Sheikh Mselem: Tukiambiwa Hapana, tusishindane na mwenye nguvu

The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
12,212
2,000
Ebaeban,
Sheikh Mselem au Muislam yeyote yule hawezi kufanya hayo.

Wamekuwa gerezani kwa miaka 9 shutuma za ugaidi zimeshindwa kuthibitishwa.
Mzee inawezekana shekh mselem Hans hulka hio ya kufanya vurugu Ila Kuna waliosikia mawaidha yake huko Zanzibar wakaenda fanya waliyoyataka hayo huweza kuwa yamesababishwa na kichocheo Cha mawaidha ya shekh japo kila mtu kafanya kwa utashi .

Sababu ya hao UAMSHO kuwekwa ndani kipindi kile Ni kutokana na kukithiri kwa matukio ovu ya uchomaji makanisa na kushambulia makasisi wa kanisa huko Zanzibar .

Unaweza jiuliza miaka yote wakiwa ndani mbona Zanzibar ilikuwa tulivu .!?hatukusikia matukio ya kishenzi Kama ya kipindi kile .

Unaweza kuwa unawatetea waislamu kwa jasho na damu lakini usitetea njia ovu kwa kofia ya dini ni haramu zaidi ya kula kitimoto.

Wasalaam

Tus
 

The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
12,212
2,000
Anaejua nini zaidi? Mimi nisingetoa statement ya kizembe namna ile.

Tunapigania kupunguza manguvu dhalimu ya serikali kwenye vi nchi vyetu vichanga vya kidikteta hivi, tumewasapoti miaka 9, tukiamini kuwa wameonewa kwa kosa la kutoa maoni ya kisiasa, whether hatuyakubali au tunakubaliana na kuvunja Muungano. Hawakutakiwa kufungwa miaka tisa.

Anatoka anasema oooh yamekwisha, furaha itoshe tumetoka, tusishindane na mwenye nguvu. Tushukuru tumetoka.

Wanaharakati wetu wa dunia ya tatu maskini ya Mungu, very uchwara. I hope Sheikh Farid does not subscribe to this man’s crap.
Naona umeanza mchochea Moto huyo sheikh Farid

Usikute mwenzio saivi hana hamu ya kurudi alikotoka .
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,725
2,000
Daaaah....
I hope and pray Sheikh Farid hakubaliani na hiki kituko cha huyu mtu.

Ana elimu gani huyu shehe? Hayuko media savvy kabisa. Sio kila swali la kila ki You Tube TV kinachokimulika lazima ujibu.

Mmepigania nchi mkarushiwa risasi jukwaani, mkafungwa miaka tisa, hata kama huna nia ya kuendelea na mikutano kwa sasa huna haja ya kutamka mambo ya kishehe ubwabwa namna ile.
Alikosea wapi kuzungumza mkuu?
 

Kifoi

JF-Expert Member
May 12, 2007
1,204
2,000
Hekima ni kitu adhimu DUNIANI.

Busara ni kitu adhimu DUNIANI.

Kuishi katika taifa bora Kama hili la TANZANIA ni jambo la kumshukuru sana MWENYEZI MUNGU 🙏.

Nchi hii isiyoendeshwa KIDINI.
Nchi hii isiyo na vita vya KIDINI,RANGI NA KIKABILA.
Nchi hii yenye kutoa UHURU WA KUABUDU NA KUTENGAMANA NA WENGINE KIUCHUMI ,KISIASA NA KIJAMII bila ya UKANDA NA UKABILA.....

Tuendelee tu KUULINDA umoja wetu kama watanzania......

#NchiKwanza
#JMTKwanza
#KaziInaendelea
nchi hii ni ya kikatoliki kama unao ushahidi mwengineo ulete
 

Kifoi

JF-Expert Member
May 12, 2007
1,204
2,000
Mzee inawezekana shekh mselem Hans hulka hio ya kufanya vurugu Ila Kuna waliosikia mawaidha yake huko Zanzibar wakaenda fanya waliyoyataka hayo huweza kuwa yamesababishwa na kichocheo Cha mawaidha ya shekh japo kila mtu kafanya kwa utashi .

