Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,847
- 30,185
Binadamu anapokata tamaa ya kupata Haki, Kisa cha Anerigo Bonasera na Don Veto Corleone. Mfano wa Sheikh Ponda.
Katika kitabu cha "The Godfather," kuna watu wawili muhimu katika kueleza nini binadamu hufanya anapodhulumiwa na jamii na watoa haki wakamdhulumu pia.
Amerigo Bonasera kazi yake ni "undertaker," yaani kutayarisha maiti kwa ajili ya maziko.
Kazi hii ilimpa maisha mazuri katika mji wa New York ya baada ya vita ya pili ya Dunia.
Amerigo Bonasera alikuwa na mtoto mmoja binti aliyempenda sana.
Huyu binti akachukuliwa na vijana wenzake wa kiume kwa matembezi kumbe ndani ya nafsi zao walikuwa na lao jambo.
Wakamlewesha kwa nia ya kumbaka.
Huyu binti alikuwa bikra na hakukubali kuvunjiwa heshima yake na wale wahuni washenzi.
Akapambana na washenzi wale na kuishinda azma yao lakini walimuacha uso wake uliokuwa mzuri umevurugika kwa kuumizwa vibaya sana.
Kesi ikaenda mahakamani.
Hawa vijana ni kutoka familia kubwa zenye satwa baba zao wakazungumza na hakimu wale vijana mahakama ikawatia hatiani lakini hukumu ikawa "suspended," yaani hawatatumikia kifungo kama sheria inavyotaka.
Amerigo Bonasera na mkewe wakatoka mahakamani vichwa wameinamisha wanabubujikwa na machozi kwa dhulma waliyofanyiwa na mahakama.
Wale washenzi na wazazi wao wakiwa wamesimama nje ya jengo la mahakama wakawa wanamtazama Amerigo Bonasera na mkewe huku wanacheka wamefurahishwa na hukumu aliyotoa hakimu.
Amerigo Bonasera akamwambia mkewe, "Twende kwa Godfather tukatafute haki yetu."
Godfather Don Veto Corleone akaisikiliza kesi ya Amerigo Bonasera kisha akamuuliza, "Umekwenda polisi na haki yako umepewa."
Hapa kuna mengi baina ya watu hawa wawili sitayaeleza.
Godfather akamwambia Amerigo Bonasera aitue roho yake yeye atampa haki yake aliyonyimwa na mahakama ya serikali.
Amerigo Bonasera alimuomba Godfather awaue wale vijana wote.
Godfather yeye mpenda haki akamkatalia akamwambia, "Hapana wewe mwanao yu hai."
Naam.
Godfather alihukumu kesi ile kwa uadilifu.
Siku ya pili wale washenzi wote walikuwa vitandani hospitali nyuso zao hazitamaniki taya zao zimeungwa kwa waya na nyuso zimepitishiwa nyuzi kadhaa, vijana waliokuwa na sura jamil wametiwa ulemavu wa maisha kama walivyomsababishia binti Bonasera.
Ujumbe ulikuwa umewafikia wazazi wa watoto wale sawia.
Amerigo Bonasera akawa anakunywa kahawa nyumbani kwake na mkewe roho zimewatua kwani haki yao waliyodhulumiwa mahakamani imepatikana nje ya mahakama.
Mpenzi msomaji mitandaoni kumejaa maneno makali dhidi ya masheikh wanaompinga Sheikh Ponda kwa kuwataka Waislam kumpigia kura Tundu Lisu.
Masheikh hawa kwa kukosa kujua hali ilivyo nje ya duru lao kuwa Sheikh Ponda anaungwa mkono na Waislam wengi wamefanya kosa lile lile lililofanywa na hakimu aliyedhulumu haki ya Amerigo Bonasera.
Waislam kwa miaka mingi walishaipeleka kesi yao kwa Sheikh Ponda kutafuta haki yao nje ya watoa haki rasmi kama alivyofanya Amerigo Bonasera.
Sheikh Ponda kama alivyofanya Godfather Don Veto Corleone ametoa hukumu ya haki.
Sheikh Ponda amewaonyesha Waislam njia ya kupita.
Katika kisa cha Amerigo Bonasera kuna mazingatio makubwa kwa hawa masheikh na pia kwa serikali ya CCM.
Ujumbe wa Sheikh Ponda ni mzito na kama ulivyokuwa ujumbe wa Don Veto Corleone umefika na kueleweka sawia.