Shehe wa msikiti wa Kimara aitaka Serikali impigie simu Allah ili awalipe gharama za kubomoa msikiti

nyakandula

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
1,198
1,595
Baada ya Serikali kuzitaka nyumba za ibada Kimara zilizo katika hifadhi ya barabara kubomoa wenyewe kabla hawajabomolewa na serikali.

Serikali imesema endapo wasipobomoa wenyewe Serikali itawabomolea kwa lazima na gharama hizo watalipa wao wenye msikiti.

Viongozi wa msikiti wameapa hawatabomoa msikiti na hawatalipa hizo gharama kwasababu msikiti sio mali yao ni wa ALLAH na watawapa namba za mwenye msikiti ALLAH ili wampigie awalipe hizo gharama.

Chanzo: Channel ten
 
Kwani sadaka zilikuwa zinaenda wapi..?? Kwa Allah..?! kamata hao wataonyesha walipozificha hizo sadaka ili walipe gharama za kubomolewa...

Sadaka zinafata maagizo yaliachwa na Allah. Hivyo shaka ondoa uliza kingine
 
Hawa jamaa kila kitu wanatafuta kick mi ningekua dereva wa lile tinga tinga wao wakiwa wanaongea na waandishi wa habari mi nafanya yangu tuone kama hawataingia kwenda kutoa makapeti yao mule ndani.Tena navunja huku nakula kitimoto

Hiyo ni strategy (aka Mkakati) ya hali ya juu ya kupata mfadhili atakayejenga mbadala tena wenye hadhi kubwa kuliko huo uliopo. Siku kijiko kikitia timu zinapigwa picha za video na kutumwa duniani huku maelezo yakiwa tofauti kabisa. Watu watajitokeza kujenga kwa haraka sana. We acha tu
 
Gharama sio kubwa sana. Wakiweka baruti moja tu ya Tsh mia tano kila kitu kinageuka kuwa vumbi. Serikali ilichofanya ni kuwapa heshima waumini kufanya kazi hiyo kwa ustaarabu na kwa kufuata taratibu zao wenyewe kama waaamini. Wasipopenda kuitumia heshima hiyo basi wasije kumlaumu mtu baadaye... Mungu wetu pia ni Mungu wa utaratibu... Yeye aliyefanya njia jangwani na kwenye bahari, anapenda pia pafanyike njia ya kutosha ya kuingia na kutokea nje ya jiji. Huwezi kuwa na jiji la wakazi milioni tano alafu ukawa na exit ambayo ni kichochoro. Pakitokea sunami hapa Dar, tutakimbiaje wote na kutoka nje ya jiji hili kwa upesi kama hakuna njia pana. Busara tu ndiyo inahitajika hapa...
 
Kwani si washaruhusiwa kuwa wavunje huo msikiti????? SASA nini kingine wanachotaka,,, kawaida msikiti sio Mali ya mtu binafsi kama ilivyo kwa MAKANISA kuwa yanamilikiwa na watu binafsi,,,

KAMA vipi wawaambie bakwata waende na shehe mkuu wa Daressalam yule mpenda camera,wabebe nyundo na tindo wakavunje kuonyesha uzalendo,,,,tena na ITV na media zingine watakuwepo
 
tunahitaji nyumba za ibada kwa ajili ya kutengeneza ubinadamu wetu wa ndani lakini pia tunahitaji barabara kwa maisha yetu ya kila siku, ifike wakati tutafute mwafaka ikiwezekana kuwanunua walio jirani ili miskiti na makanisa yafidiwe kwa kuwa vyote pamoja na barabara si mali ya mtu mmoja ni kwa ajili ya matumizi ya kijamii.
 
NI UJINGA. KWANI HUO MSIKITI ALIJENGA NANI?
NANI ANAYELIPA BILI YA UMEME KAMA UPO?
MAMBO MENGINE YANAHITAJI AKILI NDOGO TU KUELEWA HATA HAYAHITAJ ELIMU YA SHULE YA MSINGI.

Back
Top Bottom