Sababu ya hao UAMSHO kuwekwa ndani kipindi kile Ni kutokana na kukithiri kwa matukio ovu ya uchomaji makanisa na kushambulia makasisi wa kanisa huko Zanzibar .

Unaweza jiuliza miaka yote wakiwa ndani mbona Zanzibar ilikuwa tulivu .!?hatukusikia matukio ya kishenzi Kama ya kipindi kile .

Unaweza kuwa unawatetea waislamu kwa jasho na damu lakini usitetea njia ovu kwa kofia ya dini ni haramu zaidi ya kula kitimoto.

Wasalaam

Tus
mzee inaonesha ulikuwa ume overdose ya cocaine hivi hukusikiya mwaka jana watu waliouliwa pemba wapatao 20 na wanawake kubakwa na kina jusa kuvunjwa miguu ndio nikakwambia uwache cocaine bora urudie ile bangi
 

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,613
2,000
Ebaeban,
Sheikh Mselem au Muislam yeyote yule hawezi kufanya hayo.

Wamekuwa gerezani kwa miaka 9 shutuma za ugaidi zimeshindwa kuthibitishwa.
Hakuna mahakama iliyosema shutuma zimeshindwa kuthibishwa. Wewe ni mtu mzima na msomi mzuri sana tena mjuvi wa mambo unaelewa kabisa DPP anayo haki na mamlaka kikatiba kuondoa kesi mahakamani pale anapoona hana haja na hiyo kesi tena

Kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi haimaanishi makosa hayapo. Kuna Mambo mengi huchangia ikiwemo mwenendo na ushirikiano wa watuhumiwa wenyewe kwa vyombo vinavyohusika

Ikiwa kweli kwa miaka yote hiyo 9 waliwekwa kizuizini kwa kuonewa, hao ni watu wazima na waelewa wa mambo. Naamini wanaouwezo mkubwa kabisa wa kugoma kutoka mahabusu kushinikiza kesi yao isikilizwe na hatimaye hukumu isomwe

Na wafanya hivyo basi tuone Kama kweli mnahisi walionewa

Msiwapambe na kutaka kuwatakatifuza hao watu. Ukweli wa wao kuwekwa huru wanaujua wao na mamlaka zilizowaachia. Nyie wengine mtaendelea kupiga ramli tu

Wakafungue kesi za madai na majina yao yasafishwe basi tuone
 

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,613
2,000
Viongozi wa Kikristo wanapoungana na mashoga hutengwa na kukemewa na kanisa

Halikadhalika viongozi au mashekhe wanaohubiri na kuchochea vitendo vya kigaidi hawanabudi kutengwa na kukemewa na waumini na viongozi wa kiislamu. Hili kwa upande huu limekuwa ngumu badala yake huungwa mkono
Leo Kanisa limegubikwa na tatizo la ushoga.

Hatuwezi kusema kuwa haya ni mafunzo ya Yesu Kristo.

Halikadhalika tunalo tatizo kubwa la ugaidi hatuwezi kusema hayo ni mafunzo ya masheikh.
 

Ibney

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
303
250
Kati yako wewe na yeye nani anaejua zaidi? Yeye na wenzie ndio waliokuwa mstari wa mbele kupigania wanachokijua huku wameshikana mikono, unaweza vipi kumpinga mwalimu wako wewe shabiki tu.

Yaliyomfika huko alikokuwa kwa miaka tisa yamemfunza asirudie kushindana na mwenye nguvu zaidi yake, kama kuipigania "Zanzibar yao" hiyo Zanzibar yao walipewa na nani? au waliinunua wapi? na kwanini wao kuipigania "Zanzibar yao" kusababishe waumie wengine ambao hawahusiki?

