Sheikh mohamed issa afunguka kuhusu katiba mpya

wakuziba

Senior Member
Jun 24, 2012
123
43
Jana usiku mwenyekiti wa jukwaa la katiba la waislamu sheikh mohamed issa alieleza baadhi ya vipaumbele ambavyo waislamu watazingatia kama maoni yao kwa kamati ya katiba inayoongozwa na jaji warioba.

"Waislamu lazima wawe na vipaumbele". hayo aliyasema ktk kipindi cha JUKWAA KWA ASIEKUA NA JUKWAA kinachorushwa na idhaa ya kiislamu ya RADIO KHEIR iliyopo dsm.

kwanza lazima katiba itamke kumtambua Mungu. tunaposema nchi yetu ni ya kisekula maana yake ni kwamba hatumtambui Mungu. nakubali kuwa nchi yetu haina dini rasmi lkn kiwekwe kipengele cha kumtambua Mungu ktk katiba mpya. alisisitiza sheikh mohamed Issa. alitoa mfano kwa kusema "Jamhuri yetu inatambua kuwa kuna Mwenyezi Mungu Alieumba mbingu na Ardhi".

Watanzania waruhusiwe, kama ilivyo sasa, kufuata dini waitakayo. alitoa mfano wa wimbo wa taifa ambao unamtaja Mungu (MUNGU IBARIKI......) vilevile alitoa mfano wa viapo vya viongozi (.......... EWE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE) hakuishiya hapo akatoa mfano wa dua ya kuliombea bunge (EWE MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA MBINGU....) "kama Mungu tunamtambua kwa nini tusiweke baraka kwenye katiba yetu kwa angalau kumtaja kuwa nchi hii inamtambua Mungu alieumba mbingu na ardhi. hili jambo halitoathiri dini yoyote kwa sababu dini zote zinakubali Mungu yupo.

Pili katiba mpya lazima itoe UHURU WA KUABUDU. Anasema uhuru ni mdogo kwa waislamu kutekeleza ibadi zao. "leo hii wenzetu wakristo wana fursa nzuri ya kufanya ibada siku za jmoc na jpili. sisi waislamu siku za ijumaa tunapata tabu sana kupata muda wa saa moja tu kufanya ibada. baadhi ya ofisi unaambiwa ukachague kati ya kazi na kwenda msikitini kuswali ijumaa" alisema sheikh.

Vilevile akaendelea kuwa watu wengine hufanya kazi ktk mazingira magumu. ili mtu aende msikitini anahitaji kwenda kuoga kwanza kisha avae nguo safi. hili haliwezekani.

Alishangaa kuona hadi bunge linaendela siku za ijumaa hadi saa saba kamili hali ya kuwa kuna wabunge wengi waislamu. "afadhali bunge likome saa sita kamili siku za ijumaa" alisisitiza. baadhi ya wanawake wa kiislamu wanazuiwa kuvaa hijabu ktk baadhi ya ofisi! kuvaa hijabu kwetu waislamu ni ibada. kumzuia mtu kuvaa hijabu ni kumnyima uhuru wake wa kuabudu.

"Lazima katiba mpya itoe uhuru wa ibada". ama ijumaa ifanywe siku ya mapumziko ili jmoc iwe siku ya kazi, au waislamu wapewe saa tano na nusu hadi saa nane kama muda wao halali wa ibada.

Tatu HUKUMU YA KIFO IENDELEE KUWEPO KTK KATIBA. sheikh mohamed isaa aliendelea kusema kuwa kuna mpango wa kuondoa hukumu ya kifo ukiongozwa na wanaharakati. "tukiondoa hukumu ya kifo, tutapunguza amani tulionayo hapa nchini. watu hawataogopa kuwaua wenzao. mtu akijua kuwa nikiua kwa makusudi na mimi nauawa, hawezi kuua mwenzake." hukumu ya kifo lazima iendelee kuwapo kwenye katiba yetu mpya. alisisitiza sheikh.

aliahidi kutoa vipaumbele vingine jumanne ya wiki ijayo saa tatu usiku.

source: kipindi cha jukwaa, Radio Kheir, DSM
 
Amejitahidi kujenga hoja, hasa hapo kwenye katiba kutomtambua Mungu, lakini kwenye viapo, wimbo wa Taifa, sala ya Bunge MUNGU anatajwa! This is a food for thought. Lakini je kwa Wapagani (wasioamni Mungu) itakuwaje?

Mimi naona ili kuondoa mkanganyiko huu wa mapumziko tutafute siku neutral za mapumziko Mfano Jumatatu na Jumanne, siku nyingine kuanzia Jumatano - Jumapili ziwe siku za kazi. Ndiyo si hii ni nchi ya ki-secular.

Pia sherehe zote za kidini zifutwe ie Pasaka, Christmas, Idd, Maulidi etc. Hakuna mapumziko nchi hii ni ya ki-secular!

Hukumu ya kifo nashindwa kukubali wala kukataa. Tafiti nyingi duniani zinaonyesha sehemu/nchi zilizopiga marufuku hukumu ya kifo, mauaji hayakuongezeka, kama sababu ya Sheikh ni hiyo kwamba wakiondoa hukumu ya kifo mauaji yataongezeka.
 
Kama Unafiki utaondolewa basi kuna mengi ya kuongeza katika Katiba yenu. Zikiwemo haki za msingi za jamii na makundi mbalimbali ya kijamii kwa usawa na haki.

Haki za kuitambua Znz na Tanganyika kama nchi huru zilizoungana kimkataba na kuhakikisha maslahi yao yanazingatiwa kwa usawa na kwa mujibu wa sharia zenu.

Naunga mkono hoja. Insh'Allah tunasuiri darsa zaidi la vipaumbele vyao.

Similar Discussions

Back
Top Bottom