Shauri la malezi ya mtoto: Diamond, Hamisa Mobetto mambo safi

GTA

JF-Expert Member
Jul 25, 2013
878
649
Diamond-Platnumz-and-Hamisa-Mobeto.jpg

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto, imekwenda vizuri.

“Niseme tu mambo yameenda vizuri na kama mnavyojua mambo ya mahakamani ikitokea ninahitajika nitakuja,” amesema.

Diamond alifika mahakamani hapo leo Februari 8, 2018 kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul iliyofunguliwa na Mobeto. Amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto.

"Tunahitaji kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuwa katika mstari kwa sababu vitu vidogo vinaharibu upande wa mama na upande wa baba kwa hiyo tulikuwa tunaweka mambo sawa ili kesho na keshokutwa yasilete sintofahamu baina yetu,” amesema na Diamonda na kuongeza:

“Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu anakuwa na mawazo yake, kwa hiyo ni lazima kumjenga mtoto na kuhakikisha kuwa mtoto anajengwa na kulelewa katika malezi bora.” Alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha anachoweza kumudu kutoa kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo, amesema kiasi cha fedha kinazungumzwa zaidi lakini mtoto anahitaji matunzo mengi.

"Kiasi cha pesa tunachoandika sehemu kama hizi tunazungumza tu. Mtoto ana mahitaji mengi wakati mwingine mtoto wako unaweza kumpa hata Sh100 milioni. Huwezi kusema siwezi kumpa kwa sababu niliandikisha nitampa Sh100,000.

Tumeweka mazingira mazuri ya kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora,” amesema. Msanii huyo amesema kupitia kesi hiyo amejifunza vitu vingi na kwamba, mazungumzo yao ndani ya mahakama hiyo ni siri yao: “mambo yamekwisha.

” Amesema atahakikisha mtoto huyo anakuwa katika mazingira mazuri, kumsomesha kadri ya uwezo wake utakavyoruhusu kwa maelezo kuwa maisha ni kupanda na kushuka.“Kuna wakati unakuwa hauna unasema leo mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha ndivyo yalivyo,” amesema.

-Mwananchi-
 
Diamond una akili sana lakini unakubali kupelekeshwa na kufanyiwa maamuzi na yule mtu mzima Zari. Tangu mwanzo ungeisikiliza nafsi yako wala yasingefika mahakamani. Tatizo ulikuwa unamsikiliza Zari ili kumridhisha. Ona sasa aibu iliyokupata. Msanii mkubwa kama wewe kupangiwa malezi na mahakama.
 
Dogo amekua sasa kama angewaza ivi mapema hakika wasingefika hapo ni aibu kupangiwa matumizi ya mtoto wako na mahakama au watu wengine.
Kwa mujibu wa maelezo yake ya awali ambayo hayajawahi kukanushwa, sidhani kama ni sahihi kusema kupangiwa na mahakama! Tangu zamani, jamaa sio kwamba aligoma kuhudumia! Walifikishana mahakamani baada ya Hamisa kudai awe anapewa 5M for child support na jamaa akaona 5M ni nyingi mno!!!
 
Diamond una akili sana lakini unakubali kupelekeshwa na kufanyiwa maamuzi na yule mtu mzima Zari. Tangu mwanzo ungeisikiliza nafsi yako wala yasingefika mahakamani. Tatizo ulikuwa unamsikiliza Zari ili kumridhisha. Ona sasa aibu iliyokupata. Msanii mkubwa kama wewe kupangiwa malezi na mahakama.
Ungekuwa wewe ungekubali kutoa 5M kwa mwezi kirahisi rahisi tu?!
 
