Sheikh Ponda amwandikia barua Waziri Mwigulu kutaka maelezo ya mauaji

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Kufuatia mauaji yanayoendelea na hasa kufuatia mauaji ya kijana Salum Mohamed Kurasini hapo jana, Sheikh Ponda Issa Ponda amemwandikia Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ujumbe ufuatao na kuhitaji kauli ya serikali juu ya mauaji haya.
----------------

Mheshimiwa Waziri Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, nakusalimu sana. Pia nakutakia ufanisi katika kulitumikia Taifa.

Baada ya hayo ninayo haya ya kusema.

Katika baadhi ya hafla nilizohutubia hivi karibuni, nilitumia fursa hiyo kueleza masikitiko yangu kwa mauwaji ya askari Polisi zaidi ya watano waliouliwa na watu wasiojulikana hivi karibuni Mkoani Pwani. Natumia fursa hii pia kwako kutamka hivyo.

Aidha jana tarehe 14 Mei, 2017, nilipokea taarifa ya kijana Salum Muhamed Almasi aliyeuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na Polisi majira ya saa 3:00, na saa 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam akiwa anatembea barabarani kwa miguu. Taarifa ya Polisi ni kuwa kijana huyo ni jambazi aliyetaka kupora fedha.

Nimekutana na familia ya Marehemu ambaye ni mzaliwa wa Kilwa, familia inamtambua kuwa ni kijana mwema kabisa. Nimeongea na baadhi ya wakazi wa Kilwa, wao pia wanamtambua kama mtu mwema kwa tabia na anayeshiriki ibada Msikitini ipasavyo.

Salum Mohamedi pia ni Imamu Msaidizi katika moja ya Misikiti Kurasini.

Maelezo ya ziada Salum muda mwingi ni mtu wa masomo. Amemaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne, cha Tano, Kidato cha Sita na mpaka anauwawa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya Diploma fani ya ICT Network.

Mh. Waziri mauwaji kama haya yanazidi kupambamoto Tanzania na yanachafua haiba ya Taifa. Gazeti la Mwananchi la Mei 6, 2017, lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho "WALIOUWAWA RUFIJI WAFIKIA 29".

Jambo la kuzingatiwa ni kwamba kwa utaratibu huu unaoshamiri, Wananchi wanaouliwa ndugu zao au jamii kwa ujumla wanapoteza haki ya kujuwa ndugu au raia wenzao ni wahalifu kweli au wanauwawa kwa sababu nyingine?

Utaratibu wa nchi hii uliowekwa, ni mtu kuadhibiwa kwa kufungwa, kutozwa faini, kuachiwa huru au kuuwawa baada ya kuthibitika kosa na kuhukumiwa.

Utaratibu huo ni wa kitaalamu/kisheria na ndio unaotumika katika Serikali zote bora duniani. Sisi tumeshuhudia ulivyotufikisha katika Taifa (Tanzania), lenye utulivu na mahusiano mazuri kwa kiasi fulani kati ya Jamii na vyombo vya Dola. Vilevile umetufikisha katika Taifa la kistaarabu lisilofurahishwa na umwagaji wa damu kiholela.

Ni vizuri Serikali ikatoa tamko la kufafanua sababu inayopelekea watu wengi kiasi hicho kuuwawa bila ya kufikishwa Mahakamani.

Nimalizie kwa kusema, ikiwa mfumo wa nchi tuliourithi wa Mahakama, Bunge na Serikali una upungufu, basi busara ni kuuboresha na sio kuuhama na kuanzisha utaratibu mwingine kinyemela.

Natanguliza shukrani nikiwa na matumaini kuwa haya niliyoyazungumza yatazingatiwa.

Ahsante,

Sheikh Ponda Issa Ponda.


Source: Tanuru la fikra
 
Duuu...shekh Ponda anataka kuhamishia mishe mishe zake Pwani na kibiti..?
 
police brutality imezidi kutia fora nchini hawa askari sijui wanapata kiburi wapi cha kutofuata sheria labda sbb kubwa kuwa illiterate.technically kazi polisi ni kuundoa uhalifu na sio kuua wahalifu tena kwa kushuku tena unaua mtu unarmed point blank range
 
police brutality imezidi kutia fora nchini hawa askari sijui wanapata kiburi wapi cha kutofuata sheria labda sbb kubwa kuwa illiterate.technically kazi polisi ni kuundoa uhalifu na sio kuua wahalifu tena kwa kushuku tena unaua mtu unarmed point blank range
Ulikiwepo eneo la tukio, au ndio mwendo wa kuandika tu, sababu bundle bwelele???
 
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislaam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ameitaka Serikali kutoa tamko litakalofafanua sababu inayochangia watu kuuawa bila ya kufikishwa mahakamani huku akionyesha masikitiko yake juu ya mauaji ya Salum Mohamed Almasi, eneo la Kurasini jijini Dar es salaam juzi.

Sheikh Ponda alisema endapo mfumo wa nchi hii katika mahakama, Bunge na Serikali una upungufu, busara ni kuuboresha utaratibu mwingine kinyemela.

Sheikh alitoa kauli hiyo jana kupitia barua yake aliyoithibitisha katika gazeti hili, kwamba, amemwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, akihitaji kauli ya Serikali juu ya mauaji yaliyofikia idadi ya watu 29 mkoani Pwani.

"Barua tulimtumia jana (juzi), kwa njia ya mtandao na akajibu kwamba, ameshapokea na ameisoma. Sisi tunataka kuisadia Serikali na Taifa kurejea katika hali nzuri, ninaamini kabisa Jeshi la Polisi likitumia wananchi linaweza kupata taarifa sahihi", amesema huku akiishauri Serikali kufuata mfumo sahihi katika kushughulikia matukio ya uharifu nchini.

Waziri Mwigulu alipopatikana kwa njia ya simu alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno akisema asingeweza kuzungumza kwa kuwa alikuwa katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.


Chanzo: Mwananchi
 
hili tatizo lina amsha hasira miongoni mwa watu wa imani fulani jambo ambalo si jema kwa hapo baadae
 
Sheikh ponda ndo kiongozi wangu nnayemkubali sana,Mimi ni mmoja wa waathirika wa operesheni ya poliso wao wameniibia Mali zangu dukani.Hawa polisi huku wanafanya uporaji tu hawasaki majambazi.kuhusu wa kurasini kama Yule jamabazi hapo simuungi mkono ,by the way sheikh ponda azungumzie kamatakamata ya madrasa huku kwetu.je serikali inapambana na uislam
 
Polisi wetu hawana ujuzi wa kazi yao, Mfano mzuri ni tuikio la Jana la Kigoma Malima. Askari mwenye mafunzo sahihi hawezi kurusha marisasi hovyo hovyo namna ile mahala ambapo hata hakuna mwenye silaha hata Jiwe tu.
 
Back
Top Bottom