Sheikh Issah Ponda ni Mwanaharakati halisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Issah Ponda ni Mwanaharakati halisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by aduwilly, Jul 16, 2012.

 1. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama mamia ya watu wataupinga au hakuna yeyote ataeukiri hadharani kuwa ni ukweli. Wakati wanaharakati wengine wakiitwa kuwa wanaharakati kutokana na majina ya taasisi wanazozitumikia kuwa za kiharakati, SHEIKH ISSAH PONDA ni mwanaharakati kutokana na matokeo chanya ya vitendo vyake.

  Ni juzi tu ametoka kudhihilisha hili tena kwa kuwezesha jamii kubwa ya waislam kuridhia kuwa sensa lazima iweke kipengele cha dini kwani itasaidia sana kujua idadi za watu kulingana na makundi yao (umri, jinsia, dini n.k)
  Kama hiyo haitoshi amekuwa shupavu kupambana na tamaduni za magharibi zinazokinzana na matendo safi mbele za Mungu na Binadamu, mfano mzuri ni pale alipotetea kwa ujasiri kitendo cha Rais Mstaafu Alhaji Ally Hasan Mwinyi kupigwa kofi kwa kosa la kutangaza kwenye maulid kuwa Kondom ni njia sahihi ya kupambana na maambukizi ya ukimwi.

  Kwa hayo machache pamoja na mengine mengi Sheikh Issah Ponda amejipambanua kuwa mwanaharakati halisi asiye na hata chembe ya woga katika kutetea kile anachokiamini.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,550
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Atarudi lini kwao Burundi?
   
 3. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ponda ni activist wa ukweli na sio wale wanahelakati kama..!
   
 4. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nenda kawaambie wenzio kwenye vijiwe vyenu vya kahawa sio hapa
   
 5. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Inaumaaa eeh, ndo hivyo, but you av to face the reality
   
 6. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  umeona eeh, siyo ka vile vimama vikipipwa biti tu, kimyaa
   
 7. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  So huamini ka mtanzania anaweza kuwa mwanaharakati shupavu like yeye? Kumbe wewe ndo wale wale wanaoamini kuwa Nyerere alikuwa mrwanda that y ali-manage kila kitu kizuri alichokifanya
   
 8. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  mwanaharakati wa kutetea dini ya kumuua mwenzako ili uende peponi!
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuna vitu vitatu - FREEDOM, JUSTICE na EQUALITY ambavyo waumini wa kweli tumemrishwa kama ibada kubwa ya HUMANITY (UTU) na vikikosekana hivi tuna ruksa ya kuvipigania popote pale. Sasa kama wewe Mkristu na unapigania vitu hivi basi unafanya jambo la Kiislaam haijalishi wewe Sheikh Ponda au Razaro Mkaruka..
   
Loading...