Sheikh khalifa: Bunge limeoza, spika sio makini ni dhaifu....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh khalifa: Bunge limeoza, spika sio makini ni dhaifu.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Jul 23, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  WAKATI mjadala wa Bunge la Bajeti unaoendelea mjini Dodoma ukitawaliwa na vijembe, kashfa, kejeli na maneno ya kuudhi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis Khalifa, amesema mhimili huo wa dola umeoza na una udhaifu mkubwa unaotokana na kiti cha Spika kukosa umakini na baadhi ya wabunge kukosa maadili wakati wakijadili hoja zinazolihusu taifa.


  Aidha sheikh huyo amelishambulia Bunge baada ya juzi kushindwa kupitisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kutokana na utoro uliosababisha kushindwa kufikia idadi ya wabunge wanaopaswa kuwamo ukumbini wakati wa kupitisha bajeti kama kanuni inavyoelekeza.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Khalifa alisema mwenendo wa Bunge hivi sasa unahuzunisha kutokana na tabia inayozidi kujengeka miongoni mwao ya kutumia uhuru wao vibaya.
  Bila kutaja majina, sheikh huyo maarufu nchini alisema baadhi ya wabunge na hata viongozi wa mhimili huo wanaenda kinyume na maadili ya Kitanzania kwa kukosa staha na kutoa maneno ya dharau na kebehi hata matusi kwa wabunge wenzao.


  “Wabunge wetu wakati mwingine wanaonyesha kutojali heshima kwani utashuhudia kijana mdogo anashindwa kuonyesha heshima kwa kiongozi wa serikali au mtu mzima anayelingana na mzazi wake na wabunge au viongozi wazee nao wanakosa staha kwa mbunge kijana na hivyo kulifanya Bunge lionekane kama kijiwe cha wahuni,” alisema Khalifa.
  Kwa mujibu wa Khalifa, vurugu ndani ya Bunge zinatokana na wabunge wachache kutafuta umaarufu kwa njia ya mkato kwa kutotii kanuni za Bunge na kwa kutumia lugha chafu.


  “Wabunge wajue wananchi wanawaangalia. Binafsi naona malumbano hayo ni jambo jema sana kwa sababu litawasaidia wananchi kuwa makini kuchagua wabunge, hivyo mwaka 2015 tunategemea wananchi watasahihisha makosa waliyofanya kuchagua baadhi ya wabunge ambao tabia zao zinakera na hawafai kuendelea kubaki Bungeni,” alisema Khalifa.


  Hivi karibuni wakati wa mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Mwenyekiti wa Bunge, Steven Mabumba, alishindwa kuongoza kikao na kusababisha vijembe, kashfa, kejeli na maneno ya kuudhi kati ya wabunge.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Chadema mnathamini waislam? kweli huu mwezi wa ramadhani
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,751
  Trophy Points: 280
  Hata kuliita Bunge inatia kichefu kichefu....Bunge linatakiwa lijali maslahi ya nchi si hili Bunge limejaa mipasho, matusi na kejeli zinazofanywa na magamba ili kuzima moto wa CHADEMA bungeni.
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ila sheikh Khalifa hajafunguka kisawasawa, angeeleza mambo kiuwazi zaidi na sisi mafumbo mafumbo.
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hawezi funguka zaidi ya hapo kwasababu ni kizazi cha wanafiki. Anamlalamikia Spika kutokana na tukio la juzi la kukataa Bunge kujadili kuzama kwa feri huko Zanzibar. Kama siyo tukio hilo ambalo limewakasirisha Wazanzibari na Waislamu wengi usingemsikia analalamika. Alikua wapi wakati akina Makinda wanalidhalilisha Bunge mpaka kiwango cha chini kiasi hiki?!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kama akili zenyewe ndio hizi za kuwasha moto, wasitegemee kubembelezwa na kuwa pampered. Wakileta dharau watajibiwa kwa kiwango kile kile.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  LOL, Kwanini SPEAKER asimfukuze SHEIK KHALIFA Bungeni? .... mind U Sheik Khalifa is not MP remember Mnyika and Thaifu

  (just for slow people who did not understand)
   
 8. GIBA KB

  GIBA KB JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 369
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ningekuwa mpoki job ndugai ningemwita kilaza yan sehemu ya tarehe anaandika jina na sehmu ya jina anaandka tarehe
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  sisi wananchi tumewatuma chadema wawadharau hao wabunge wa ccm, na fito za kuwacharaza (ccm) tushaaziandaa 2015. N.B ukiona mtoto anakushupalia kukukoromea jua katumwa!!!! na aliyemtuma hayuko mbali. ccm si muda mrefi mnakosa mwana na maji ya moto.
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Na mwaka 2015 mtakuja na wimbo ule ule, kura zimechakachuliwa tusubiri mwaka 2020. Nimezoea kusubiri.
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I agree with u hili bunge letu la sasa ningekua mi ni mbunge ningekaa nyumbani kuliko kukaa bungeni na kumuona mwigulu anaongea pumba zake ni bora nikae home hakuna bunge saivi
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mwigulu ndio kiboko ya watoto.
   
 13. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Ndumilakutatu

   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa maneno mengine ni kuwa spika kaoza!!
   
 15. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Khalifa angeenda kwao Burundi akatoa grievances zake. Laiti angeondoka na mrundi mwenzake Mohamed Rukara aliyekuwa jijini hivi majuzi. Huyu hana tofauti na Mtikila. Anapiga kelele akikatiwa kitu ananywea. Hakuna mganga njaa Tanzania kama huyu shosti mrundi anayejifanya mtu wa Kigoma.
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hivi bungeni kuna mbung anayeitwa SHEIK KHALIFA KHAMIS KHALIFA?
   
 17. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  mungu wangu tayari saa tisa nooooooooooooo
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  It was a JOKE... Don't U remember John Mnyika alisema Rais ni Dhaifu akaondolewa Bungeni? ... people just slow? (just in the nutshell)
   
 19. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hayupo wazi, kwa mtazamo wake hapendi neno dhaifu hivyo anatetea viongozi dhaifu kazi ipo
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  Hakuna kazi ya kutunga sheria tena,
  bunge letu limekuwa kama genge na wahuni.
   
Loading...