Sheikh mkuu mkoa wa Dar aonya maneno ya Lukuvi kutafsiriwa vibaya

Kwani uongo.

Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun, akhiy... huu ni msiba. Kila kitu kiko wazi halafu kweli bila kumuogopa ALLAH anakimbilia kupindisha ukweli kwa maslahi yake ya kidunia...?!!!! Ya ALLAH Tujaalie mwisho mwema waja wako.
 
Yaani huyu Sheikh wa mkoa hapo hamna mtu kabisa,huyo kama kijiti kimevishwa kanzu na kofia ila mtu hukuna.......hii ndio kazi ya bakwata.

Kwa maono yangu jamaa sio shekhe ni mwanasiasa indirect na ni mwanachama wa CCM sikiliza kauli zake, angalia mihaliko yake ya shunguli mbalimbali, matamshi yake, na BAKWATA kama yeye ndio msemaji, anajifanya mnyeyekevu sanaa...

Kiufupi simuelewi kama ni mlezi wa wasilaamu Dar bali ni kada wa chama!
 
  • Ni Alhad Mussa, aonya asichukiwe kwa itikadi
  • Awashangaa wanaomsomea dua bila sababu
  • Awapa somo UKAWA, atoa msimamo wa Z’bar
  • Balozi Seif: Msajili aichunguze UKAWA kwa makini

NA MWANDISHI WETU
SHEIKH wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amewataka waislamu nchini kuacha kumshambulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwa tofauti za kiitikadi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Sheikh Alhad alisema katika siku za karibuni, kumekuwepo na propaganda zinazowataka waislamu kumchukia Lukuvi bila sababu za msingi.
Alisema hatua hiyo imewafanya baadhi ya waumini kuomba dua maalumu dhidi ya Lukuvi bila kutambua msingi wa hoja hiyo.
Kwa mujibu wa Sheikh Alhad, chuki dhidi ya Lukuvi inadaiwa kutokana na kauli yake ya kupinga serikali tatu kwa kuwa pamoja na mambo mengine, haina vyanzo vya mapato jambo ambalo linaweza kuiweka nchi sehemu mbaya na pengine hata kuchukuliwa na jeshi.
“Tunasema hivyo baada ya kugundua kuwa kuna kundi la fulani la waislamu, ambao ni wafuasi wa chama kimoja cha siasa, ambao wamelibeba suala la hotuba ya Lukuvi kwa mlengo wa kisiasa unaowanufaisha.
“Waislamu tukumbuke kuwa dini yetu inatufundisha kuwa kumchukia mtu kusitufanye kutomtendea haki. Hivyo ni vizuri tukamtendea haki hata kama hatokani na chama chako unachokipenda au si muumini wa dini yako.
“Tunawaomba waislamu kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa kwa maslahi binafsi, jambo ambalo linaweza kusababisha chuki miongoni mwetu pasipo na sababu za msingi,” alisema.
Akizungumzia suala la Zanzibar kuwa dola ya kiislamu, alisema Lukuvi aliwasaidia waislamu kujua wasiwasi walionao viongozi wa serikali kuhusu Zanzibar na kwamba huo ndio mlengo wa wanaotaka kujitenga kwa kuachana na Tanzania Bara.
“Mimi sioni dhambi kama Wazanzibar watajitenga na kuwa nje ya muungano na kuanzisha dola ya kiislamu nje ya muungano,” alisema.
Katika hatua nyingine, aliwataka viongozi wa UKAWA kurudi katika meza ya majadiliano pamoja na wenzao wa chama tawala ili kukubaliana na kukamilisha mchakato wa katiba.
Alhad alisema kilichofanywa na UKAWA kutoka kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba na kwenda kwenye mikutano ya hadhara, hakutasaidia kupatikana kwa katiba mpya.
Alisema hatua hiyo itachochea vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi, jambo ambalo si vizuri kuliacha liendelee.

UKAWA mikononi mwa Msajili
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi la Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA), ambalo limeanza kuendesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya kuzingatia taratibu za kisheria.
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi, wakati akisalimia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Kibanda Maiti Mjini Zanzibar.
Balozi Seif, ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alisema kundi hilo lililoundwa na baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya kisiasa vya upinzani, limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na wananchi ya kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la Katiba.
Alisema kitendo cha viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile wanalolihitaji, kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa kushughulikia mahitaji yao ya kimaendeleo na kujikita zaidi katika mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.
Balozi Seif aliwatahadharisha wana- CCM na wananchi wote kujiepusha na kundi hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu waliyowakabidhi.
“Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi, mbona walisubiri kwanza kutia mfukoni mkwanja (posho) halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia vikao vya Bunge Maalumu kwa kujenga hoja,“ alisema Balozi Seif.
Aliwaonya wale viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa, kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa udhaifu wao wa kisiasa.
Alisema iwapo viongozi hao wataendelea na hulka hiyo, waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.
 
Huyu ustadhad naona kashiba mapesa na mali za waqfu sasa anataka uma aru ili awe mrisi wa hicho kiti cha mufti na hawana lolote juu ya waisilam kwanza hizo ofisi zao hakuna utasibii wala juzuu na misahafu na hivi vitu ni muhimu sana lakini utaona mafaili teli ya kudai makodi ya maduka na majumba na huyu jamaa ananishangaza sana badala ya kumsujudia mungu yeye hupenda kusujudia viongozi na hapo akifukuzwa basi huwa nai mpizani
 
  • Ni Alhad Mussa, aonya asichukiwe kwa itikadi
  • Awashangaa wanaomsomea dua bila sababu
  • Awapa somo UKAWA, atoa msimamo wa Z'bar
  • Balozi Seif: Msajili aichunguze UKAWA kwa makini

NA MWANDISHI WETU
SHEIKH wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amewataka waislamu nchini kuacha kumshambulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwa tofauti za kiitikadi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Sheikh Alhad alisema katika siku za karibuni, kumekuwepo na propaganda zinazowataka waislamu kumchukia Lukuvi bila sababu za msingi.
Alisema hatua hiyo imewafanya baadhi ya waumini kuomba dua maalumu dhidi ya Lukuvi bila kutambua msingi wa hoja hiyo.
Kwa mujibu wa Sheikh Alhad, chuki dhidi ya Lukuvi inadaiwa kutokana na kauli yake ya kupinga serikali tatu kwa kuwa pamoja na mambo mengine, haina vyanzo vya mapato jambo ambalo linaweza kuiweka nchi sehemu mbaya na pengine hata kuchukuliwa na jeshi.
"Tunasema hivyo baada ya kugundua kuwa kuna kundi la fulani la waislamu, ambao ni wafuasi wa chama kimoja cha siasa, ambao wamelibeba suala la hotuba ya Lukuvi kwa mlengo wa kisiasa unaowanufaisha.
"Waislamu tukumbuke kuwa dini yetu inatufundisha kuwa kumchukia mtu kusitufanye kutomtendea haki. Hivyo ni vizuri tukamtendea haki hata kama hatokani na chama chako unachokipenda au si muumini wa dini yako.
"Tunawaomba waislamu kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa kwa maslahi binafsi, jambo ambalo linaweza kusababisha chuki miongoni mwetu pasipo na sababu za msingi," alisema.
Akizungumzia suala la Zanzibar kuwa dola ya kiislamu, alisema Lukuvi aliwasaidia waislamu kujua wasiwasi walionao viongozi wa serikali kuhusu Zanzibar na kwamba huo ndio mlengo wa wanaotaka kujitenga kwa kuachana na Tanzania Bara.
"Mimi sioni dhambi kama Wazanzibar watajitenga na kuwa nje ya muungano na kuanzisha dola ya kiislamu nje ya muungano," alisema.
Katika hatua nyingine, aliwataka viongozi wa UKAWA kurudi katika meza ya majadiliano pamoja na wenzao wa chama tawala ili kukubaliana na kukamilisha mchakato wa katiba.
Alhad alisema kilichofanywa na UKAWA kutoka kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba na kwenda kwenye mikutano ya hadhara, hakutasaidia kupatikana kwa katiba mpya.
Alisema hatua hiyo itachochea vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi, jambo ambalo si vizuri kuliacha liendelee.

UKAWA mikononi mwa Msajili
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi la Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA), ambalo limeanza kuendesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya kuzingatia taratibu za kisheria.
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi, wakati akisalimia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Kibanda Maiti Mjini Zanzibar.
Balozi Seif, ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alisema kundi hilo lililoundwa na baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya kisiasa vya upinzani, limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na wananchi ya kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la Katiba.
Alisema kitendo cha viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile wanalolihitaji, kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa kushughulikia mahitaji yao ya kimaendeleo na kujikita zaidi katika mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.
Balozi Seif aliwatahadharisha wana- CCM na wananchi wote kujiepusha na kundi hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu waliyowakabidhi.
"Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi, mbona walisubiri kwanza kutia mfukoni mkwanja (posho) halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia vikao vya Bunge Maalumu kwa kujenga hoja," alisema Balozi Seif.
Aliwaonya wale viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa, kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa udhaifu wao wa kisiasa.
Alisema iwapo viongozi hao wataendelea na hulka hiyo, waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.

Sheikh ametuaibisha wakristu wakati wote tunajua kwamba mjadala wa udini ulianzishwa na Prof. Ibrahim Lipumba aliyehamisha mambo ya kanisani na kuyaleta Bungeni. Tuliufyata kimya wakati Lukuvi anasulubiwa kwa kurudia maneno ya boss wake Rais Kikwete. Kama sio udini au kujipendekeza au yote mawili, kwa nini Prof. Lipumba hakumlaum Rais Kikwete??
 
Wanaendelea kutumika na watatumika sana kisha wataachwa solemba. Hizi dini nazo zimevamiwa na zimekua miradi na mitaji mikubwa ya chama cha mamumiani.
 
Ramadhan Ally said:
Katika hatua nyingine, aliwataka viongozi wa UKAWA kurudi katika meza ya majadiliano pamoja na wenzao wa chama tawala ili kukubaliana na kukamilisha mchakato wa katiba.
Katika sababu mojawapo iliyowatoa UKAWA bungeni ni matusi,dharau na kejeli.

Wiki kadhaa baadaye JK (hata makada wengine wa CCM kama Kigunge) ambaye ni Mwenyekiti wa CCM alikuja hadharani na kuelezea kukerwa kwake na tabia ya matusi bungeni hii inaonyesha kuwa JK na CCM wanalielewa tatizo la matusi,kama Alhadi ni muadilifu kama anavyotaka Waislamu wawe waadilifu kwa adui yao Lukuvi kwa nini asiwaambie CCM wawaondoe bungeni wale wote waliohusika na kashfa ya matusi ili kuiondoa sababu mojawapo ya UKAWA kujitoa?
 
Bakwata ni tawi dogo la c.c.m ambalo linatumika kila uchao bila kuwa na mipaka ya kutumika.
Ukimfatila kwa mbali utagundua huyu shekhe anausaka u mufti kwa gia za kuwabeba mabwana zake,
anaongelea kuwa msajili afute ukawa?
Ninalaani huu upuuzi wa huyu msakatonge na shekhe mchumia tumbo.
 
huyu ni sheikh pekee ambaye namuheshimu nchini kwetu lakini ajiangalie ile heshima na trust tuliyompa anaibetray yeye mwenyewe. hivi vipande therasini vya fedha huwa avimuachi mtu salama ataumbuka.
 
hapa ndipo BAKWATA inajidhihirisha kuwa chombo cha kuongoza Waislamu na jamii ya Watanzania kwa ujumla katika kujenga Taifa lisilokuwa na udini. Ni kosa kwa Muislam (Prof. Ibrahim Lipumba) kumulaumu Mh. Lukuvi (Mkristu) kwa kuongea mambo ambayo Rais Kikwete (muislam) alishaongelea Bungeni tena Prof. Lipumba akiwepo, akakaa kimya, lakini akachukua kisingizio kuwa yameongelewa na Mh. Lukuvi kanisani kuyafanya hoja! Cha kusikitisha zaidi ni jinsi wengi wetu waislam tulivyokurupuka kumlaum Mh. Lukuvi kana kwamba hatujui maovu mengine yanayozungumzwa Misikitini na wakristu wakakaa kimya!
Wakiyaleta Bungeni tutafika??
 
Katika sababu mojawapo iliyowatoa UKAWA bungeni ni matusi,dharau na kejeli.

Wiki kadhaa baadaye JK (hata makada wengine wa CCM kama Kigunge) ambaye ni Mwenyekiti wa CCM alikuja hadharani na kuelezea kukerwa kwake na tabia ya matusi bungeni hii inaonyesha kuwa JK na CCM wanalielewa tatizo la matusi,kama Alhadi ni muadilifu kama anavyotaka Waislamu wawe waadilifu kwa adui yao Lukuvi kwa nini asiwaambie CCM wawaondoe bungeni wale wote waliohusika na kashfa ya matusi ili kuiondoa sababu mojawapo ya UKAWA kujitoa?

na amesema anawajuwa waovu wote na madhambi yao, kwenye Quran kuna sifa 3 za mnafki nadhani huyu inamuhusu.
 
hapa ndipo BAKWATA inajidhihirisha kuwa chombo cha kuongoza Waislamu na jamii ya Watanzania kwa ujumla katika kujenga Taifa lisilokuwa na udini. Ni kosa kwa Muislam (Prof. Ibrahim Lipumba) kumulaumu Mh. Lukuvi (Mkristu) kwa kuongea mambo ambayo Rais Kikwete (muislam) alishaongelea Bungeni tena Prof. Lipumba akiwepo, akakaa kimya, lakini akachukua kisingizio kuwa yameongelewa na Mh. Lukuvi kanisani kuyafanya hoja! Cha kusikitisha zaidi ni jinsi wengi wetu waislam tulivyokurupuka kumlaum Mh. Lukuvi kana kwamba hatujui maovu mengine yanayozungumzwa Misikitini na wakristu wakakaa kimya!
Wakiyaleta Bungeni tutafika??
wewe ni kibaraka wa mfumo kristo huna hata chembe ya uislamu.
 
Hapa tena hakuna swali, ila ni bora angekaa kimya jambo hili lipotee kama mengine. Maana watanzania kila jambo liwe zuri ama baya huwa ni la msimu. Zaidi huyu kiongozi amejidhalilisha sana. Alikuwa ni mmoja wa viongozi wa dini niliokuwa nawaheshimu sana, sasa naona ameamua kutumika kwenye jambo baya na la hatari kama hili.
 
Kwa maono yangu jamaa sio shekhe ni mwanasiasa indirect na ni mwanachama wa CCM sikiliza kauli zake, angalia mihaliko yake ya shunguli mbalimbali, matamshi yake, na BAKWATA kama yeye ndio msemaji, anajifanya mnyeyekevu sanaa...

Kiufupi simuelewi kama ni mlezi wa wasilaamu Dar bali ni kada wa chama!

Kiongozi yeyote wa dini anaye"side" na watawala ni wa kuogopwa kama ukoma. Siku zote viongozi wa dini wanaotambua wajibu wao kwa jamii ni mwiba mchungu kwa watawala kwa sababu watawala mara nyingi ni waongo na wenye kupindisha mambo na viongozi wa dini wanajitahidi kuwa wa kweli na kunyoosha mambo. Sasa Huyu shekhe kumtetea Lukuvi ni ajabu sana. ameamua kuungana na watawala na kuwasaliti umma wa waislam. hata Pengo (kardinali) alipoonesha dalili za kuside na watawala kwenye hili la katiba tulimpasha na sasa ameshika adabu na hamtamsikia tena akitoa kauli zenye ukakasi!
 
hapa ndipo BAKWATA inajidhihirisha kuwa chombo cha kuongoza Waislamu na jamii ya Watanzania kwa ujumla katika kujenga Taifa lisilokuwa na udini. Ni kosa kwa Muislam (Prof. Ibrahim Lipumba) kumulaumu Mh. Lukuvi (Mkristu) kwa kuongea mambo ambayo Rais Kikwete (muislam) alishaongelea Bungeni tena Prof. Lipumba akiwepo, akakaa kimya, lakini akachukua kisingizio kuwa yameongelewa na Mh. Lukuvi kanisani kuyafanya hoja! Cha kusikitisha zaidi ni jinsi wengi wetu waislam tulivyokurupuka kumlaum Mh. Lukuvi kana kwamba hatujui maovu mengine yanayozungumzwa Misikitini na wakristu wakakaa kimya!
Wakiyaleta Bungeni tutafika??

Hata hivyo kaka haikuwa sawa yale mambo kutamkwa kanisani. Haikuwa sawa kwenda kuzungumzia hofu yake dhidi ya watu wa imani nyingine pale. Na bado kuna tofauti ya jambo lilelile, hata kama lina udini linapozungumzwa Bungeni kama alivyofanya Rais na linaposemwa Kanisani au msikitini!

Ni hatari sana kupeleka siasa kwenye maeneo ya kiimani hasa unalolizungumzia linapolenga kuwagawa watu badala ya kuwaunganisha.

Ni vizuri pia ikakumbukwa kuwa ni tabia ya CCM kutumia udini pale inapozidiwa na hoja za upinzani. Tuliona wakati ilipozidiwa ujanja na CUF Zanzibar. Wakaja na CUF ni ya kiislamu, mara kontena la majambia likakamatwa Bandarini likiwa na lebo za CUF. Mbona hakuna akiyekuja na hatua ya kushtakiwa? Japo mmiliki tu wa chombo kilicosafirisha?

Na labda tumeanza kusahau kuwa baada ya kuzidiwa na spidi ya CHADEMA CCM hiyohiyo ikaja na Ukabila na ukanda wa CHADEMA, ilipoona hiyo haikamati vizuri ikaja na U-RC wa CHADEMA, just kwa kuwa kuna Slaa mule! Kwani CCM inakuwa ya kiislamu kwa vile kuna Kikwete? Lakini hilo hamlikumbuki tena!

Ni ukweli kuwa CCM inapenda kuwagawa watu kwa udini na hii ni tabia ya kukemewa. Ukweli uko hivyo. Na wanaosema waachwe waseme.
 
Huyu shekh dhambi inamtafuna ya kusujudia ma bwana zake kuliko Mungu mmoja
 
Ni sheikh anaejipendekeza kila siku ili awe Mufti wa Tanzania wakati tayari anakofia ya usalama
 
Back
Top Bottom