Sheikh Mwaipopo: Tundu Lissu alikuwa mwanasheria na mbunge, kwanini hakuwatetea Masheikh waliopo Gerezani?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mhubiri wa neno la Mungu Ostadh Mwaipopo ameongea na wanahabari na kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Masheikh ya kumuonya Sheikh Ponda aliyetumia neno la Mungu kuwaapisha baadhi ya viongozi wa CHADEMA akiwemo Tundu Lissu kuwa ndio Rais wa Tanzania.

Mwaipopo ameomuomba Rais Magufuli kutofuata maneno ya watu bali afanye kazi kufuata sheria ya Nchi ila amemuomba awaonee huruma Masheikh ambao wapo gerezani ingawa yeye hakuwakamata na Rais Magufuli hajawahi kukamata kiongozi yeyote wa Dini.

“Lissu anatudanganya kuwa atawaachia masheikh waliopo gerezani, wakati wanakamatwa alikuwa bungeni na ni mwanasheria hajawahi kuwatetea hata siku moja bungeni, lakini pia tunatakiwa tumuombe Rais Magufuli awaachie kwa huruma yake kumbukeni aliyewakamata sio Magufuli tena walikamatwa na viongozi wakubwa wote walikuwa Waislamu.

Zitto Kabwe wakati anaondoka CHADEMA na kuanzisha ACT Wazalendo alisema kwa kinywa chake kuwa CHADEMA kuna Udini, Udikteta na Ukabila leo anageuka na kuwaunga mkono walewale aliowakimbia kama sio maslahi binafsi ni nini?

Atueleze kilichomkimbiza CHADEMA ni kipi kwanza na Sheikh Ponda alikuwa anampigia kampeni Lipumba, kwanini sasa hivi amehamia kwa Tundu Lissu tatizo nini kama hatafuti maslahi yake binafsi?
 
Waislamu wa Tanzania kihistoria wana bad blood na chadema, na hilo haliwezi badilika leo wala kesho, ni rahisi sana kubomoa imani lkn kuirudisha itachukuwa vizazi ni kama kura za Mikoa ya Dodoma, Singida, Mwanza na Shy kwa chadema ni 0, watu wa Dodoma hawawezi kuisamehe wala kuipigia kura chadema, ...
 
Jibu ni simple tu.

Alikuwa akipigania mambo mengine, angeendelea kuwa bungeni kwa miaka 3 aliyokuwa nje ya bunge kwa hila za Magufuli ambaye amegeuka Mungu mtu angelisemea na hili pia.

Kumbukizi: Magufuli hajawahi kuongea jambo la kuwatetea Watanzania kwa miaka yote aliyokuwa bungeni.

Napekua hansadi hapa niweke clip ya Tundu Lissu alipokuwa akipinga hawa Masheikh wasishitakiwe bara ilhali Zanzibar kuna courts.
 
Nina imani huna kumbukumbu sahihi bora amuone Ndugai akupe hasandi za bunge.
TL alipinga kwa nguvu zote masheikhs kushitakiwa Dar es Salaam kwa makosa yaliyofanyika Zanzibar.
Hawa washachanganyikiwa kama babu yao aliyesema Mbunge wa Kawe hakuwa anasemea mambo ya Kawe that's why hakufanya ABC. Watu tumemwambatanishia video za Mdee bungeni akipigania miundombinu kabaki domo kama msukule
 
Watu wanajua kuuliza maswali!!!!
Sana nchi ina watu wana akili mno, huyo mwaipopo ni Muislamu siasa Kali kama alivyo Sheikh Ponda

Swali murua kabisa Lissu alikuwa mwanasheria kwa nini hakusimama mahakamani na bungeni kuwatetea Leo anatafuta kura ndio anajitia kutafuta kura za waislamu wakati walimfukuza mwislamu Zitto Kabwe CHADEMA na wakamfukuza muislamu Duni Haji
 
Sheikh pilau huyu, kwa hiyo kama hakuwatetea sasa waliowafunga ndiyo bora? hii ni kama mtu kauwa halafu unamlaumu mwingine kwa kusema nitatoa ushahidi niliona akiuwa, halafu ndugu wanamtetea aliouwa na kusema mbona hujamuokoa wakati uliona akiuliwa, mawazo ya kijinga kabisa nafuu angekaa kimya
 
Angalau umekubali kuwa masheikh wetu wanaonewa na utawala dhalimu wa Magufuli na wanahitaji kutetewa.
Hakuwekwa ndani na Magufuli aliwekwa ndani kwanza na Shein kisha Kikwete akapigilia msumari hawakuwekwa ndani na Magufuli wewe yeye kawakuta ndani na miaka yote hiyo Lissu alikuwa Bungeni akiongea kiingereza chake Bungeni na Mahakamani lakini hajawahi wasemea wala kwenda hata kuhudhuria kesi tu
 
Back
Top Bottom