Sheikh Fareed wa Uamsho apatikana akiwa yu hai na mwenye afya tele

si vizuri kulazimisha kutawala ( colo-union ) hata watawaliwa wameshajua hayo yanayotokea ndio matunda yake tanganyika isome alama za nyakati //chukua mfano wa IRELAND na IRA na hivi sasa Scotland hiyoooo hawajivunii kuwa chini ya UNITED KINGDOM //Hata mbwa geti likiwa wazi hutoka aktoroka na asirejee pamoja na kwamba unampa makombo ya chipsi na pilau tusileteane ukoloni wa kiafrikaaaaa !!!! uhuru muhimu


Scotland hawaui POLISI watafanya Referendum sio kila mtu wa Scotland hapendi Muungano Huo, kwahiyo hawapigani

Northen Ireland ni Ugomvi kati ya Catholics and Protestants walioko huko hawana lolote na Muungano
Umeona IrA wamewekwa kwenye kundi la Magaidi na wametulia sasa. Na Uamsho lazima wawe kwenye kundi la magaidi sababu wameua MAPOLISI

IRELAND iko Independent na UK; Wales hawataki kutoka kwa MUUNGANO na UK


Lakini kuna Wazanzibari kibao UK;
 
Yupi mmoja wapo?, Baba, Mwana au Roho? badili hapo kwenye "mungu" weka, miungu.

Yesu ni jina lipitalo majina Yote.
Kwa Bwana Yesu kila goti litapigwa

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Kwa sababu za kiusalama inabidi makachero wamuhoji ili kujua alikuwa wapi na atoe ushirikiano, then hao waliomshikilia wabanwe ili tujue ni kina nani!. Hii itasaidia ka deal uchwara walichofanya Uamsho kadhibitiwe.


UKiona hawajamuhoji basi jua ndo kama yale ya Ulimboka, wanajua alikuwa wapi!
 
kwa nini wawakilishi wasililazimishe serekali kuengeza juhudi za kumtafuta amiri faridi ili ichi itulie badala yake wasema uamsho ifutwe
wawakilishi wa ccm walishindwa kujuwa sheria sababu kwanza itibiwe sukari ndio utibu kidonda cha sukari
wao walitibu kidonda cha kisonge na maduka ya pombe badala ya kutibu yuko wapi farid serekali ongeza juhudi za kumtafuta faridi
huwezi kudanganya muda ukifika kubali matokeo badilisha muelekeo wa sera ili ziendane na mahitaji ya wakati ukikataa hivyo soma histoia ya tawala zilizo angukaa
 
kwa nini wawakilishi wasililazimishe serekali kuengeza juhudi za kumtafuta amiri faridi ili ichi itulie badala yake wasema uamsho ifutwe

abdul 28

Kichwa cha habari kwa thread hii ni Sheikh Fareed wa Uamsho apatikana akiwa yu hai na mwenye afya tele.

Au huyu aliyepatikana ni tofauti na amiri faridi unayemzungumzia wewe?

Alieibuka tena anaitwa Sh.Fareed, kiongozi wa UAMSHO, taarifa nyengine zinasema sasa anashikiliwa na polisi baada ya kuchukuliwa maelezo na inatarajiwa atafikishwa mahakamani jumatatu.

Soma post #374. ipo link yenye habari za kushikiliwa na polisi.
 
Huyu jamaa ananifurahisha sana. Alijikamata mwenyewe, akajificha mwenyewe, akamwambia mwenzake atoe altimatum ya 26 hrs baada ya masaa 10 akarudi home kwake. Wakashangilia ushindi. Kifupi ameji-feck mwenyewe.

Alikamatwaje: Alotoka nyumbani na dereva wake, kwenda kununua umeme. Njiani likatokea gari lingine kwa mbele, akambwambia dereva asimamishe gari. Kisha akateremka akahamia kwenye lile gari lingine. Basi! Hivi utekwaji ndo uko vile. Ni vizuri serikali ya Zanzibar iwalipe watoto wa shule posho ili kuwahamisisha waende shule na kuepukana na kushadadia ujinga huu.
 
si vizuri kulazimisha kutawala ( colo-union ) hata watawaliwa wameshajua hayo yanayotokea ndio matunda yake tanganyika isome alama za nyakati //chukua mfano wa IRELAND na IRA na hivi sasa Scotland hiyoooo hawajivunii kuwa chini ya UNITED KINGDOM //Hata mbwa geti likiwa wazi hutoka aktoroka na asirejee pamoja na kwamba unampa makombo ya chipsi na pilau tusileteane ukoloni wa kiafrikaaaaa !!!! uhuru muhimu

Kweli kazi ipo.
Ni uhuru wa nani au nchi gani mkuu? Kutoka kwa nani? Na tangu lini hilo koloni lilianza?

Katika historia ya ulimwengu sijapata kusoma pahala pameandikwa ati mtu kutoka katika nchi inayotawaliwa chini ya ukoloni wa nchi nyingine, mtu kutoka katika nchi inayotawaliwa akapata kuwa amirijeshi mkuu wa majeshi yote ya nchi inayotawala!!!!

Kama unamaanisha Tanganyika na Zanzibar, mbona Mhe. Mwinyi alipata kuwa amirijeshi mkuu, alishindwaje kutumia majeshi yote yaliyoko Tz, kuutangaza uhuru wa Zenji? Au hao wana uamsho walikuwa hawajazaliwa?

Tatizo ni kwamba, hii kasumba mnayolishwa na hao wanaojiteka na kujiachia wenyewe inawafanya wengi wafikiri kwa kutumia bongo za walishaji wa kasumba badala ya kutumia vichwa vyao wenyewe. Very pathetic!
 
Back
Top Bottom