Swahilian
JF-Expert Member
- Apr 28, 2009
- 591
- 66
Nilisikitika hata mie baada ya kutangazwa matokeo yale, japo ndio hivyo ilishatamkwa Dr. Ally M. Shein Ndio Rais Mteule wa Zanzibar.
Hamad alipoitwa alipongeza ushindi huo japo alitamka dhahiri mbinu chafu za baadhi ya watendaji wa tume ya uchaguzi ( ZEC )
Hakika kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwake, aliamua kukaza moyo na kutoa kauli ya mdomoni kuwa Dr. SHEIN ametawazwa kuwa Rais na alisisitiza kwamba ktk uchaguzi huo hakuna mshindi yaani kama ungelikuwa mpira wa miguu ni matokeo ya sare au suluhu baina ya CUF na CCM.
Pembeni ya hapo kwa wale tulomtathimini kwa undani Maalim hasa usoni, alikuwa si yule Maalim mcheshi, mchangamfu na anayejiamini.
Alifanya kila jambo kama amelazimishwa au inambidi afanye hivyo kwani hakukuwa na njia mbadala.
Hisia na Mtazamo halisi wa Hamad (Sharif) umejionesha zaidi ktk machozi yalokuwa yakimtoka kila alipokuwa akizungumza, yalimchuruzika kwa vipindi japo aliweza kujikaza kisabuni asiangue kilio kikubwa.
Pole sana Hamad kwa kuumia, mie niliyaona machozi yako yalonipa ujumbe fulani ktk maisha.