Sheikh Abuu: Tujihadhari, amani inaweza kuvunjika kupitia mijadala ya kimadhehebu inayoendelea

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,274
24,140
19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA MADHEHEBU HAYA MAWILI

Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha ktk utumishi kwa dini na jamii kwani yeye ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni na Shia yanayo shambuliana kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao.

Amewataja Sheikh Mziwanda na Samir wa upande wa Sunni huku upande wa madhehebu ya Shia kupitia Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Abdul na wenzie watatu wakijitetea.

Na pande hizi mbili za madhehebu haya yakinukuu kile wanachoamini kwamba ni sawa kwa upande wa madhehebu yao.

Pande hizo zimewekuwa zikirushiana maneno yanayotishia amani za kila aina mfano amani ya viungo, amani ya roho, kuvunjiana heshima n.k huku wote wa pande hizi mbili wakiwa na wafuasi wao hivyo kutishia amani kwa ujumla ya Tanzania maana wafuasi wa pande hizi mbili zinaweza kukabiliana kutetea pande zao na viongozi wao .

Mfumo wa uendeshaji wa mijadala hii imeleta ukakasi mkubwa huku maneno ya kutishiana uhai baina ya pande hizo yakitamkwa asema Sheikh Abuu Iddi kwa masikitiko makubwa.

Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......
 
Aache mashia watandikwe mpka wafaham wapokea misaada kutoka kwao kuwa watoaji wanawakusudia kuwa wafuasi wao na si kwa ajili ya kutaka thawabu,,,
 
Lifahamu dhehebu ya Shia Tanzania

Toka maktaba:

Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1

KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania

HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2

Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif

Source : Asadiqmedia
MK254
 
19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI YA MADHEHEBU KULINGANIA

Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha ktk utumishi kwa dini na jamii kwani yeye ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni na Shia yanayo shambuliana kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao.

Amewataja Sheikh Mziwanda na Samir wa upande wa Sunni huku upande wa madhehebu ya Shia kupitia Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Abdul na wenzie watatu wakijitetea.

Na pande hizi mbili za madhehebu haya yakinukuu kile wanachoamini kwamba ni sawa kwa upande wa madhehebu yao.

Pande hizo zimewekuwa zikirushiana maneno yanayotishia amani za kila aina mfano amani ya viungo, amani ya roho, kuvunjiana heshima n.k huku wote wa pande hizi mbili wakiwa na wafuasi wao hivyo kutishia amani kwa ujumla ya Tanzania maana wafuasi wa pande hizi mbili zinaweza kukabiliana kutetea pande zao na viongozi wao .

Mfumo wa uendeshaji wa mijadala hii imeleta ukakasi mkubwa huku maneno ya kutishiana uhai baina ya pande hizo yakitamkwa asema Sheikh Abuu Iddi kwa masikitiko makubwa.

Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......
Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......
 
Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......
Hebu Muulize huyo Shk Abuu Idd kwanini yeye mwenyewe hataki dhehebu la Wsisilamu wa Ahmadiyya kuwemo ndani ya Bakwata?

Yeye kama kiongozi hataki Ahmadiyya iwemo ndani ya Bakwata na ndio maana na wangine nao hawataki Shia wawemo ndani ya Bakwata. Sumu ya ubaguzi inaendelea kuwatafuna hatimaye Bakwata yote itasambaratika vipande vipande.
 
Hebu Muulize huyo Shk Abuu Idd kwanini yeye mwenyewe hataki dhehebu la Wsisilamu wa Ahmadiyya kuwemo ndani ya Bakwata??. yeye kama kiongozi hataki Ahmadiyya iwemo ndani ya Bakwata na ndio maana na wangine nao hawataki Shia wawemo ndani ya Bakwata. Sumu ya ubaguzi inaendelea kuwatafuna hatimaye Bakwata yote itasambaratika vipande vipande.
Kwanini Balukta ilifutwa? Mzee Mohamed Said naomba jawabu kutoka kwako NGULI wa historia ya nchi yetu, historia ambayo kwa miaka mingi haikuandikwa popote, lakini kwa mkono wako imeweza kuandikwa japo kwa uchache. Amani iwe kwako
 
Bakwata Top cream yote imejaa Masunni. Masheikh wa Bakwata wananawapiga vita Answaar Sunna hasa kwenye masuala ya kuandama mwezi na Maulidi(Madufu)

Tatizo limeanzia hapa, BAKWATA walipaswa kuwa kama walezi wa madhebu yote(administratively) na siyo Kujiingiza kwenye mambo ya kiimani kwa kuBASE sana upade wa Sunni.

Sheria iliyounda Bakwata ifutwe , iletwe mpya itakayoyapa hadhi madhehebu yote kwa USAWA.
 
Kwani BAKWATA maana yake ni ni ni?
Mi nilidhani ni Baraza la Jumuiya za Kiislamu Tanzania.

Ilitakiwa liwe na vitengo vya madhebu yote makubwa ya kiislamu yaliyoko katika nchi za Kiislamu hasa za Kiarabu ambako ni chimbuko la Uislamu.

Mfano madhehebu makubwa kama Sunni, Shia, Ahamadiya, Aswalisuna, Ismailiya, Sufi, Wahabi, Shafi, Hanafi, Abadi. Maliki. Yaliyakiwa kuwepo na wawakilishi BAKWATA.
 
Bakwata Top cream yote imejaa Masunni. Madhekh wa Bakwata wananawapiga vita Answaar Sunna hasa kwenye masuala ya kuandama mwezi na Maulidi(Madufu)

Tatizo limeanzia hapa, BAKWATA walipaswa kuwa kama walezi wa madhebu yote(administratively) na siyo Kujiingiza kwenye mambo ya kiimani kwa kuBASE sana upade wa Sunni.

Sheria iliyounda Bakwata ifutwe , iletwe mpya itakayoyapa hadhi madhehebu yote kwa USAWA.
Bakwata ni chombo kwa ajili ya kuwadhibiti waislamu waswahili.

Hawa ndiwo wengi Tanzania. Bakwata haijishughulishi sana na madhehebu ya Shia, Ahmadiya, Bohora, Ismailiya nk.

Wafuasi wao ni zaidi wahindi.
Taasisi za waislamu zimeagizwa na RITA kurekebisha katiba zao zitamke kwamba wako chini ya Bakwata.

Serikali isiyo na dini kwa nini inajiingiza kwenye mambo ya dini.
 
Back
Top Bottom