Sheikh Mkuu wa Mbeya, Mohamed Mwansasu: Baadhi ya wasomi ni hawana akili kabisa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,239
24,099
Baadhi ya wasomi ni wajinga kabisa na wapumbavu
Mohamed Ali Mwansasu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Tanzania amesema maneno hayo ''makali'' baada ya kufuatilia juhudi kubwa nzuri za Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amegundua kuwa baadhi ya wasomi Tanzania ni wajinga kabisa na wapumbavu. Maneno hayo yalisemwa katika mkutano maalum uliohudhuriwa na viongozi wa dini mbalimbali katika hafla hiyo ya CCM mkoani Mbeya.

Sheikh Mwansasu amesema kabla ya kutoa kauli hiyo kali, alifuatilia na kusoma maandiko ya Critical Thinkers wenye kufikiria kwa undani kuhusu maana pana ya elimu na kuelimika. Katika ma-critical thinkers alikutana na mwanafalsafa Plato na amegundua elimu si tu kusoma vitabu mbalimbali na kuhitimu shahada ya kwanza, Uzamili au Ph.D bali ..... pia Mwl. Nyerere alipata kusema .....uhuru bila nidhamu ni sawa na uwendawazimu....

Source: MbeyaYetuOnline TV
 
Baadhi ya wasomi ni wajinga kabisa na wapumbavu
Mohamed Ali Mwansasu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Ukisha sema baadhi ya watu fulani, basi hiyo ina-mqualify na kumuingiza kwenye hiyo domain karibu mtu yeyote yule, hata wale ambao Sheikh anawapenda;

Baadhi ya marais ni wajinga kabisa na wapumbavu
Baadhi ya mawaziri ni wajinga kabisa na wapumbavu
Baadhi ya wanasiasa ni wajinga kabisa na wapumbavu
Baadhi ya mameneja ni wajinga kabisa na wapumbavu

Na hata...

Baadhi ya Masheikh ni wajinga kabisa na wapumbavu.

So what? Hakuna jipya. Life goes on.
 
Juni 20, 2017

Sheikh Mohamed Mwansasu : Ataka walaaniwe wanaombeza Magufuli

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mwansansu amesema anayezibeza juhudi za Rais John Magufuli anapaswa kulaaniwa.

Sheikh Mwansasu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu) usiku alipokuwa akisoma dua ya kumuombea Rais Magufuli kwenye kusanyiko la waumini wa Kiislamu wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Dua hiyo ilienda sambamba na futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, kwa waumini wa dini ya Kiislam na kufanyikia katika Ukumbi wa Royal Tughimbe jijini hapa.

“Lazima kwa umoja wetu tuendelee kuungana na Rais wetu katika kupambana na wezi na mafisadi wa rasilimali zetu, na nitamshangaa mtu mwenye akili timamu anapinga juhudi hizi kwa sababu ya itikadi za chama chake au mtu yeyote ni lazima aangamie mara moja,” amesema.

Amesema anachokifanya Rais Magufuli ni kwa ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo familia yake wala chama chake hivyo Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kuungana kwa pamoja katika kumuunga mkono ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu kwani ndiye mlinzi mkuu.

Kuhusu futari hiyo amesema alichokifanya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake ni jambo la thawabu hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati yeye ni Mkristo.

“Huu ni mfano mkubwa, Tulia kuwapa chakula Waislamu hivyo na sisi waislamu tuweze kufanya hivi kwa kuwaita jamii isiyo ya kiislamu na kukaa nayo pamoja zungumza na kufuturu pamoja,”amesema. Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Songwe, Hussein Issah Batuzi, amesema uislamu ni kuitisha jamii tofauti tofauti kukaa pamoja na kuzungumza na kuleta amani na utulivu badala ya kuleta shida, vurugu na patashika kwa jamii nyingine jambo ambalo mwenyezi Mungu anakataa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya (CCM) Wilson Nkhambaku, ametoa rai kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu na Watanzania wote bila kujali tofaui za kiitikadi kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali kwa kazi ngumu wanayofanya ya kupambana na mafisadi wa rasilimali za Taifa.

“Naomba muendelee kuwaombea vingozi wetu ili Mungu aweze kuwapa ujasiri mkubwa na upendo kwa manufaa ya Taifa letu na waendelee kusimamia uchumi wa nchi yetu kwani kufanya hayo kunahitaji ujasiri na ulinzi wa mwenyezi Mungu.”amesema.
Source: Sheikh ataka wanaombeza JPM walaaniwe
 
Alipewa bahasha kabla ya kuongea,hata arusha wale madiwani walikula pesa,wakalala mbele

Bila shaka pembeni alikuwa anasikia harufu ya pilau,hii ndio uchawi wa hawa jamaa,waandalie wali tu akili zao zinabadilika na kukuunga mkono
 
Hawa wanaogopa wasiojulikana..Mfalme Daudi hakuwa na visasi juu ya adui zake bali alimuachia Mungu.,alimuachia Sauli andelee kuishi ingawa alikuwa na uwezo wa kumuua na aliitunza familia ya adui yake Sauli ikaishi vyema.
 
Huyu naengoja nimstahi lakini ajiandae kwenda kuhojiwa kwani niuchochezi kumlazimisha MTU kuamini kile anacho amini yeye ni uchochezi tukirudisha tusi yeye alioshikiwa akili kwanza hayuko huru pili yeye ndio alaniwe usimlani Mtu kwa kukataa kuamini kile ulicho amino wewe ndio maana vitu vinavyo simamiwa na watu kama hawa huwa vinamatatizo kwani hiyo anaiyongoza ndio imani yangu roho huwa inaniuma
 
Juni 20, 2017

Sheikh Mohamed Mwansasu : Ataka walaaniwe wanaombeza Magufuli

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mwansansu amesema anayezibeza juhudi za Rais John Magufuli anapaswa kulaaniwa.

Sheikh Mwansasu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu) usiku alipokuwa akisoma dua ya kumuombea Rais Magufuli kwenye kusanyiko la waumini wa Kiislamu wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Dua hiyo ilienda sambamba na futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, kwa waumini wa dini ya Kiislam na kufanyikia katika Ukumbi wa Royal Tughimbe jijini hapa.

“Lazima kwa umoja wetu tuendelee kuungana na Rais wetu katika kupambana na wezi na mafisadi wa rasilimali zetu, na nitamshangaa mtu mwenye akili timamu anapinga juhudi hizi kwa sababu ya itikadi za chama chake au mtu yeyote ni lazima aangamie mara moja,” amesema.

Amesema anachokifanya Rais Magufuli ni kwa ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo familia yake wala chama chake hivyo Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kuungana kwa pamoja katika kumuunga mkono ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu kwani ndiye mlinzi mkuu.

Kuhusu futari hiyo amesema alichokifanya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake ni jambo la thawabu hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati yeye ni Mkristo.

“Huu ni mfano mkubwa, Tulia kuwapa chakula Waislamu hivyo na sisi waislamu tuweze kufanya hivi kwa kuwaita jamii isiyo ya kiislamu na kukaa nayo pamoja zungumza na kufuturu pamoja,”amesema. Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Songwe, Hussein Issah Batuzi, amesema uislamu ni kuitisha jamii tofauti tofauti kukaa pamoja na kuzungumza na kuleta amani na utulivu badala ya kuleta shida, vurugu na patashika kwa jamii nyingine jambo ambalo mwenyezi Mungu anakataa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya (CCM) Wilson Nkhambaku, ametoa rai kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu na Watanzania wote bila kujali tofaui za kiitikadi kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali kwa kazi ngumu wanayofanya ya kupambana na mafisadi wa rasilimali za Taifa.

“Naomba muendelee kuwaombea vingozi wetu ili Mungu aweze kuwapa ujasiri mkubwa na upendo kwa manufaa ya Taifa letu na waendelee kusimamia uchumi wa nchi yetu kwani kufanya hayo kunahitaji ujasiri na ulinzi wa mwenyezi Mungu.”amesema.
Source: Sheikh ataka wanaombeza JPM walaaniwe
Pilau yakusheresha imedhaminiwa na Tulia Trust ya naibu spika Tulia .okeee sio mbaya kampeni ya 2020 kuanza mapema kwa wanaccm mbaya kwa wapinzani
 
Ulitegemea Aseme Nini Wakati Yupo Kwenye Afla Ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)???

Hapo Unahitaji Akili Ndogo Tu Kujua Falsafa Ya Lugha Aliyoitumia Ukilinganisha Na Mazingira Ya Lugha ilikofanyika.

Ili Ugundue Hilo Pia Huyo Sheikh Aalikwe Kwenye Afla Nyingine Ya Chama Tofauti Na CCM Utaona Nini Atakiongea
 
Back
Top Bottom