Sheikh Ponda na wenzake wasisitiza waislam kugomea sensa!

Status
Not open for further replies.
Ndg mi simwelewi rais wetu kwa hili sijui kwa nini analilea,tutajuta hebu angalia baadhi ya magazeti na redio zinavyochochea chuki miongoni mwa wa tz jamaa kauchuna tu!!,sijui ndio utawala bora!.

hata tamko la polisi anatoa chagonja. Kova na said mwema wako kimya. Hawa ni watu waliokuwa wakitoa sana matamko kwenye sakata la madaktari,walimu na mikutano ya cdm. Naona wameamua kuupandikiza udini wazi wazi.
 
kuwa mwanadiplomasia? Yaani unajua kabisa watu wanavunja sheria na unakuwa mwanadiplomasia? Only in this govt, but with Mwinyi, or Mkapa, this nonsense could have not happened!!

kuna wapuuzi wanatafsi vibaya neno diplomasia. Wao kila kitu wanataka diplomasia, mpaka wa malawi diplomasia upuuzi wa waislamu diplomasia, huu upumbavu ukiendelea kuendekezwa hatufiki popote!
 
Jamani mbona mnapenda kumbebesha mzigo Baba wa watu,Hivi si alisha lizungumzia hilo suala ya kuwa watu wasitumie Uhuru wao wa maoni vibaya,vile vile hilo suala akaliacha kwenye vyombo husika na ushahidi upo wa wale wachochezi kukamatwa,Stilll zoezi la kuhesabiwa linaendelea na Waislamu wengi tu wamehesabiwa bila ya kikwazo.Je ndugu yangu ulitaka usikie Sheikh Ponda ameokotwa akiwa hoi,Natumai wewe ndio utakuwa wa kwanza kulamika tena Ya kuwa Babu yake Aziza anatumia Mkono wa chuma kunyamazisha watu.Jaribu kuwa na utamaduni wa kufikiria vitu kabla ya kuongea,kwa vile akili yako umei tune imchukie fulani basi hata akinywa maji kwenye glass ya mvinyo unalalama.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom