MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Katika jambo ambalo haliko sahihi mahali popote lisemwe bayana ili umma wa waislam wengine nao ujue.
Leo Katika viwanja vya Mwembe yanga ulioko Temeke jijini DSM waaislam wa maeneo mbali mbali mkoani humo walikutana kusali kwa pamoja sala ya Eid Elhadj, Katika sala hiyo walihudhuria viongozi mbali wa serikali akiwemo Waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa, walikuwepo viongozi wa dini ya kiislam akiwemo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za kiislam Sheikh Issa Ponda.
Chakushangaza zaidi ni katika itifaki yao Sheikh Nurdin Kishki ndiye aliyepewa mike kama mtoa khutba au mhutubiaji kwa lugha rahisi, na mwanzo wa khutba yake amewataja viongozi wote kuanzia waziri mkuu Majaliwa,aliyekua Mbunge wa Rufiji Muntaza Mangungu na DC wa Temeke na kuwataja viongozi wengine wa dini hiyo lakini hakumtaja kabisa Sheikh Ponda.
Alipomkaribisha wazi mkuu Kassim majaliwa kuja kutoa salaam za Eid ndipo Katika salamu zake za utangulizi akawashukuru viongozi wote huku akirudia rudia kumtaja Sheikh Ponda kama kiongozi wa dini ya kiislamu.
Kituko kiingine ni wakati wa kupiga picha ya pamoja na waziri mkuu, yeye Sheikh KISHKI akawaita viongozi wote wa dini na serikali kusimama mbele kwa majina lakini akaacha kumtaja Sheikh Ponda.Bado kule mbele kwenye picha waziri mkuu na viongozi akahitaji ulazima wa sheikh Ponda ambapo nahisi baada ya kugundua kitu alianza kuelekea nyumbani ndipo akatafutwa kuja kupiga picha hizo.
Nilikua nafuatilia sana Mawaidha ya huyu Sheikh Kishki lakini nimegundua kua ana matatizo, sio bure ndani ya nafsi yake kuna kitu.
Katika itifaki huwezi kumwacha kiongozi mkubwa tena msomi kama sheikh Ponda, huyu ni kiongozi wa taasisi na jumuiya za kiislam nchini na BAKWATA ikiwemo.Chuki na ubinafsi haviwezi kutupeleka peponi zaidi tutakua wapiga kelele wa mtaani huku tukiendelea kujinasibu kua ni wachamungu kumbe hakuna kitu.
Jamani wenzetu tuepukane na asiyoyapenda M.Mungu kwani islamu sio kanzu ndefu,uislam sio kofia ndefu,uislam sio suruali mfupi,uislam sio hijabu,uislamu sio kufuga ndevu ndefu,uislamu sio sala tano tu bali uislam matendo,salama na amani.
Haiwezekenani mpaka kiongozi wa serikali tena waziri mkuu atambue uwepo wa Sheikh Ponda huku kuna viongozi wa uislamu wa wilaya wasitambue, tena Shekhe KISHKI na wenzake ndio walikua waandaaji na wenyeji wa kumkaribisha waziri mkuu wasitambue uwepo wa Sheikh Ponda kweli? Na hata kama Sheikh Ponda kahudhururia ibada bila kualikwa lakini kama kiongozi kwa wadhifa wake huwezi kumwacha kwenye itifaki.
"Amakweli kuna kitabu kimesema sio wote wamwitao bwana ndio ndio watakaouona ufalme wa Mbingu" na katika Uslam siyo kila atamkae Shahada ndiye atakayekwenda peponi"