Sheikh Amri Abeid ni nani katika historia ya taifa hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Amri Abeid ni nani katika historia ya taifa hili?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by mpalu, Aug 25, 2011.

 1. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,488
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wadau naomba mwenye taarifa kamili za SHEIKH AMRI ABEID anipatie kwani nimejitahidi kufuatilia kwenye vyanzo tofauti nimeshindwa kabisa kupata taarifa zake,nimeuliza wakazi wengi wa Arusha lakini wengi wao hawana taarifa za kueleweka.Ni nani huyu hasa katika historia ya Taifa letu au kwa mkoa wa Arusha mpaka uwanja wa mpira jijini humo kupewa jina lake.TAFADHALI MWENYE TAARIFA AWASILISHE!
   
 2. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Alikuwa mmoja wa wanaTANU na viongozi wa awali wa Tanganyika huru akitokea Arusha
   
 3. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280
  na ni moja wa washairi muhimu sana katika historia ya lugha ya Kiswahili
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hii nchi bwana ukishaaga dunia historia yako pia wanaiweka kapuni! Yaani hata ule uwanja wa mpira hapo Arusha pamoja nakuupa jina la huyu Sheikh Amri Abeid kiwanja kimechoka mpaka hapa wakazi wa Arusha wameukatia jina wanauita uwanja wa Vitunguu kwakua unavichuguu ile mbaya sijui hizi mechi wanazichezaje??
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Eti nasikiaga huu uwanja ni wa chama tawala nikashangaa sana, je? Kwa kuwa huyu Sheikh Amri Abeid si ali2mia pesa ya umma ktk ujenzi wake? Kwnn iwe ya chama? Na hata nasikia uwanja wa Kirumba pale Mwanza ni ya chama cha majambazi. Mwenye uwelewa a2juze jamani!
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kihalali kabisa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni mali ya manispaa ya Arusha,
  Title ya uwanja iko manispaa inasomeka hivyo na si mali ya CCM, ila tu CCM wameuchukua na kuufanya wao!
  Uwanja huu ulijengwa enzi za ukoloni na ulijulikana kama King George Stadium, hivyo haujajengwa na Sheikh Amri Abeid.
   
 7. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,488
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  duh..awa ccm hatar.... kwa stail hiii utakuta ikulu inaweza ikawa mali ya ccm.....akija rais wa chama kingine aweza daiwa kodi hivihivi kimzaamzaa
   
 8. B

  Bijou JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  huyu ni sheikh amri abeid Kaluta mmoja wa wana tanu, alikuwa ni meya wa kwanza wa jiji la dar baada ya uhuru, mtaa wa kaluta umeitwa kwa ajili ya kumbukumbu yake
   
 9. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sheikh Amri Abeid alikuwa waziri wa kwanza wa sheria katika serikali ya madaraka ya Tanganyika ya mwaka 1960. Alikuwa member of the Legislative Council [kama Bunge la Tanganyika likiitwa wakati huo] toka Kigoma. Alifariki dunia nafikiri mwaka 1961 au 62. Stadium ya Arusha ilijengwa na Lt. Col. Middleton settler mzungu aliyekuwa akilima maeneo Arusha lakini alikuwa akiishi Arusha. Alikuwa mpenda mpira na mara nyingi alikuwa referee katika mechi zilizokuwa zikichezwa hapo. Hii stadium ilikuwa zawadi yake kwa watu wa Arusha. In fact huu ulikuwa uwanja wa kwanza Tanganyika kuwa na taa za usiku nje ya National stadium ya Dar.

  Col. Middleton aliendelea kuishi Arusha mpaka early 1970s - sijui kama alifariki au alirudi kwao Uingereza. Alipofariki Sheikh Abeid - Arusha Town Council [ATC] ikaamua uwanja huo uitwe Sheikh Amri Abeid Stadium. Huyu Shekh Abeid alikuwa na uhusiano wa karibu na madiwani kadhaa wa ATC. Sijui lini CCM iliuchukua uwanja huu lakini sisi wazaliwa na ma al watan wa hapo Arusha tunajua kuwa hii stadium ilitolewa zawadi kwa watu wa Arusha by Col. Middleton. So it should belong tpo Arusha City Council.

  I should add mimi ni CCM damu lakini ni mpenda haki.
   
 10. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hivyo viwanja chama kimeving'ang'ania-lakini vimejengwa kwa hela ya umma,tatzo ndio lipo hapo-ingekuwa vimejenga na hela,za chama ingekuwa si tatizo
   
 11. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  UWANJA huu umechukua jina kutoka kwa Rais wa kwanza wa zanzibar. Sheikh Abeid Amani Karume (1905-1972), Tanzanian political leader, became the Zanzibar first president and vice president of the republic of Tanzania. He was one of Africa's least-known leaders.
   
