Sheha Mpemba Faki, Mbunge mteule wa Konde (CCM) ajiuzulu

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,335
2,000
Muislamu wa kweli hawezi kuwa sehemu ya dhuluma na uonezi. Hongera kwake kwa kufanya uamuzi sahihi
Hii ideology ndo imezifanya nchi za kiislamu kustawi kiuchumi.Na kuondoa gap Kati ya watawala na watawaliwa.
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,258
2,000
Huyu ameshasoma ramani,yaani ile dua iliyofanyika tarehe 27/10/2020 inafanya kazi wezi wa kura wanapukutika mdogo mdogo, kaogopa ghadhabu ya Mungu huyo. Hadi 2025 wengi tutakuwa tumewazika. Mungu hadhihakiwi,wao wana mitutu ya bunduki sisi tuna Mungu
me nadhani hii ni njia nzuri sana isiyokuwa na usumbufu.
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,936
2,000
ACT wametishia kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, hivyo ccm wameona watazidi kuchafuka, hatimaye ikabidi wamtake huyo mbunge ajitoe kuepusha chama chao kuzidi kuchafuka.
Ila mjue wapinzani wao siku zote wameibiwa kura. Kama unavyohisi ni sawa bora warudie tena uchaguzi huku sheria na taratibu ikizingatiwa kwa uwazi zaidi tuone nani anachukua jimbo.

Sio watu kulilia tu kufikiri uongozi ni kugawiwa kama sima washibe wakati ni kuchaguliwa na wananchi..ngoja tuone kinachofuata.
 
Brother Kaka

Member
Jun 11, 2013
81
125
Yaani anajiuzulu kabla ya kula kiapo. !!?? Tayari aneleta hasara ya kufanya uchaguzi kwa mara nyingine tena.
 
chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
769
1,000
Taarifa

Mbunge wa CCM amejiuzulu

View attachment 1877201
Huyu Shehe Mpemba kuna kitu alichoshtukia manake kaona sio haki kunufaishwa na dhulma, kutokana na inavosemekana kashindwa na mpinzani wake kwa kura asilimia 70%, dhulma ikampitisha yeye wa 30% awe mbunge wa konde. naona hiyo ndio iliomsababisha khofu ya kumuogopa Mungu imfanye ajuuzulu huo ubunge.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,864
2,000
Ila mjue wapinzani wao siku zote wameibiwa kura. Kama unavyohisi ni sawa bora warudie tena uchaguzi huku sheria na taratibu ikizingatiwa kwa uwazi zaidi tuone nani anachukua jimbo. Sio watu kulilia tu kufikiri uongozi ni kugawiwa kama sima washibe wakati ni kuchaguliwa na wananchi..ngoja tuone kinachofuata.
Kwa taarifa yako hata huyo aliyejiuzulu dhamira inamsuta maana anajua fika hakushinda. Na ikitokea siku ccm wakakubali uchaguzi huru na wa haki, hata wakishinda hawataweza kuvuka 55%, na hawataweza kupitisha chochote watakacho bungeni kama wafanyavyo sasa.

Usidhani ccm wanafurahia kutangazwa washindi kihuni, bali hawana jinsi, na wanaogopa kuachia madaraka kwa njia ya amani maana wengi hawawezi kujitegemea, na wana miradi waliyoipata kwa wizi, na hawalipi kodi. Kitisho kikubwa kabisa ni usalama wao wakitoka madarakani, haya wanayowafanyia kina Mbowe wanahisi yatawarudia. Hivyo kila wakiwaza maisha bila madaraka, ama uchafu wao kulindwa, wanaona bora wanajisi uchaguzi.
 
chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
769
1,000
ACT wametishia kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, hivyo ccm wameona watazidi kuchafuka, hatimaye ikabidi wamtake huyo mbunge ajitoe kuepusha chama chao kuzidi kuchafuka.
Kwa maana hiyo, utafanyika uchaguzi mwingine mshindi atakua wa ACT, ili chombo kisiende mrama?
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,718
2,000
Yaani anajiuzulu kabla ya kula kiapo. !!?? Tayari aneleta hasara ya kufanya uchaguzi kwa mara nyingine tena.
CCM wanachezea sana kodi zetu. Ila mwisho wa ubaya ni aibu na mshahara wa dhambi ni mauti. Wizi wa kura ni dhambi na wote walioshiriki lazima mabaya yawakute hata isiwe kifo lakini kamwe hawatapata amani ya moyo.
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,105
2,000
ACT wametishia kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, hivyo ccm wameona watazidi kuchafuka, hatimaye ikabidi wamtake huyo mbunge ajitoe kuepusha chama chao kuzidi kuchafuka.
Kwa hiyo akishajitoa kama hivyo kinachofuata ni nini?
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,105
2,000
Huyu ameshasoma ramani,yaani ile dua iliyofanyika tarehe 27/10/2020 inafanya kazi wezi wa kura wanapukutika mdogo mdogo, kaogopa ghadhabu ya Mungu huyo. Hadi 2025 wengi tutakuwa tumewazika. Mungu hadhihakiwi,wao wana mitutu ya bunduki sisi tuna Mungu
Mungu siyo Lisu wala Amsterdam
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom