Sheikh Mselem: Tukiambiwa Hapana, tusishindane na mwenye nguvu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,802
Sheikh Mselem: Usalama wa Nchi ni jambo linalopewa kipaumbele na sisi tunapenda usalama, furaha ikizidi inaweza ikazalisha kitu halafu mara nyingi kutokana na uzoefu kuna vitu watu wa kati huchomeka.

Inawezekana tumefanya jambo halali, tumeliombea ruhusa serikalini, tukapewa ruhusa lakini kuna watu wale wasiojulikana, kama wanataka kuharibu kitu au ku-create kitu basi hutengeneza sababu ambayo itatupa sisi dhima kwa hiyo tuwe wavumilivu.

Furaha itoshe tumetoka, tuko huru na tusubiri tutakaporuhusiwa kufanya mijumuiko tutafanya, tukiambiwa hapana basi tusishindane na mwenye nguvu.

 
Daaaah....
I hope and pray Sheikh Farid hakubaliani na hiki kituko cha huyu mtu.

Ana elimu gani huyu shehe? Hayuko media savvy kabisa. Sio kila swali la kila ki You Tube TV kinachokimulika lazima ujibu.

Mmepigania nchi mkarushiwa risasi jukwaani, mkafungwa miaka tisa, hata kama huna nia ya kuendelea na mikutano kwa sasa huna haja ya kutamka mambo ya kishehe ubwabwa namna ile.
 
Daaaah....
I hope and pray Sheikh Farid hakubaliani na hiki kituko cha huyu mtu...
Kati yako wewe na yeye nani anaejua zaidi? Yeye na wenzie ndio waliokuwa mstari wa mbele kupigania wanachokijua huku wameshikana mikono, unaweza vipi kumpinga mwalimu wako wewe shabiki tu.

Yaliyomfika huko alikokuwa kwa miaka tisa yamemfunza asirudie kushindana na mwenye nguvu zaidi yake, kama kuipigania "Zanzibar yao" hiyo Zanzibar yao walipewa na nani? au waliinunua wapi? na kwanini wao kuipigania "Zanzibar yao" kusababishe waumie wengine ambao hawahusiki?

Ile Zanzibar ninayoijua mimi ni ya wote, hakuna mwenye Zanzibar yake pale, ule waliofanya ulikuwa ni ulevi tu wa ubinafsi na mihemko uliowasababishia matatizo, sasa mwenzako anakiri alikosea, wewe bado unataka umrudishe alikotoka wakati akiteseka kule wewe ulikuwa nyumbani na familia yako unakunywa chai na vitumbua.
 
Wewe na yeye nani anaejua zaidi?
Anaejua nini zaidi? Mimi nisingetoa statement ya kizembe namna ile.

Tunapigania kupunguza manguvu dhalimu ya serikali kwenye vi nchi vyetu vichanga vya kidikteta hivi, tumewasapoti miaka 9, tukiamini kuwa wameonewa kwa kosa la kutoa maoni ya kisiasa, whether hatuyakubali au tunakubaliana na kuvunja Muungano. Hawakutakiwa kufungwa miaka tisa.

Anatoka anasema oooh yamekwisha, furaha itoshe tumetoka, tusishindane na mwenye nguvu. Tushukuru tumetoka.

Wanaharakati wetu wa dunia ya tatu maskini ya Mungu, very uchwara. I hope Sheikh Farid does not subscribe to this man’s crap.
 
Nimejiuliza sana hili, kama matukio yote yalikuwa wazi kabisa kwa nini imechukua miaka 9 wao bila upelelezi kukamilika!
Ili Kupewa fundisho kuwa Tanzania ni ya sete wote, nafikiri miaka 9 wamelijua hilo na kama watarudia, watakuwa wanajitakia makubwa! Maana tangu wawekwe ndani nchi haikuwangoja. Na waislamu wengine na madhehebu mengine, Wali endelea na ibada zao.
 
Akili yao imekuwa sawa kwa mafunzo ya miaka 9 ule upuuzi waliokuwa wakiuhubiri kwa sasa hakuna atakayethubutu hapo walipo hata wakiwa wamekaa wakasikia salamu ya Mama nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaweza kusimama kwa ukakamavu maana wanaijua jamhuri sasa ni nini
 
Mimi nisingetoa statement ya kizembe namna ile.

Tunapigania kupunguza manguvu dhalimu ya serikali kwenye vi nchi vyetu vichanga vya kidikteta hivi, tumewasapoti miaka 9, tukiamini kuwa wameonewa kwa kosa la kutoa maoni ya kisiasa, whether hatuyakubali au tunakubaliana na kuvunja Muungano. Hawakutakiwa kufungwa miaka tisa..
Hujui kitu, wewe ni mmoja kati ya lile kundi lililoshibishwa mahubiri ya hao jamaa ambao mlikuwa mnapokea mafundisho toka kwa walimu wajinga, unamuita mwenzio mzembe aliekuwa frontline wakati wewe hata hujulikani ulipokuwa.

Nyie mlikuwa mnapigana vita ambayo hata hamkumjua adui yenu ni nani, badala ya kuelekeza mashambulizi yenu panapostahili, mkayaelekeza kwa wengine ambao kimsingi hawahusiki.

Hivi mnaposema "Zanzibar yenu" mnakuwa mnakumbuka hiyo Zanzibar ina mchanganyiko wa makundi ya watu wenye imani tofauti? au mnataka hao wengine waondoke Zanzibar mbaki peke yenu?

Rudi kawaulize walimu wako hayo maswali wakikujibu ndio urudi hapa na hizi story zako zisizoeleweka, ile Zanzibar sio yenu peke yenu, ni ya wote, huu ubinafsi wenu ndio unawaletea shida halafu mnalia mnaonewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom