Sheikh Ponda Issa Ponda amkubali Rais Magufuli

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,083
image.jpg


- Sheikh Ponda amkubali JPM
- Amuunga mkono urudishaji mali za Waislam
- Amuomba kuingilia kati zuio la mikutano ya kisiasa.

Ni miongoni mwa dondoo zilizopo kwenye gazeti la Majira. Hakika Rais Magufuli anakubalika kwa kila makundi ya kijamii

==========

SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kuahidi kusaidia kurudisha mali ambazo Waislamu wamenyang’anywa au kurubuniwa,

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibuka na kusema anamuunga mkono Rais katika hatua hiyo huku akimtaka kukaa na jumuiya yao ili washauriane juu ya mahitaji yao ya msingi.

Sheikh Ponda, ambaye alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Nipashe jana, alisema Rais Magufuli ameonyesha moyo wa kusaidia dini hiyo kwa kitendo chake cha kutoa fedha za kusaidia wanaokwenda hija.

Alimshauri Rais sasa kukaa na jumuiya yao ili asaidie maeneo ya kipaumbele kama elimu na afya, baada ya kutoa mchango kwa watu wanaokwenda kuhiji.

“Jana (juzi) nimeona ametoa hela kusaidia wanaoenda hija, lakini ukweli ni kwamba Jumuiya ya Waislamu ina mambo ambayo ni vipaumbele, mambo kama ya afya na elimu ambayo itakuwa vizuri tukae tuone ni namna gani atakavyotusaidia,” alisema Ponda.

Alipoulizwa kama haoni kwamba Rais anasimamia mambo hayo mawili kwa ngazi ya taifa, Ponda alijibu; “Ukiangalia wenzetu Wakristo wana hospitali na shule, na sisi pia tunayataka hayo mambo kwa hiyo ingekuwa vizuri kama tukishauriana naye ili aone namna ambavyo ataweza kutusaidia.”

Akizungumza kwenye Baraza la Idd El Fitr, juzi jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema anafahamu kwamba wapo baadhi ya watu wenye mali ambao huwatumia viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwarubuni kwa kuingia nao mikataba mibovu na hatimaye mali za baraza hilo hupotea.

“Mtu anakuja na kuwadanganya danganya katika kiwanja chenu eti atajenga kituo cha mafuta, ambako mngejenga msikiti. Kwani kituo cha mafuta na msikiti wapi na wapi, kipi bora?" alihoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliitaka Bakwata kutumia wanasheria wake kuhakikisha mali hizo zinarudishwa na kuwaonya wasiingie mikataba mibovu ambayo inasababisha migogoro.

“Serikali inapenda kuona mali za waislamu zinarudi mikononi mwa waislamu na mali za wakristo zinarudi mikononi mwa wakristo,” alisema Rais Magufuli.

Kutokana na kauli hiyo, Sheikh Ponda, ambaye amekumbana na misukosuko mingi na vyombo vya dola katika miaka ya karibuni, alisema: “Kauli ya Rais inaonyesha namna anavyojali wananchi, suala hili limeniponza kuwa na kesi mahakamani kwa miaka miwili mpaka nikashinda na sasa Rais amekuja na kauli hii, kwa kweli tutaamunga mkono.”


Chanzo: Nipashe
 
"Icons" za Taifa this term zitachokonolewa ili mradi tu zitoe neno lenye positive attitude juu ya Rais then liwe ndiyo front bolded heading katika magazeti ya "chama".

Ponda hakuwa kuukataa au kutoukubali uongozi wa awamu zingine ila HAKI ndiyo imekuwa ikimkataa Ponda (Ponda vs Right). Between the line katika hiyo habari bado utaona Ponda anapambana tena vs haki ya kikatiba ya shughuri za kisiasa (mikutano).

Ijumaa Karim....
 
"Icons" za Taifa this term zitachokonolewa ili mradi tu zitoe neno lenye positive attitude juu ya Rais then liwe ndiyo front bolded heading katika magazeti ya "chama".

Ponda hakuwa kuukataa au kutoukubali uongozi wa awamu zingine ila HAKI ndiyo imekuwa ikimkataa Ponda (Ponda vs Right). Between the line katika hiyo habari bado utaona Ponda anapambana tena vs haki ya kikatiba ya shughuri za kisiasa (mikutano).

Ijumaa Karim....
Kisha mpongeza tayari, hayo mengine ni yako na una sababu zako.
 
Kisha mpongeza tayari, hayo mengine ni yako na una sababu zako.
Mkuu
Facts hukaa mbali na light politics. Katika kupongeza hapo hapo pia ameonyesha kukosoa juu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa of which ni haki ya kikatiba.
Kwa nini mnakuwa na mioyo migumu ya kushindwa kuguswa na uvunjifu wa katiba unaoendelea ? I bet unayatazama masuala kwa jicho la political sentiments na siyo kwa ukweli wake. Unafiki uwe na kiwango
 
Hivi kati ya Magufuli na Sheikh Ponda nani kamkubali mwingine. Kwa uelewa wangu mheshimiwa raisi kamuunga mkono mpambanaji Sheikh Ponda na kawaumbua wanafk bakwata na wanaowaunga mkono. Wasisi wetu ni juu ya utekelezaji wa tamko hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom