#COVID19 Sheikh Ponda Issa Ponda aunga mkono waraka wa KKKT na Kanisa Katoliki kuhusu kujikinga na Corona

View attachment 1702454

Sheikh Ponda ambaye ni miongoni mwa Masheikh wanaoheshimika sana na Waislam wa Afrika kutokana na kupigania haki za Waislam bila uoga amesema Juhudi za Makanisa kuwaelekeza waumini wao njia bora za kujikinga na Corona haziwahusu waumini hao pekee, bali zinawahusu wananchi wote wa Tanzania.

Amewaasa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona .

Chanzo: MwanaHalisi Digital
Mbona bado msikiti anaoswali watu wamejaa pomoni? Angepiga marufuku wasiswali aone kama hajabaki peke yake. Kila nafsi itaonja mauti akiwemo na yeye, wewe na mimi! TUSITISHANE!!!
 
Mbona bado msikiti anaoswali watu wamejaa pomoni? Angepiga marufuku wasiswali aone kama hajabaki peke yake. Kila nafsi itaonja mauti akiwemo na yeye, wewe na mimi! TUSITISHANE!!!
😆😆😆 Hakuna anayekutisha ila tambua kwamba kule makumbusho wanakochomea mabohora na wahindi foleni ya kuchoma imefika barabarani
 
Jumuiya anayodai kuiwakilisha ilishamkana kitambo!!! ...
Ni mawazo yake binafsi, na ya chama chake cha siasa alichojinasibisha wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Lakini kama Mtanzania ana haki ya kutoa mawazo yake wakati wowote anapojisikia, ingawa alichokinena hakina upy !.
Jumuiya ipi iliyomkana Ponda ?
 
Back
Top Bottom