Shehe: Walichokifanya polisi ni sahihi

Huyo Mkenya kilimpeleka nini kwenye fujo?

Nani kasema mkenya alikuwa kwenye maandamano. Huyu alipigwa risasi pale stend ya magari ya kwenda Namanga.Kwa hiyo alikuwa anasubiri gari pale na kwa baahati mbaya polisi walirusha risasi zikapitiliza zikampiga. Hata yule bwana mdogo aliyepigwa risasi hakuwa kwenye maandamano bali maeneo ya karibu na stendi pale jogoo house. Sisi wa Ar tunajua hilo acha kushabikia mauaji Zomba.
 
JK: "Mauaji ya Arusha ni bahati mbaya"
Shehe: "Mauaji ya Arusha ni sawa"
Membe: "Mauaji ya Arusha ni ukiukwaji wa maadili"
Nahodha: "Mauaji ya Arusha ni ya kisiasa"

Ukiona mauaji yanaitwa BAHATI MBAYA au SAWA ujue ni kawaida kwao

Ahsante mwanajamvi.
Karibu kwetu Gah-wa.
 
Kama aliesema ni shehe basi hayana uzito yachukulieni poa tu, subirini tamko na Masheikh wa Dsalaam muone tofauti ya "Shehe" na "Sheikh"
Masheikh hawatatetea watu wa zanzibar pekee kama wengine wanaoumia wa Tanzania bara kuuwawa na kuchukulia "powa" wa Visiwani kumiminiwa risasi.


Hapa sijakuelewa mwanajamvi!
Masheikh kamwe hawawezi kukubali mauaji hivyo!
Huyo wa A town ni shehe.
 
Thanks woote walioshiriki kuandaa mjadala wa katiba mpya, to me it is a good step toward real changes, harakati kama hizi hazitakiwi kukoma, sijui baada ya Kongamano la leo, nini kinafuata?
 
Huyu sijui Sehe au Shehe,whatever they call!Ndio msemaji wao hapo Arusha?Au ndio nitoke vipi?Maneno hayo atakuja kuyajutia siku moja!
 
Ukiambiwa huna elimu hujui hata kitu kinaitwa haki utasema tumekuonea? Au tuna udini? Hivyo vihela vidogo unavyosaidiwa ndo ufikie kiwango cha kusema intelijensia walikuwa na haki ya kuua? Kwani tuko iraq? Acha ujinga hata wazee wa intelijensia fake hawajatoa kauli ya kusema walikuwa na haki ya kuua! Ww na elimu yako ndogo na vijihela unavyopewa unasema ni haki kuua! Hivi uko ulimwengu gani? Dark ages? Unanipandisha hasira sana, tatizo lako ni elimu finyu
 
jeshi la polisi nchini halistahili kulaumiwa kwa mauaji ya arusha, kwani halikuwa na njia ya mkato ya kujihami zaidi ya kufanya lilivyofanya.

Hiyo ni kauli ya imam wa msikiti mkuu wa ijumaa jijini hapa, shehe mohamed hambal, aliyekuwa akihutubia msikitini hapo katika swala ya ijumaa jana.

Alisema hivyo wakati akitoa msimamo wa waislamu wa arusha juu ya tukio hilo lililosababisha vifo vya watu watatu, watanzania wawili na raia mmoja wa kenya.

Shehe alisema katika mkutano wa hadhara wa chadema ulioongozwa na katibu mkuu, dk. Willibrod slaa na mbunge wa moshi mjini, philemon ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani.

Alisema kwa kauli yake, dk. Slaa aliwataka wafuasi wake kuandamana hadi kituo kikuu cha polisi walikokuwa wameshikiliwa viongozi wao wa kitaifa, baada ya kufanya maandamano yasiyo na kibali, huku akitoa saa moja waachiwe, hali ambayo shehe alisema ilikuwa na lengo la kuvunja amani.

“mbali na kauli hiyo, pia dk. Slaa alitoa kauli mbaya zaidi ya kuwa kila kijana aliyeko katika mkutano ule, apite njia yake wakutane polisi huku akiwahadharisha wanawake wenye watoto,
kutokwenda huko kwa kuwa kungetokea mapigano,” alisema.

Shehe hambal alisema kutokana na kauli hizo ni wazi kuwa viongozi hao walikuwa wamedhamiria na walifahamu nini kitatokea, baada ya wao kuamuru vijana na wafuasi hao kuvamia kituo cha polisi wakiwa na mawe na silaha zingine.

“hali hiyo ilisababisha polisi nao wajihami kwa mabomu, risasi za mpira na walipoona wanataka kuzidiwa nguvu, walilazimika kutumia risasi za moto ili kuwatawanya wafuasi hao,” alisema shekhe.

Kuhusu kauli ya ndesamburo kwa rais jakaya kikwete kuwa kamwe nchi haitatawalika, hambal alisema ni ya kichochezi na kumdhalilisha, kwani ni rais aliyepo kikatiba na ana mamlaka kubwa.

“jamani polisi ni dola na ni serikali ile, na pale kuna silaha mbalimbali za hatari sasa ingekuwaje kama wafuasi wale wangefanikiwa kukiteka kituo, si wangeua hadi watu wasio na hatia?” alihoji shehe hambal.

habarileo | shehe: Walichokifanya polisi sahihi

pumba tupu!

 
Naona Ivanovic kascore...so its Chelsea 1 and B'Burn 0.............Big UP wajomba....naona msondo (Uzoefu) sasa unawatoa....More to PLAY
 
Huyo Mkenya kilimpeleka nini kwenye fujo?

Kama kawaida ushabiki unapelekwa kidini. Anayeitwa shehe kanukuu taarifa ya polisi ikionyesha wazi kabisa hana utashi wake binafsi. Pili kama wanachokifanya polisi ni sahihi waambieni wawaonyeshe ni wapi walau tu hao waliopigwa risasi za moto na kufa walipigwa wakiwa wapi?
 
Hapa kinacho msumbua ni njaa................Mwacheni ajipendekeze maana kutunza wake wanne na watoto wao sio kzi rahi ati......
 
My take: Busara hapa Slaa angewatutliza wafuasi wake na kuwaeleza warudi majumbani kwa amani na wao viongozi waende polisi kufuatilia hatima ya viongozi wenzao badala ya kuhamasisha umati wote kuelakea kituoni, nachelea kuhoji busara na uadlifu wa Slaa.

CDM wanajua wanachofanya, ulitegemea polisi wangefanya nini??? tuache kuwalaumu polisi bila sababu za msingi!
 
Not sure where are we heading to, but seems Mohamedans are coming in from the COLD!
 
Yaani jamaa wameua na hii mi njemba inahalalisha? Kweli imezoea damu na bila damu imani yao ni butu!
 
Busara mbele! Nachelea kusema kuwa wafuas wa chadema walkuwa sahih kuvamia police station kwani police wasingekubal na hvyo mapgano yangetokea tu,lakin pia nahoji utashi wa jesh letu kwan naamin hakukuwa na sabab ya msingi ya kuzuia maandamano ya wananch.hvyo kama wote wanamakosa mie ningeanza kumwadhib aloanza makosa yaan jesh la police.
 
Na kuna Mapdri na Mapadiri, Padir!, kwa nini usimshngae padiri aliyeamrisha fujo?

simba asipocheza na yanga basi ubingwa bado hivyo hivyo umashuhuri wa mashehe au mapadri ni kupingana na msimamo wa dini ya mwingine. hiyo ndio falsafa ya dini inavyoenda.. utakuta mtu anatoa mfano kwanini mapadri awakulaani mauaji ya pemba wakati mashehe walilaani kwani ni lazima wao kusema kwa kila mauaji.......au utakuta mapadri wanalaamu mashehe kupinga kitu fulani nao huu ni ushindani usio na maana
cha msingi tujiulize mapadri wakisema wanaelekeza tuhuma za mauaji kwa nani mashehe au serikali? na kama kwa serikali basi mashehe wakijibu wanakuwa wameamua kupoteza muda wao.

vivyo hivyo kama mashehe wakitaka mahakama ya kadhi basi mapadri watulie serikali iwajibu na si wao wawajibu mashehe
 
Back
Top Bottom