Sheikh Aboubakar Zubeir amewahimiza mahujaji watakaoenda kuhiji Makka na Madina nchini Saudia Arabia kuwa na moyo wa uvumilivu na kusamehe

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Dar es Salaam. Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir amewahimiza maujaji watakaoenda kuhiji Makka na Madina nchini Saudia Arabia kuwa na moyo wa uvumilivu na kusamehe wakati wa kipindi chote cha ibada watakachokuwa nchini humo.

Sheikh Zubeir ametoa rai hiyo leo Jumatatu Julai 22, 2019 wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo maujaji 100 watakaoenda kuhiji chini ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Amesema ibada ya hijja ina mkusanyiko wa watu wengi wanaotaoka kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni na ikitokea umeganyagwa bahati mbaya kuwa na moyo wa kusamehe.

" Kwenye hijja kuna mambo mengi ikitokea umegawanywa na mwenzako, usikasirike bali kuwa wa kwanza kumshika bega na kumuomba radhi. Pia mkifika msiongee maneno machafu na ya kuhudhi kuweni wavumilivu," amesema Sheikh Zubeir.

Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Himid Jongo amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo kuhusu taratibu wanazotakiwa kuzifuata wakiwa nchini Saudi Arabia.
 
Back
Top Bottom