali na hivyo mahakama hiyo ikalazimika kuanza kusikiliza pingamizi hilo kabla ya kuendelea na maombi ya msingi. Pingamizi hili liliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Bernard Kongola.

Wakili alidai kuwa hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo ni batili kwa kuwa ina kasoro za kisheria.

Alibainisha kasoro hiyo kuwa ni kutokuwa na tarehe ambayo kiapo hicho kilitolewa na kwamba hakuna mahali panapoonyesha kuwa msimamizi wa kiapo alikuwa akimjua mla kiapo na wala kueleza kuwa mla kiapo alitambulishwa kwake na nani.

Wakili Kongola alieleza kuwa hata kwenye hati ya kiapo iliyoko katika jalada lililoko mahakamani inaonyesha kuwa kuna kasoro hizo na kwamba walijiridhisha hivyo baaada ya kudurusu katika jalada hilo la mahakamani.

“Mheshimiwa Jaji, dosari hizi haziwezi kurekebishika, kwa hiyo maombi yote ni batili,” alisema Wakili Kongola.

Hata hivyo, Wakili wa Ponda, Nassoro alisema kiapo hicho ni sahihi na kimetimiza matakwa ya kisheria kwa kuwa nakala aliyonayo inaonyesha kiapo hicho kilitolewa na Oktoba 8, 2013 na kwamba, msimamizi wa kiapo alikuwa akimfahamu mla kiapo, ambaye ni Ubaidi Hamidu.

Pia wakili Nassoro alisema Serikali haijatoa ushahidi mahakamni kuonyesha kuwa kweli ilidurusu jalada la mahakama na kubaini kuwa hati hiyo iliyoko mahakamani ina dosari hizo wala kueleza ni lini alifanya hivyo hivyo.

Akijibu hoja hiyo Wakili Kongola alisisitiza kuwa kiapo hicho ni batili kama walivyojiridhisha kwenye jalada la mahakama, Novemba 21, 2013, na kwamba wanao ushahidi wa kutosha katika hilo. Baada ya kusikiliza hoja hizo, Jaji Rose Teemba anayesikiliza maombi hayo aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 11.

Sheikh Ponda sasa njiapanda - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Hata Mandela aliwahi kufungwa miaka takribani 27, kwa sababu za kutetea ndugu zake weusi. Sasa huyu anadhaliliswa kwa sababu ya kutetea Dini Ya Mwenyenzi Mungu. Hakika huyu ametuzidi wengi. Nina hakika moyo wake unaamani sana. Lakini hili sio la ajabu sana Duniani, kwani hata Mitume wa Mungu walikutana na Madhila kama hayo katika kutangaza na kulinda na kupambana na Maadui wa Mwenyenzi Mungu (WANAO HALALISHA POMBE, ZINAA NA USHOGA). Kama vile Nabii Yusuphu, Nabii Musa, Nabii Isa a.k.a Jesus, Yesu, Yehova, Mwana wa Mungu, Mungu etc.
 
jitanganye na mawazo yako ya ajabuajabu sheria lazima zifuatwe mkosefu yoyote akikosea lazima sheria imwandame bila kujali katoka dini gani dini isiwe kisingizio cha kufanya uharifu.
 
Unatumia makalio kufikiri eeeeee. ? Usrudie tena kumlinganisha Mandela na huyo kanjanja wako
 
Eti dini ya Mungu ,Mungu kila kitu ni chake lakini dini ni za wanadamu kwa sababu ukisema hivyo hata taarabu utasema ya mungu.
 
Unatumia makalio kufikiri eeeeee. ? Usrudie tena kumlinganisha Mandela na huyo kanjanja wako

Wanaotumia makalio kufikiri nadhani unawajua. Niwale wano halalisha Ndoa za jinsia moja kikatiba na nyumba za ibada. Need I elaborate???.
 
jitanganye na mawazo yako ya ajabuajabu sheria lazima zifuatwe mkosefu yoyote akikosea lazima sheria imwandame bila kujali katoka dini gani dini isiwe kisingizio cha kufanya uharifu.

Hilo sijakataa. Soma ujumbe wangu vizuri, usiwe kilaza.
 
