Sheikh Mkoa wa Dar ataka viongozi wa dini kutoa azimio kumuunga mkono Magufuli

Ringo Malisa

Member
Nov 3, 2019
25
13
mashekh.PNG

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amewataka viongozi wa dini kutoa azimio la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Amesema miaka minne tangu Magufuli alipoapishwa kuwa Rais amefanya mambo makubwa ambayo hawakuyategemea. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 18, 2019 katika mkutano uliotishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda uliowakutanisha viongozi wa dini kwa ajili ya kuwaeleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo tangu kiongozi mkuu huyo wa nchi aingie madarakani.

“Jamani niwaulize wenzangu haya mambo hamjayafurahia? Kama mmefurahi kwa nini tusitoke na azimio la kumuunga mkono kwa mambo mema aliyotufanyia hapa nchini.” “Sema tu kuna vitu hatuwezi kusema kwa sababu ya haya mambo ya demokrasia. Watu tunataka maendeleo, nidhamu kama hii iendelee tatizo ni hizi nchi zetu ukisema kitu utaambiwa demokrasia,” amesema Sheikh Salum.

Wazo la Alhad Salum limeungwa mkono na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) jimbo la Dar es Salaam, Alex Malasusa. “Katika kusimamia jambo kutakuwa na mishale hasa unapolisimamia kwa haki. Tutaendelea kukuombea na pale tutakapohitaji kushauriana nawe tutafanya hivyo. Tunashukuru kwa kutupa habari maana tutatoka hapa tukiwa na maarifa mengi,” amesema Malasusa.

Malasusa aligusia hatua zilizochukuliwa kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana jijini Dar es Salaam.

View attachment 1266033

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amewataka viongozi wa dini kutoa azimio la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Amesema miaka minne tangu Magufuli alipoapishwa kuwa Rais amefanya mambo makubwa ambayo hawakuyategemea. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 18, 2019 katika mkutano uliotishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda uliowakutanisha viongozi wa dini kwa ajili ya kuwaeleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo tangu kiongozi mkuu huyo wa nchi aingie madarakani.

“Jamani niwaulize wenzangu haya mambo hamjayafurahia? Kama mmefurahi kwa nini tusitoke na azimio la kumuunga mkono kwa mambo mema aliyotufanyia hapa nchini.” “Sema tu kuna vitu hatuwezi kusema kwa sababu ya haya mambo ya demokrasia. Watu tunataka maendeleo, nidhamu kama hii iendelee tatizo ni hizi nchi zetu ukisema kitu utaambiwa demokrasia,” amesema Sheikh Salum.

Wazo la Alhad Salum limeungwa mkono na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) jimbo la Dar es Salaam, Alex Malasusa. “Katika kusimamia jambo kutakuwa na mishale hasa unapolisimamia kwa haki. Tutaendelea kukuombea na pale tutakapohitaji kushauriana nawe tutafanya hivyo. Tunashukuru kwa kutupa habari maana tutatoka hapa tukiwa na maarifa mengi,” amesema Malasusa. Malasusa aligusia hatua zilizochukuliwa kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana jijini Dar es Salaam.

This mkusanyiko ni mashetani! kama hawawezi kuona matendo ya uovu ya serikali hii, basi ni Mashetani wakubwa! Azory yukowapi? Ben? sandarusi?
 
huyu Ramadhan hii alijipa cheo cha "uenyekiti wa kamati ya mwezi"...huwez kumshangaa na kauli hizi!!
 
Back
Top Bottom