 12. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  [h=1][/h][h=1]Sheikh Amri Abeid Amani Karume[/h]
  Sheikh Amri Abeid Amani Karume (1905-1972), Tanzanian political leader, became the first president of Zanzibar and vice president of the republic of Tanzania. He was one of Africa's least-known leaders.
  Sheikh Abeid Karume was apparently the son of a slave woman from Ruanda-Urundi who moved to Zanzibar when the boy was young. He had little formal education, in 1920 becoming a seaman working cargo boats out of the island. He ultimately rose to quartermaster. A member of the British Seamen's Union, after 1938 he operated a syndicate of motorboats carrying passengers to and from harbor ships.
  Karume first entered politics in 1954 when he was appointed town councilor. Later he became president of a social organization for black migrant workers called the Zanzibar African Association. In 1957 this group united with the Shirazi Association to form the pro-British AfroShirazi Party (ASP) with Karume as president. In July 1957, by appealing directly to the African community making up four-fifths of the population, the ASP won four of five seats in the colonial Legislative Council.
  In the years before the 1964 revolution, Karume led the ASP in opposition to the ruling Arab coalition which was seemingly intent on maintaining the political economic dominance of the Arab community. Zanzibar Pemba, an area the size of Rhode Island, became independent on Dec. 10, 1963. On Jan. 12, 1964, young ASP militants overthrew the Sultan and established African rule.
  Karume was leader of the Revolutionary Council and subsequently became president of the new Zanzibar People's Republic. He was described as a big, slow, even phlegmatic, man who was honest, dependable, and strong-minded to the point of stubbornness. An eloquent Swahili orator, Karume spoke only halting English. He was a devout Moslem and the father of two sons. His role in the revolution was disputed; claims were made that he was a figurehead, even a prisoner of the real leadership which was said to center on Abdulrahma Babu, Kassim Hanga, and Hassan Moyo.
  The revolutionary goal was to establish a wholly egalitarian society and, to this end, President Karume proclaimed the Zanzibar Manifesto on March 8. This nationalized and redistributed the land, 80 percent of which was held by the Arab 13 percent of the population.
  In April 1964 Karume negotiated a union with mainland Tanganyika under which Zanzibar retained considerable authority in domestic affairs. He became first vice president of the United Republic, renamed Tanzania in October. Speculation was rampant whether Zanzibar was saved from becoming a Communist state or whether Tanganyika would go Communist along with the island.
  After the union, despite extensive aid largely from East-bloc countries, Zanzibar's economy stagnated as each partner went its own way domestically. Karume both hailed the union as an example for other African states and raised objection to any further integration.
  On April 7, 1972, Karume was assassinated by four gunmen in Dar es Salaam. Two members of the Revolutionary Council were wounded in the attack.
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Uwanja uliochukuwa jina la Sheikh Abeid Amani Karume ni ule wa pale Ilala, makutano ya barabara inayokwenda kigogo (Rashid Kawawa road na Uhuru street)
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Don't worry! Haki itapatikana ktk miaka siyo nyingi na hakika hakuna litakalopita.
   
 15. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nachanganyikiwa. Ni karume au kaluta?
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni Sheikh Amri Abedi Kaluta.
   
 17. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kijana hapa ndiyo umechanganya madawa kabisa..... ya hospitali na ya wadudu labda!

  Sh. Abedi Amani Karume ni mwengine na Amri Abedi Kaluta ni mwengine. Ama kweli Tanzania hatuna hata historia ya watu kama hawa, tunamsoma Nyerere tu.

  Sisi vijana wa zamani tulikuwa tunatumia kitabu cha Amri Abedi cha mashairi katika o level exams in Kiswahili. Pamoja naye vilikuwepo vitabu vya Shaaban Robert (naye utasema humjui)

  Vijana hebu chakarikeni angalau musome historia ya nchi yenu siyo kuishia na Nyerere na Kawawa tu.
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Angalizo: Sheikh Amani Abeid Karume , huyu ni first president wa Znz Huru.

  Na Sheikh Amri Abeid Kalute ni waziri wa kwanza wa sheria wa Tanganyika huru na pia alikuwa mshahiri mahiri sana. Na jina lake la kishairi aliitw STAHARAKI akiwa na maana kuwa hababiki.

  Hiki ni kipande cha shairi lake akilitambulisha jina lake

  Staharaki kwa tendo,tendo nikilibaini silifanyii vishindo,
  Vishindo ulimbukeni, limbuko si wangu mwendo,
  Staharaki kwa tendo, mso nijua jueni,
   
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  UKOSAPO NENO JEMA, KHERI UJINYAMAZIE.

  Nakuasa usikie, usemaji ni karama,
  Maneno usirukie, sema mambo kwa kupima,
  Utamkapo ujue, neno halirudi nyuma,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Kheri ujinyamazie, ovu huleta khasama,
  Majuto yasikujia, “Laiti nisingesema”,
  Mtu baa azuae, Motowe utamchoma,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Ni wengi wajiponzao, kwa zao mbovu kalima,
  Heshima waitakao, waseme usemi mwema,
  Wale waumbukanao, ni kwa ndimi kuparama,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Watazame wakuao, dunia kuwatazama,
  Ni wale wapimiao, kabla ya kuyasema,
  Na kimya wanyamazao, wakosapo neno jema,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Neno huenda likuwe,lizidi hata vilima,
  Mambo mawi liyazue, akili zende mrama,
  Au mema yatukie, liwapo neno la wema,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Funzo walitufunzao, wazungupule wa zama
  Zama za kale na leo, walokimcha Karima,
  Yawe mema tusemao, tusije zusha zahama,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Mola akubarikie, na ambaye akusoma,
  Na furaha ututie, uwe ni diwani njema,
  Mema utuhadithie, wana kwa watu wazima,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Mtunzi: Bwana Amri Abedi Kaluta.
   
 20. B

  Bijou JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145


  msamehe bure HUYU AMECHELEWA KUJUA!!!!!!!!!!!!!!!!!! na inaonesha jinsi watanzania tusivyokuwa watu wakupenda kujisomea na kudadisi. HUO UWANJA NI KUMBUKIZI YA SHEIKH AMRI ABEID KALUTA
   
Loading...