#COVID19 Sheikh Farid Mussa aibuka na Msimamo wa Waislamu Juu ya Chanjo na Imani ya Kiislamu

Magufuli alikuwa alfa na omega.

Aliwacompromise wataalamu karibia wote.

Anachotaka yeye kiwe sahihi au kisiwe sahihi lazima kifanyike.

Kupima mapapai na kusema yana corona ule wote ni upuuzi.

Tatizo nani angeweza kwenda kinyume apoteze mkate wake.

Matokeo yake sasa wanapata tabu sana na wapuuzi kina gwajima.
Inashangaza sana wale waliokuwa mstari wa mbele kuzipinga hizi chanjo (watendaji wa wizara ya afya) leo ndio wanaongoza harakati za kutaka raia wachanjwe, ingekuwa vyema kama wangeteuliwa wataalamu wapya.

Halafu hawajatuambia kuhusu zile njia walizotuambia tuzitumie badala ya chanjo ikiwemo kupiga nyungu (hata Muhimbili waliweka mtambo wa kujifukiza), kula juisi ya tangawizi na limao, kama bado zinatakiwa kutumika.

Hii nchi yetu aliye juu ndio mwenye kauli ndio maana msimamo wa mtu mmoja uligeuzwa msimamo wa taifa zima.
 
Farid mjinga tuh kama wajinga wengine,yeye ndie anajua Sana dini kuliko huko Makkah na medina ambako authority hairuhusu hujaji kwenda huko bila kupata chanjo ya Covid 19??


Mambo ya wataalam awaachie wataalam
 
Inashangaza sana wale waliokuwa mstari wa mbele kuzipinga hizi chanjo (watendaji wa wizara ya afya) leo ndio wanaongoza harakati za kutaka raia wachanjwe, ingekuwa vyema kama wangeteuliwa wataalamu wapya.

Halafu hawajatuambia kuhusu zile njia walizotuambia tuzitumie badala ya chanjo ikiwemo kupiga nyungu (hata Muhimbili waliweka mtambo wa kujifukiza), kula juisi ya tangawizi na limao, kama bado zinatakiwa kutumika.

Hii nchi yetu aliye juu ndio mwenye kauli ndio maana msimamo wa mtu mmoja uligeuzwa msimamo wa taifa zima.
Kweli kabisa kwa sasa watu kuwaamini itachukua mda sana.

Na watanzania linapokuja swala la tiba za kisasa hasa chanjo wako very negative.

Siyo chanjo ya corona tu inayopingwa bali hata dawa za kisasa nyingi zinapingwa.

Nakumbuka miaka hiyo shule ya msingi vidonge vya kuzuia minyoo tulivyokua tukipewa vilipingwa sana.

Serikali ilifanya jambo baya sana kuwaaminisha watu malimao tangawizi pamoja na kujifukiza ni dawa.

Leo imani imewakaa watu awasikii la muadhini wala la mnadi swala.

Matokeo yake watu wasiokua na elimu yoyote ya afya kama shekhe farid na gwajima wanaaminika zaidi kuliko wataalamu wa afya.
 
Wataalamu wana kazi kubwa sana ya kuwaelimisha watu wengi mfano wa huyu shekhe.

Tena kazi kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri.
Mimi siyo mwislam lakini shehe
Shekhe upo sahihi,hachanjwi mtu.
Wachanjane wenyewe! Kama wamekula cha mtu kwa ahadi ya kutuchanja imekula kwao! Drones za Biden zinawahusu! Marekani wametoa hicho kitu kidogo kwa malengo! Malengo yao yasipotimia mtazitapika!
 
Tusiendelee kuwa wazito wa kuelewa vitu vidogo vidogo vya level hii.Siyo Siri tulishajulishwa na watalaamu kwamba chanjo haizuii kuambukizwa covid,inazuia yale madhara ya covid.
Uko nyuma ya wakati. Data zz hivi karibuni zinaonesha kuwa chanjo haizuii madhara ya covid 19 ambayo ni kuugua kiasi cha kulazwa hospitalini na hata kufa. Nakuwekea link hapa usome. Hii ni taarifa ya jana 31-07-2021 toka CDC Marekani!! Sasa chanjo ya nini kama haizuii pia madhara ya corona!! Kama lugha ya malkia ni tatizo tafuta mkalimani.

 
Hii chanjo nahisi ni kuwapa matumaini wazee tuu, maana wanaogopa kufa sana.
 
Nampongeza sana huyu shekhe pamoja na Askofu Gwajima , hawa wamekataa unafiki, wamebaki na msimamo wao wa mwanzo ambao serikali ya mwendazake ilituaminisha kuwa chanjo hizo hazifai, na mbaya zaidi watendaji wakuu wa wizara ya afya pamoja na wakubwa serikalini waliziponda chanjo hizo na kutumia nguvu nyingi kusifu nyungu.

Haikuishia hapo, nyungu ilishika kasi kabisa, hatimaye hospital ya mhimbili kukafungwa mtambo wa kujipiga nyungu kwa yule aliyetaka, huu ulikuwa ujinga wa hali ya juuu sana, kwa kifupi utawala ule haukuamini katika science.

Ukisoma bajeti ya wizara ya afya kwa mwaka wa fedha 2020/2021, kipaumbele mojawapo kilikuwa ni kujenga kituo cha kutolea tiba asili kwa kila kanda, Huu ulikuwa ni uthibitisho mkubwa kabisa kuwa kama nchi tumeamua kuiaga science na kusujudu ujinga.

Sasahivi imekuwaje watu walewale walioamini katika tradional medicine na kuiponda science ghafla wanageuka na kuiamini science na mda huo huo wanaiponda tradional medicine???
 
Hizo nchi ndizo chimbuko la DINI mbili kubwa....

Rejea ya dini hutoka huko ama hutokea Mwanerumango?

Je Kuna awezaye kwenda HIJJA bila ya kuchanjwa chanjo dhidi ya HOMA YA INI na YELLOW FEVER?!!
Hijjah ni ibada ambayo haimfungi mtu katika kuiendea katika mwaka fulani tu.Hivyo hakuna ulazima wa mtu kwenda kuhiji mwaka huu tu.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Hijjah ni ibada ambayo haimfungi mtu katika kuiendea katika mwaka fulani tu.Hivyo hakuna ulazima wa mtu kwenda kuhiji mwaka huu tu.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Fanya tafiti....

Ujue mahujaji hawaingii SAUDI ARABIA bila ya kupimwa magonjwa mengi na KUCHANJWA BAADHI YA CHANJO....

Fanya tafiti mwenyewe.....

#TujitokezeniKuchanjwa
 
Farid mjinga tuh kama wajinga wengine,yeye ndie anajua Sana dini kuliko huko Makkah na medina ambako authority hairuhusu hujaji kwenda huko bila kupata chanjo ya Covid 19??


Mambo ya wataalam awaachie wataalam
Ingekua Iran kidogoooo ningekuelewa,lakini Soudia inayoongozwa na wafalme na haina kiongozi wa dini anaye isimamia serikali, haiwezi kuchuliwa kuwa ndiyo msemaji wa dini.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Maradhi mengi yaliokuwa yanauwa maelfu ya watoto kabla hawajafika miaka mitano
Sasa yana athari kidogo sana kwa ajili ya chanjo

Kila mmoja ana mawazo yake ila asiwaongelee waislam
Ila amkataze mama yake na baba yake wasichanje
 
Ukisikia upuuzi ndio huu COVID aina dawa rasmi.

Attack yoyote ya mwili ambayo aina dawa, defence pekee ya mwili inakuwa immune system yako.

Na kufanya ivyo T Cells lazima zimsome kirusi kwanza kikisha mfahamu kina adapt na kutoa antibodies za kupambana na kirusi; ndio maana baadhi ya watu wakishapata COVID na kupona wanakuwa washatengeneza kinga wenyewe.

Baadhi ya chanjo za COVID sio zote navyojua mimi AstraZeneca na Pfizer; zenyewe zinafanya kitu kile kile ambacho kinga ya mwili inafanya.

Lengo la chanjo ni short cut badala ya mwili kutumia muda kukielewa kirusi chanjo inawezesha T Cells kukielewa kirusi kabla ujapata COVID na kutengeneza antibodies mapema kikiingia tu inakuwa sio kitukigeni kwao na kukizuia mapema kisilete madhara.

Hilo ndio lengo la chanjo pale ambapo mwili unapokuwa attacked na kitu kigeni T cells lazima zimsome kirusi kwanza kijibadilishe kupambana nae na kutoa antibodies sahihi.

Hiyo ndio science hawa masheik uchwara na maaskofu unga unga wanawajaza ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom