Sheikh Ponda atoa ujumbe mzito

Sep 19, 2019
43
383
Shuura ya Maimamu Nchini kwa kushirikiana na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, imeandaa Baraza la Eid lililofanyika katika Ukumbi wa ......uliopo katika Masjid Mtambani Kinondoni-Dar es Salaam.

Baraza hilo limehudhuriwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu na Masheikh mbalimbali. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na Tathmini ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan na jinsi ilivyofikiwa Malengo yake. Mada hiyo imewasilishwa na Sheikh Iddi Jengo (Muhadhiri wa Chuo Cha MUM) akisisitiza MABADILIKO na Kuimarisha Mahusiano.

Mada ya Pili; Sheria ya UGAIDI na Athari zake kwa Jamii ya Waislamu. -Msomi Wakili Mashaka Ng'ole. Ambaye amezungumzia Sheria ya Elimu Nchini ya mwaka 2016. Sheria ya Usajili Nchini (RITA), Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 na mapungufu ya Sheria hizo.

Pia amezungumzia Sheria ya UHUJUMU UCHUMI NA SHERIA YA UGAIDI.
Sheria hizi zimekuwa mbaya na Kali mno na SHERIA hizo zimeshindwa kutafsiriwa kueleza tafsiri halisi ya nini UGAIDI na nani ni Gaidi? Pia SHERIA ya utakatishaji wa fedha. Pia imekosa tafsiri sahihi. Kuna mtu ameshtakiwa kwa tuhuma za kutakatisha fedha kwa kosa la kumtoa mimba mwanamke.
Ametoa wito kwa Jamii ya Kiislamu kuchukua hatua sahihi kuzinasihi mamlaka husika kufanya maboresho ili Jamii yetu iwe na ustawi kwema, Haki, usawa na Amani.

Mwisho; Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini Sheikh Ponda ISSA Ponda ambaye ametoa ujumbe na salamu za Eid pamoja na mambo mengine alisisitiza nukta zifuatazo;

1. Kuna haja na ulazima wa kuwa na Uongozi wa nchi unaozingatia mfumo wa Utawala Bora na serikali Adilifu.

2. Kuna haja serekali kujipanga na kurudisha mchakato wa Katiba mpya ambao uliachwa na Serekali ya awamu ya nne ukiwa katika hatua za mwisho. Mchakato huo umevurugwa na wana siasa waio jali maoni ya wananchi.

3. Katika kipindi hiki cha mpito Serekali ianzishe mchakato wa kuunda tume huru ya Uchaguzi itakayo simamia chaguzi zijazo na kuhakikisha zina kuwa chaguzi huru na za haki.

4. Bunge la Tanzania lipitie upya Sheria kandamizi na za kibaguzi kama Sheria ya Kuzuia na kupambana na Ugaidi, Sheria ya uhujumu uchumi na Utakatishaji Fedha.

5. Tunaishauri Serekali kuzingatia weledi katika teuzi katika nafasi za kisera. Na kujiepusha na teuzi kwa kuzingatia itikadi za vyama, dini, kabila nk.
 
Mitizamo ya waislam objective inavutia sana. Wana mitazamo ya haki na uhuru iliyojaa hekima sana.

Linganisha huyu hata na Gwajima:

No wonder marais waislam kwa ujumla hapa kwetu wamekuwa bora zaidi.
 
Back
Top Bottom