Hata Mandela aliwahi kufungwa miaka takribani 27, kwa sababu za kutetea ndugu zake weusi. Sasa huyu anadhaliliswa kwa sababu ya kutetea Dini Ya Mwenyenzi Mungu. Hakika huyu ametuzidi wengi. Nina hakika moyo wake unaamani sana. Lakini hili sio la ajabu sana Duniani, kwani hata Mitume wa Mungu walikutana na Madhila kama hayo katika kutangaza na kulinda na kupambana na Maadui wa Mwenyenzi Mungu (WANAO HALALISHA POMBE, ZINAA NA USHOGA). Kama vile Nabii Yusuphu, Nabii Musa, Nabii Isa a.k.a Jesus, Yesu, Yehova, Mwana wa Mungu, Mungu etc.

wapi Mungu kasema ana dini?? uskurupuke mkuu somaga na maandiko vzr aisee uctuvuruge, ponda anatetea dini yake na yako shwaini ww!
 
Tuache na yote kosa lake linastahili dhamana,na mkicheza na katiba ipo siku yatakua ktk familia yenu,
 
wapi Mungu kasema ana dini?? uskurupuke mkuu somaga na maandiko vzr aisee uctuvuruge, ponda anatetea dini yake na yako shwaini ww!

DINI ni neon ambalo asili yake ni lugha ya kiarabu na mojawapo ya maana ya neon hilo ni njia mfumo wa maisha , utaratibu maalumu wa juu ya kuyaendesha maisha yetu hapa duniani, kwa muktadha huo sio sahihi kusema Mungu hana dini vinginevyo utakuwa umekosa kufahamu nini hasa maana ya dini. Ikiwa wewe unawawekea wanao utaratibu wa jinsi ya kuishi kwa sababu ni mkuu wa familia sio zaidi ya Mungu kuwawekea wanadamu aliowaumba mfumo wa kuishi hapa duniani? ikiwa mungu analo kusudio la kutuleta wanadamu hapa duniani iweje asiwape utaratibu wa kuyafikia malengo hayo? utaratibu huo ndio DINI. Watu wamejiwekea njia zao mbalimbali wakidai kwamba nazo zinalengo la kuwafikisha kwa Mungu lakini tujiulize ni sahihi kwa mwanao ajipangie utaratibu wake wa maisha akidai kwamba eti naye yeye anataka kuyafikia malengo ambayo wewe mzazi umeyakusudia?
 
Hata Mandela aliwahi kufungwa miaka takribani 27, kwa sababu za kutetea ndugu zake weusi. Sasa huyu anadhaliliswa kwa sababu ya kutetea Dini Ya Mwenyenzi Mungu. Hakika huyu ametuzidi wengi. Nina hakika moyo wake unaamani sana. Lakini hili sio la ajabu sana Duniani, kwani hata Mitume wa Mungu walikutana na Madhila kama hayo katika kutangaza na kulinda na kupambana na Maadui wa Mwenyenzi Mungu (WANAO HALALISHA POMBE, ZINAA NA USHOGA). Kama vile Nabii Yusuphu, Nabii Musa, Nabii Isa a.k.a Jesus, Yesu, Yehova, Mwana wa Mungu, Mungu etc.

Mungu akuzidishie ndugu,,hongera sana kwa kulitambua hilo!!
 
wanamwonea tu ...
ukiwa muislam unatakiwa unyamaze ....ukisema sema sana basi ujue mfumo utakuonesha kuwa upo...
haya ni maonevu tu...yote ni uzushi na kesi za kubambikiwa..na mapolisi wetu.....kwa kupata presha ya wanasiasa na vingozi wa dini....
 
Hata Mandela aliwahi kufungwa miaka takribani 27, kwa sababu za kutetea ndugu zake weusi. Sasa huyu anadhaliliswa kwa sababu ya kutetea Dini Ya Mwenyenzi Mungu. Hakika huyu ametuzidi wengi. Nina hakika moyo wake unaamani sana. Lakini hili sio la ajabu sana Duniani, kwani hata Mitume wa Mungu walikutana na Madhila kama hayo katika kutangaza na kulinda na kupambana na Maadui wa Mwenyenzi Mungu (WANAO HALALISHA POMBE, ZINAA NA USHOGA). Kama vile Nabii Yusuphu, Nabii Musa, Nabii Isa a.k.a Jesus, Yesu, Yehova, Mwana wa Mungu, Mungu etc.

Kwani huyo gaidi hajanyongwa tu?
 
wanamwonea tu ...
ukiwa muislam unatakiwa unyamaze ....ukisema sema sana basi ujue mfumo utakuonesha kuwa upo...
haya ni maonevu tu...yote ni uzushi na kesi za kubambikiwa..na mapolisi wetu.....kwa kupata presha ya wanasiasa na vingozi wa dini....

waumini wa subuana siku zote wamekua ni chanzo cha migogoro..magaidi hoyee!
 
Back
Top Bottom