TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,603
68,509
Wana Jf,

Kuna habari za kusikitisha na uhakika kuwa msanii aliyekuwa maarufu kwa jina la Sharo Millionea jina lake Hussein Ramadhani, msanii wa muziki na maarufu katika kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Tanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

tuzosharonmajuto.jpg


attachment.php



====================
UPDATE
====================

Kamanda wa Polisimkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwao. Sasa naweza kusema R.I.P Sharomilonea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga kathibitisha - kutoka Clouds radio

Picha za gara aliyopata nayo ajali Marehem Hussein a.k.a Sharo millionea.

390328_172001262941773_1626460190_n.jpg


252283_172000949608471_2058031321_n.jpg


30372_171998639608702_2102846982_n.jpg
 
Ndugu wana jf sina hakika na hii habari but katika pitapita yangu mtaani nikaskia hizi habari ambazo sio rasmi,tunaomba wenye uhakika basi watujuze maana wasanii wetu ndo wanazidi kuisha,nawasilisha
 
inasemekana kuwa msanii nguli wa comedy na muziki sharo milionea amefariki dunia kwenye ajali ya gari iliyotokea huko muheza tanga. Source: channel ten tv
 
Kuna habari zinasema msanii Mchekeshaji Sharo Millionea kafariki dunia kwa ajali ya gari huko Muheza, Tanga.
(Habari hazijathibitishwa)

SOURCE; Channel ten.
 
Confirmed mkuu ni kweli ametuaga jamaaa.....

Nimepata habari kutoka kwa Steve Nyerere jamaa amevuta.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kuna habari zinasema mchekeshaji sharo millionea kafariki dunia kwa ajali ya gari huko Muheza, Tanga.
(Habari hazijathibitishwa)

SOURCE; Chanel ten.
nami nimeiona hii habari channel ten ............RIP sharo!!!
 
ukiangalia chanel ten sasa hivi wanapitisha ufito kuelezea kuhusu hiyo ajali ingawa wanasema bado hazijathibitishwa.
 
Lala Salama Sharo,,,mungu wa majeshi atakufufua siku ya mwisho..ila ningepata faraja sana kama ningejua kama ulipata muda wa kutubu dhambi zako!
 
no way, nilikuwa nampenda sababu ya watoto kupenda tangazo lake.

rip sharo
 
Back
Top Bottom