Ile Zanzibar ninayoijua mimi ni ya wote, hakuna mwenye Zanzibar yake pale, ule waliofanya ulikuwa ni ulevi tu wa ubinafsi na mihemko uliowasababishia matatizo, sasa mwenzako anakiri alikosea, wewe bado unataka umrudishe alikotoka wakati akiteseka kule wewe ulikuwa nyumbani na familia yako unakunywa chai na vitumbua.
Jombaaaa umetoa bonge la point. Ila Ni wachache wenye kutafakari.

C ajabu huyo anayefosi kingi hata hajui dini yake inamuelekeza nini wakati kama huo, Ila shekh ameshastuka kuwa waliteleza
 

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
2,484
2,000
Ebu toa ushaidi Kama Kuna Clip waliwai kuhamasisha kuchoma makanisa????isiwe chuki tu za uislamu na waislamu
Mm muislam ila ile mihadhara yao, walichanganya DINI na siasa dhahiri wa shahiri. Binafsi nilitamani waozee ndani maisha yao yote kwa upuuzi ule.
 

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
627
1,000
Huo ushahidi wako kwa nini umekaa nao hadi magaidi wanatoka mkuu? Si ungeupeleka wangekuwa washafungwa?
Kwani makanisa yalipochomwa Zanzibar, watalii kumwagiwa tindikaki wewe hukusikia? Hoja ya msingi matukio yalitendeka au hayakutendeka? Hoja ingekuwa nani alitenda huo uhalifu.
 

Nnangale

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
2,112
2,000
Kwani makanisa yalipochomwa Zanzibar, watalii kumwagiwa tindikaki wewe hukusikia? Hoja ya msingi matukio yalitendeka au hayakutendeka? Hoja ingekuwa nani alitenda huo uhalifu.
Baada ya kushikiliwa yakakoma.
 

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,216
2,000
Alikosea wapi kuzungumza mkuu?
Alikosea aliposema tusishindane na mwenye nguvu.

Basi tusingedai himaya ya Mwingereza iondoke Tanganyika maana walikuwa na nguvu ya kutawala dunia.

Shehe Mselem ametoa kituko kikubwa katika historia ya uanaharakati duniani.

Amefungwa kidhalimu kwa kutoa maoni kuhusu Muungano, anatoka anasema ametosheka na furaha ya kutolewa jela, tusishindane na mwenye nguvu. Huko jela atakuwa amelishwa sumu ya kumpumbaza, zombified.
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,804
2,000
Mkuu labda ulikuwa huangalii TV hawa JAMAA walikuwa wamejiaminisha Sana kiasi.cha kutamba kwenye vyombo vya habari hakuna anayewaweza, nikiri kwamba Shein na serikali yake iliwashindwa, nashukuru kipo walichojifunza
Wengine waanamiaka 22, kipindi cha uamsho walikua Form 3 Wanajifunza what is biology kudiscuss nao unapoteza muda mkuu, hv huyu hakusikia mambo ya uamsho kusema watachinja polisi mara Zanzibar Dola ya Kiislamu isimame
 

edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,804
2,000
Umeandika ukweli ktk post 115, sio Wazanzibari wote wanao chukia Muungano.
Ila ni baadhi ambao hawana maslahi nao. Kama ni hivyo
Tumieni vyombo husika, waambieni Wawakilishi wenu waseme Bungeni, au serikalini.
Sasa hivi mnaye Mwinyi na Samia wote Wazanzibari.
Nendeni mkazungumze nao.
Na sio mbinu mlizotumia za kumwagia tindikali wageni, kuchoma Makanisa, kuchinja Polisi Nk.
Hiyo ni Vita na katika vita ukipigwa inabidi utulie.
Semeni mnadai nchi yenu kwa Vita au Amani ?
Hiyo nchi yao walipewa na nani mpaka waidai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom