MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
Tukio hilo la kusikitisha, limedaiwa kutokea hivi karibuni Chang'ombe Toroli ambapo sheikh huyo aliyekuwa akifundisha Madrasa ya Istiqama, amedaiwa kuwa na tabia ya kumwingilia kimwili binti ambaye alikuwa mwanafunzi wa hiyo madrasa, kwa muda mrefu sasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho tunakipa hifadhi ya jina lake, wakati sheikh huyo akiendeleza tabia hiyo chafu ya ufuksa, wazazi wa binti hawakuelewa chochote, hadi siku za hivi karibuni waliposikia kutoka kwa majirani kuwepo kwa mchezo mchafu wa kimapenzi kati ya sheikh huyo na binti yao.
Habari zaidi zinasema kuwa kufuatia hali hiyo, wazazi wa binti huyo walimbana binti yao, ambaye hatimaye alikiri kuingiliwa kimwili na sheikh huyo.
Hata hivyo, binti huyo aliwaeleza wazazi hao kuwa alikuwa akitishiwa na kiongozi huyo wa dini asitoe siri hiyo kwa mtu yeyote.
Waandishi wetu walifanikiwa kuongea na mama mzazi wa binti huyo (jina tunalihifadhi) ambaye alikiri mwanae kufanyiwa kitu mbaya na sheikh huyo.
Nilimwita binti yangu na kumbana aeleze ukweli ndipo akaniambia kuwa sheikh huyo mara kwa mara amekuwa akimchezea matiti, kumtomasatomasa, na kumwingilia kimwili, na muda wa kutoka madrasa unapofika humwambia awe wa mwisho ili wafanye mchezo huo hapohapo msikitini, alisema mama huyo.
Mzazi huyo aliendelea kuwaeleza waandishi wetu kuwa, waliitisha kikao na viongozi wa Msikiti wa Toroli, walimu wa madrasa yote ya Toroli pamoja na wazee wa kiislamu na kujadili juu ya suala hilo, ambapo iliamriwa chuo hicho kifungwe hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Wakati sakata hilo likipamba moto, mshtumiwa alifanikiwa kutoroka kwa kuogopa kukamatwa.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wazazi walimpeleka binti yao Hospitali ya Temeke kwa vipimo mbalimbali, daktari aliyempima alisema kuwa ni kweli binti huyo huwa anaingiliwa kimwili, lakini hakukuwepo mbegu za kiume zilizopatikana kwenye vipimo.
Wazazi wa binti huyo waliamua kwenda Kituo Kidogo cha Polisi Keko na kumfungulia kesi yenye jalada namba KPP\ RB\2269\2008, lakini kutokana na uzito wa kesi yenyewe, ilihamishiwa Kituo kikubwa cha Chang?ombe na kufunguliwa jalada lingine lenye namba CHA\RB\7796\2008.
Waandishi wetu walifanikiwa kuongea na mmoja wa viongozi wa msikiti wa Toroli ambaye alikiri kufungwa kwa muda kwa madrasa ya Istiqama kutokana na madai ya sheikh huyo kumuingilia kimwili mwanafunzi wake. Hadi hivi sasa uchunguzi bado unaendelea na sheikh huyo anatafutwa na polisi kujibu tuhuma hizo.
Nimeikama Global Publishers