Sheikh Ponda na wenzake wasisitiza waislam kugomea sensa!

Status
Not open for further replies.

...lol! walipojaribu kulivua likawa linachukua na ngozi ya mwili

Kilimo Kwanza...hadi hii leo sijaona lolote jipya katika sekta ya kilimo nchini na kauli hii ilitolewa zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Na hutakaa uone lolote jipya BAK ......kilimo kwanza wanasema wakiwa wamekaa kwenye viyoyozi ......waulize lini walienda mashambani kufanya kilimo kwanza kwa vitendo?......au wamefanya juhudi gani kuwawezesha hao wakulima?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwanini iwe sisi tu kuja kwenye hospitali za wakristo tunazochangia pamoja fedha.Tunataka na nyinyi mje kuhukumiwa kwenye mahakama ya kadhi pia mkiona mahakama hizi hazitoi haki.

Mlijenga nyie hizo hospitali?.......jengeni na nyie hospitali zenu sio mnalumbana vitu havina maana!
 
Na hutakaa uone lolote jipya BAK ......kilimo kwanza wanasema wakiwa wamekaa kwenye viyoyozi ......waulize lini walienda mashambani kufanya kilimo kwanza kwa vitendo?......au wamefanya juhudi gani kuwawezesha hao wakulima?

Change ya Rada ($46 miilion or equivalent to 29.5 million pounds) walidai itaelekezwa kuboresha sekta ya Elimu lakini hadi hii leo hakuna chochote kilichoboreshwa. Sekta hiyo bado iko hohehahe. Sijui peza zile wamezifanyia nini.
 
Kwa hili suala sensa kuna mambo ya kutafakari upya:1.CCM wamekuwa wanaendekeza Udini ktk kutafuta Utawala 2.CCM ndio walioweka kipengele cha kadhi Kwenye ilani CCM 3. Leo waislam wamempiga kijembe Jk wakisema liwalo na liwe hatushiriki Sensa.CCM wapo tayari kumusikiliza Kanumba na kufadhiri msiba wake lakini hawako tayari kuwajali waislamu.4.Jk alisema uchaguzi 2010 kulikuwa na udini akimaanisha kuwa alipigiwa kura na Waislam sasa iweje leo?
 
Hehehehe wamemalizia kujenga majumba yao ya kifahari! Chezeiya wezi wa ccm wewe!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Change ya Rada ($46 miilion or equivalent to 29.5 million pounds) walidai itaelekezwa kuboresha sekta ya Elimu lakini hadi hii leo hakuna chochote kilichoboreshwa. Sekta hiyo bado iko hohehahe. Sijui peza zile wamezifanyia nini.
Zinatumika kama matumizi kwenye jopo la Mashehe na serikali kuanzisha Mahakama ya Kadhi na tayari Kadhi mkuu na Makadhi wa Mikoa wamekwisha teuliwa
 
Kuna siku haya yote yatafikia mwisho na Watanzania kuchukua nchi yao toka mikononi mwa mafisadi. Itakuwa kama kuupata uhuru wetu kwa mara ya pili. Siku hiyo Watanzania wengi katika kila kona nchini watalia machozi ya furaha na kusema hatimaye tumeikomboa nchi yetu.

Zinatumika kama matumizi kwenye jopo la Mashehe na serikali kuanzisha Mahakama ya Kadhi na tayari Kadhi mkuu na Makadhi wa Mikoa wamekwisha teuliwa
 
Udini upo Bungeni, Mahakamani, Ikulu, Gerezani, vituo vya polisi, Hosipitalini. Wabunge wana apishwa kwa dini, Ikulu wana apishwa kwa dini , Mahakamani watu wanaapa kinyume na torati,
 
Hata wanaowahesabu raia wetu ni Waislamu na wapo Wanachama wa CUF, kwa hiyo sioni ugumu wa kuwahesabu huko walikolala, iwe Majumbani, au Misikitini
Serikali haishindwi kwa hili, tukutane baada ya Sensa mtamsikia huyo Lipumba Mtaalam wa Uchumi asiyetaka Data kamili atasemaje?
 
CCM wanatawala kwa Udini ,Wanalazimisha watu kuapa Mahakamani wakati ni Kinyume na bible,Wafungwa mahabusu na wanafungwa kwa misingi ya dini! polisi wanahoji dini na kabila , mahakama wanahoji dini na kabila .Lakini CCM haohao wanakuwa wa kwanza kusema Cdm kuna udini!
 
Kwa hili suala sensa kuna mambo ya kutafakari upya:1.CCM wamekuwa wanaendekeza Udini ktk kutafuta Utawala 2.CCM ndio walioweka kipengele cha kadhi Kwenye ilani CCM 3. Leo waislam wamempiga kijembe Jk wakisema liwalo na liwe hatushiriki Sensa.CCM wapo tayari kumusikiliza Kanumba na kufadhiri msiba wake lakini hawako tayari kuwajali waislamu.4.Jk alisema uchaguzi 2010 kulikuwa na udini akimaanisha kuwa alipigiwa kura na Waislam sasa iweje leo?
 
Hata wanaowahesabu raia wetu ni Waislamu na wapo Wanachama wa CUF, kwa hiyo sioni ugumu wa kuwahesabu huko walikolala, iwe Majumbani, au Misikitini
Serikali haishindwi kwa hili, tukutane baada ya Sensa mtamsikia huyo Lipumba Mtaalam wa Uchumi asiyetaka Data kamili atasemaje?

data kamili za waislamu,wakristu au wapagani tutazipataje bila kipengele cha dini?
 
kuhusu hili swala sensa serikali ilitakiwa kuliangalia kwa marefu na mapana lakin hawa wanaopinga nadhani kuna nguvu fulani ipo mahali inawasukuma kufanya haya mambo ndiyo maana wanajiamini sana kumbuka hii hali ilianza wakati wa awamu ya pili awamu ya tatu ikatulia lakini awamu hii imezidi sana na sijui tatizo litakuwa wapi?
 
hili suala lijadiliwe kwa uwazi.serikali inatakiwa kueleza sensa ni nini na inasaidia nini.pia ieleze kwa nini kipengele cha dini hakipo,madhara na faida ya kipengele hicho yawekwe wazi na sio kubisha na kutisha tu.Je serikali itakapotoa takwimu zake za dini mbalimbali nchini zitatoka wapi?unapoingia chuoni au kazini kuna kipengele kinachoulizia dini yako sasa ni sababu ipi inayoifanya serikali ikatae kuweka kipengele hiki kwenye sensa?hivi leo hii akajitokeza mtu akasema idadi kubwa ya watanzania ni wapagani tutabisha au kukubali kwa takwimu zipi?
Kwa nini tumekubali kuwa na masomo ya dini mashuleni?kwa nini tunapumzika siku za idd na christmas wakati hatujui kama wengi wa watanzania hawana dini?tunaposema jumapili au ijumaa iwe siku ya mapumziko tunaongozwa na takwimu zipi?
Naamini kuna wasomi wanafanya utafiti juu ya makabila,lugha,dini au utamaduni wa watanzania je watapata vipi takwimu za mwanzo za tafiti zao?
Nasisitiza ni vyema serikali ikatoa maelezo ya kina na sio simple NO!

Kama nia halisi ni kujua idadi ya waumini wao. Ni jambo rahisi sana, wanaweza kufanya hivyo kwa kuweka rejista misikitini au kwa kuwatumia viongozi wao wa dini kwenye ngazi za mitaa/vijiji. Pia Kila mtaa waislam wanafahamiana, kama ilivyo kwa wakristo wa madhehebu mbali mbali.

Kwa mfano inapotokea msiba unomhusisha muislam wanakuwa tayari wanajua kuwa huyo mhusika ni muislam na taratibu za mazishi zinakuwa kwa mujibu wa dhehebu husika. Kama hilo linawezekana inashindikana vipi kujua idadi ya waumini wao?.

Kwa hiyo hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi kupinga sensa, badala yake wangejihesabu wenyewe wakawa na takwimu zao.

Mfano mwingine, wakatoliki wanayo rejista kwa kupitia rejista za jumuia ndogo zilizopo kwenye mitaa/vijiji, rejista hizo hutumiwa na kanisa kujua idadi ya waumini (walio active na ambao sio active).

Kwa hiyo hata waislamu Wanaweza kutumia utaratibu huo bila kupoteza muda wao.

Hata wakisusia sensa haitawasaidia kujua idadi ya waumini wao kwa hiyo tatizo litakuwa halijatatuliwa.

Serikali haiwajibiki kufanya sensa ya waumini kwa sababu haifanyi mipango yake kwa kufuata imani za watu.

Iwapo viongozi wa waislam ndio hao wanaotegemewa wanafanya ushawishi wa aina hiyo wataendelea kudumaza maendeleo ya waislamu na wataendelea kulalamika huku wenzao wanasonga mbele.
 
kwanini kuna watu huwa wanapenda kupinga hata kama jambo halimuhusu...waislam walipotaka mahakama ya kadhi kwa ajili yao watu walipinga...leo kadhi yupo na hiyo vita hatuioni wala nn!
Leo wanataka kipengele cha dini kiwepo, wengine waliozoea kupinga wanapinga! nendeni mkahesabiwe pekeyenu mimi sitaki tuonei kama mtapata majibu ya ukweli...agrrrr!
 
wakitaka kujua wako wangapi waangalie ni wangapi watakao enda kujificha misikitini... a very simple arthmetic

NIMEFURAHI SANA HII YA LIPUMBA.......

sawa ukishapata waliojificha ukaongeza na waliojitokeza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom