Sheikh auawa kinyama

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108

Barlow(7).jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow,

Sheikh wa Msikiti wa Shamsiya, Haruna Mlala (39), uliopo katika mtaa wa Ibungilo Kirumba wilayani Ilemela jijini hapa, ameuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa 7:00, baada ya kundi la majambazi kuvamia nyumbani kwake na kuvunja mlango kisha wakaingia ndani na kuanza kumshambulia.
“Mara baada ya majambazi kuvunja mlango wa nyumba yake, waliingia ndani na kumkuta mtoto wake anajisomea. Walimuamuru awaonyeshe aliko baba yake na mara baada ya kuwaonyesha alikolala, majambazi wale walimuamuru Sheikh huyo kutoka chumbani na kumtaka atoe brief case (sanduku dogo) iliyokuwa na fedha,” alisema Kamanda Barlow.
Hata hivyo, Sheikh huyo hakuwa na sanduku hilo linaloaminika kuwa lilikuwa fedha, hali iliyowafanya majambazi hayo kushambulia na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Barlow alisema baada ya kutenda unyama huo, majambazi hayo yalitoweka na Sheikh huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu, lakini alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.
Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Sheikh huyo alijaribu kupambana na majambazi hao, lakini walimzidi nguvu kutokana na majeraha ya kichwani na sehemu mbalimbali
za mwili aliyoyapata na kupoteza damu nyingi.
Aliongeza kuwa, Polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio ambaye hakumtaja jina kwa maelezo kuwa uchunguzi unaweza kuvurugika.
Majambazi hao walifanikiwa kuiba simu moja aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh. 85,000.

CHANZO: NIPASHE

Kweli cha mjinga huliwa na mwerevu...

Dhahabu na almasi zote hizo zilizojaa Kanda ya Ziwa...!!! Watu wanabaki kutoana roho kwa simu ya elfu themanini...!!! Lahaula walakwata.
Si wangeni-PM niwatumie hiyo simu kama zawadi ya krismas badala ya kumdhulumu mwenzao nafsi yake? :confused2:
 
mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.isije ikawa ni yale ya kufanyiana revenge kwa waliochomeana makanisa na msikiti.
 
Innallilah wainaillah rajuun

Barlow(7).jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow,

Sheikh wa Msikiti wa Shamsiya, Haruna Mlala (39), uliopo katika mtaa wa Ibungilo Kirumba wilayani Ilemela jijini hapa, ameuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa 7:00, baada ya kundi la majambazi kuvamia nyumbani kwake na kuvunja mlango kisha wakaingia ndani na kuanza kumshambulia.
"Mara baada ya majambazi kuvunja mlango wa nyumba yake, waliingia ndani na kumkuta mtoto wake anajisomea. Walimuamuru awaonyeshe aliko baba yake na mara baada ya kuwaonyesha alikolala, majambazi wale walimuamuru Sheikh huyo kutoka chumbani na kumtaka atoe brief case (sanduku dogo) iliyokuwa na fedha," alisema Kamanda Barlow.
Hata hivyo, Sheikh huyo hakuwa na sanduku hilo linaloaminika kuwa lilikuwa fedha, hali iliyowafanya majambazi hayo kushambulia na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Barlow alisema baada ya kutenda unyama huo, majambazi hayo yalitoweka na Sheikh huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu, lakini alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.
Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Sheikh huyo alijaribu kupambana na majambazi hao, lakini walimzidi nguvu kutokana na majeraha ya kichwani na sehemu mbalimbali
za mwili aliyoyapata na kupoteza damu nyingi.
Aliongeza kuwa, Polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio ambaye hakumtaja jina kwa maelezo kuwa uchunguzi unaweza kuvurugika.
Majambazi hao walifanikiwa kuiba simu moja aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh. 85,000.

CHANZO: NIPASHE

watu bana kuondoa uhai wa mtu na kuiba Samsung ...?
Itakuwa ni njaa walifikiri Marehemu Sheikh ana mapesa kumbe hana kitu masikini wamee Mdhulumu nafsi yake Mwenyeezi Mungu atawalipa kwa hayo waliyoyatenda maovu zidi ya Sheikh wa watu.
 
Ukimwaga damu ya mtu lazma nawewe itakuandama,tayari wauaji 2 waliohusika wameshakamatwa na wamekiri kuhusika,sasa ilioyobaki ni kamanda barlow aongeze juhudi awakamate wote wauaji ili sheria ilichukue mkondowake,mauaji haya inaonekana kuna visasi vulani sio bure.
 
Inawezekana jambazi nao tupo nalo hapa na lenyewe linasema "Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Rajiun," because that's all we do after such insensate mayhem, just Mungu this Mungu that, hakuna cha jambazi anatafutwa, hakuna cha polisi waliitwa au hawakuitwa, hakuna cha any leads, arrests so far? Nothing. Mungu ametoa Mungu ameua, Mtanzania kamaliza hapo, ndivyo tunavyo solve majanga yetu, kwa salamu za rambi rambi nyingi na kumwachia Mungu awa punish, hivi huyo Mungu angekuwa anaweza kum punish mtu angewaacha wamuue mtumishi wake kikatili namna ile for no freaking reason? "Mwanga wa Milele umwangazie ee Bwana," Bwana kashindwa kumlinda na mivisu ya majambazi amuangazie mwanga marehemu saa ngapi?

Crime and punishment is the issue, si dua na mapambio, tuzidishe juhudi kwenye law enforcement efforts, end of story.
 
Bwana alitoa,
Bwana ametwaa,
Mapenzi ya Bwana yatimizwe!!
 
nchi yetu imeingiliwa na mdudu gani kila kukicha matukio ya mauaji kila kona mbeya nako watu wanapigwa nondo kila kukicha,jeshi la polisi limekuwa linaripoti mauaji kama wamekuwa maofisa habari na sio walinda usalama wa wanachi na mali zao wao kazi yao kwenda kuwakamata cdm tu wakifanya mikutano,fanyeni kazi tafteni waalifu watu waishi kwa amani,raia hawana imani na jeshi la polisi maana limejaa rushwa na wizi na ndo hao wanashilikiana na majambazi........cdm chukueni nchi ondoeni hawa askari wazembe tumechoka kutumikia mafisadi......rest in peace wote waliotangulia mbele ya haki
 
Back
Top Bottom