Mnamtaman zari eee

Huyo mabeto alitaka million 5 kwa mwezi,zari kahusikaje hapa?pyeeeee
Diamond una akili sana lakini unakubali kupelekeshwa na kufanyiwa maamuzi na yule mtu mzima Zari. Tangu mwanzo ungeisikiliza nafsi yako wala yasingefika mahakamani. Tatizo ulikuwa unamsikiliza Zari ili kumridhisha. Ona sasa aibu iliyokupata. Msanii mkubwa kama wewe kupangiwa malezi na mahakama.
Wapambane wao lakini alee mtoto na kile kibibi kiache kupendelea wa kusini tu
 
Kwa mujibu wa maelezo yake ya awali ambayo hayajawahi kukanushwa, sidhani kama ni sahihi kusema kupangiwa na mahakama! Tangu zamani, jamaa sio kwamba aligoma kuhudumia! Walifikishana mahakamani baada ya Hamisa kudai awe anapewa 5M for child support na jamaa akaona 5M ni nyingi mno!!!

Mwanamke hakukurupuka tu kukaza 5M lazima kulikua na tatizo sehemu hasa upande wa pili walipoanza mambo ya kienyeji naamini alienda mahakamani akijua hawezi kupata hizo sarafu ila nae aliamua kumwaga mboga.
 
Kwanini unadhani tatizo lilikuwa upande wa pili?! Of course, tatizo lilikuwepo na lilianza baada ya Hamisa kuanza kuvujisha picha za faragha za yeye na Diamond wakati walikubaliana suala la kupeana ujauzito liwe siri for the sake of Diamond's family!

Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe; kabla hawajakorofishana alikuwa anatoa 70K per day tena hata kabla Hamisa hajajifungua!! Sasa walipokorofishana, jamaa akaona ujinga, ikiwa walishakubaliana for the sake of Diamond's family hili jambo liwe siri kwanini Hamisa anakusudia kumharibia!!!

Kuona hivyo, yale mahusiano ya kirafiki ya wapenzi yakakoma na mtoto alipozaliwa, Diamond akamtumia Mwanasheria wake ku-handle issue ya matunzo ya mtoto!! Kuangalia sheria za Tanzania, matunzo ni 70K per month lakini wakakubaliana na Mwanasheria wake awe anapeleka 200K per month. Hiyo 200K Hamisa akakataa ndo akakimbilia mahakamani na kudai 5M.

Sasa hivi hapo mtu unaweza kusema tatizo lilikuwa upande wa Diamond?! Ni mwanaume gani anaweza kukubali kuweka hadharani kirahisi kwamba amezaa na mwanamke mwingine wakati ana famili yake?!

Na wakati Diamond anazungumza suala la kutoa 70K per day na kumnunulia Hamisa gari, watu walidhani ni stunts tu za Diamond hadi siku Idris Sultan alipolikoroga:

Hamisa02.png

Hiyo post, ikamfanya Hamisa amjie juu Idris Sultani!​

Hamisa.png

Sasa, ukimsoma hapo Hamisa, utaona anakiri kulamba hizo 70K per day! Sasa ikiwa mtu alikuwa anahudumia mimba kwa pesa yote hiyo, ndo angekacha kuhudumia mtoto?!

Tatizo ndo kama hiyo habari inavyosema hapo juu... Hamisa alikuwa anashikwa makisio na watu badala ya kula kimya kimya! Mwanzoni ile kuvujisha picha ilikuwa ni kwa ajili ya kumkomoa Zari! Baadae wakaingia akina Mange Kimambi hapo hapo na kuwa consultants wake wa masuala ya child support!
 
Mahakama imeamua Diamond awalipe Hamisa na Majizo shilingi milioni 15 kwa wiki. Mimi nafikiri hazitoshi, hapo wangeongezwa nyingine 5, maana maisha yamepanda sana siku hizi, hasa bei ya petroli. We fikiria kuendesha gari kila siku inawa-cost Hamisa na Majizo shing' ngapi?
 
Mahakama inipangie kiasi cha kumpa imenipa ajira? Diamond 08/02/2018
 
Kupelekana mahakamani kwa issue za child support ni UZWAZWA......Kama alikuwa anauza Mechi hayo ndio matokeo hasikimbie MAJUKUMU YAKE.
 
kweli mahakama kiboko mbwembwe zote zile mara nimetuma mwanasheria alipe laki mbili chakushangaza kawa mdogo kama piriton shubaamit
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom