Sheikh Ponda: Hali ni mbaya sana, mauaji ya kutisha yanaendelea nchini na Serikali ipo kimya



Sheikh ponda ametoa wito kwa jamii na kwa rais magufuli na kusema kuna mauaji ya kutisha yanaendelea nchi hii na kusema upo umuhimu wa mamlaka nyingine kama bunge kushughukikia suala hili na sio kuiachia serikali pekee

Amesema kwa sababu hali ni mbaya sana ipo haja ya kuunda tume huru ya bunge
Ameonyesha habari iliyoandikwa na gazeti la Nipashe ya miili ya watu 15 kukutwa kwenye viroba baharini na walioua hawajulikani hii ni ishara kuwa hali ni mbaya

Pia ameziasa taasisi za kutetea haki za binadamu kukemea hali hii

Amesema waliopotelewa na ndugu watoe taarifa polisi na kwa viongozi kama wao


Ndugu zetu askari polisi walipokua wakiuwawa kila uchao, mbona hakuna tume ya haki za binadamu wala huyo Ponda kujitokeza kusema lolote. Tulieni sindano iwaingie kwanza....na sasa hivi Kibiti kimyaaaaaa....***** ngoja tuheshimiane kwanza
 
Akili Tupi ni ya kwako we mburura. Huwezi kujiuliza hapo doti kwamba ni lini Ponda akawa mtetezi wa haki za binadamu? Je Ana uhakika kuwa waliouawa ni waislamu? Kama ni waislamu, ni wa maeneo gani na alijuaje? Je Hana mahusiano nao?
Usisahau ni kiongozi wa kiroho ana dhima kubwa juu ya salama ya nchi hiii anapaswa kuijenga jamii katika mitazamo chanya

Labda una chuki kwa kuwa msemaji wa ushauri ni ponda mvaaa kanzu na kofia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo gazeti aliloshikilia ni mali ya nani? aliyeandika hiyo habari ni nani? Sheikh anaposema waliopotelewa ndugu zao waende wakatoe taarifa kunakohusika anamaanisha nini? ama hujamsikiliza vema?
Hayo majitu yana roho mbaya kuliko shetani unadhani wana haja na hayo yamelenga chuki zao kwa ponda tuuu hawana haja na maneno yake hats kama yangekuwa mazuri kwa kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wote wa dini wamekuwa kimya kuhusu hofu kubwa iliyotanda nchini. Kupotea kwa Watanzania katika mazingira ya kutataninsha, bomoa bomoa isiyo na fidia, chuki za kutisha nchini. Huyu angalau anajitahidi kutamka hadharani mambo haya yaliyoleta hofu kubwa nchini. Hongera Sheikh Ponda kwa juhudi zake,
 
Kwa kweli katika hili nampongeza sana shehe Ponda. Nawashangaa sana maaskofu wetu kwa kimya hiki dhidi ya mamlaka kwani ndio yenye dhamana ya ulinzi wetu.
Hivi zile sala za kumuombea mkuu Wa mamlaka ni kwa ajili ya haya yanayotokea na kuhusishwa chinichini na hayo mamlaka? Maana wakati mwingine kimya ni sawa na kusema ndio.
Viongozi wangu Wa kikristo wanapotea njia

Ningependa utufahamishe.
Shekh Ponda ni NANI na anawakilisha kundi gani katika jamii?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S
Yaaaani Weeweeeeee, kwa hili Ponda yuko sahihi 100%

Akina Ben Saanane wamepotezwa kijinga jinga tu. Roma Mkatoliki mwanamuziki naye aliambiwa ataachiwa mwaka 2030

Mi nafikiri wanaompinga Ponda kwenye hili wanafurahia ushetani wa hawa mashetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
si tuliambiwa Roma atapatikana kabla ya DOMINICA na akapatikana?, huyo aliyemwambia kuwa atapatikana 2030 ni nani?, tusaidie tumjue ili tumuepuke
 
Rudi darasani we we mwenyewe ushafaham anaitwa shekh unauliza non hapo achadharau walikuwepo kwenye viburi kuliko wewe
mueleweshe aelewe, ponda si maarufu au muhim kihivyo mpaka kila mtu amjue na amchukulie utakavyo wewe, sheikh ponda ni mchumia tumbo asiyejua asemacho
 
Rudi darasani we we mwenyewe ushafaham anaitwa shekh unauliza non hapo achadharau walikuwepo kwenye viburi kuliko wewe
Sijui ni nini kipo nyuma ya povu lako. Actually lengo langu lilikua Ni moja tu.
Wote wenye ujasiri WA kumkosoa Mkuu ni wale ambao hawana affiliation na utawala huu. Kwa ufahamu wangu, Shekh Ponda ni mmoja wao.
Taasisi zote zenye mahusiano chanya na serikali haziwezi thubutu kukosoa. kwasababu ya urafiki watamuonea aibu mkuu kumueleza. Kwahiyo "wanaokosoa hawana cha kupoteza."



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni aibu kwa wanadamu hasa Mkristo tunaofundishwa kila kukicha kupendana na kuchukia kumwaga damu tunashabikia mauaji ya binadamu wenzetu. Kumbukeni AMRI kuu tuliachiwa na Bwana wetu Yesu Kristo.
 
Huyu Sheikh abanwe aseme vizuri, itakuwa anawajua waliouawa na aseme kwa nini ana uhakika kuwa maiti zimetoka upande wa Tanzania Wakati zimekutwa baharini? Kwani bahari ipo Upande wa Tanzania tu?
Kuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kupambanua mambo Tz ingekuwa ya mwisho duniani kwa wenye IQ ndogo. Unawezaje kumkamata msoma gazeti kwa kile kilichoandikwa gazetini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom