Share za ACACIA zazidi kuporomoka baada ya TRA kupeleka Tax Invoice

Hivi katika washauri wa Mh. Raisi hakuna hata mmoja aliyesoma Corporate Finance? Achana na Uchumi, achana na uhasibu. Kama kuna mshauri huyo mwenye hiyo elimu asinge kubali mshauri this way ambapo mambo yanaharibika na nchi haitakuwa salama kiuchumi. Naona mnafurahia shares za acacia kuanguka, wengi wenu hamjui maana yake. Tutalipa gharama (we will pay the price) whichever the outcomes.
Poor thinking yani umpelekee madai hisa zishuke wewe uogope ni zaidi ya woga wa kike.
Na hapo hata mgoni hatujaufunga bado.
Wao wametuongopea wewe ukaa na fikra finyu kiais hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makusanyo ya TRA kwa mwaka ulioisha kutoka VYANZO VYAKE VYOTE ni less than USD 7 bn/-. Leo wanaidai ACACIA 190/- about USD 19 b/- kwa mwaka. Hivi inaingia akilini mapato ya kampuni moja ni karibu mara tatu ya makusanyo yote ya kodi ndani nya nchi ile ile? Hebu tuacheni mizaha wajameni.
Huwe unasoma vitu uelewa b4 hujachangia hayo ni malimbikizo ya miaka 17 pamoja na penalties zake.
Na sio mwaka mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tutakuja kupata mwekezaji wa level ya Barrick tena kweli?
Ni heri asipatikane kama ni mwizi, kabla ya Barick miaka ya 1994 wachimbaji wadogo waliingiza kipato kikubwa kuliko hao tuliowaita wawekezaji, Mh Mrema aliwaruhusu wauze madeni kupitia mabenki na hasa NBC, mawazo yangu ni TUNAWATAMANI WAWEKEZAJI LAKINI KAMA NI WEZI MADINI YAACHWE, KIKIJA KIZAZI CHENYE AKILI WATACHIMBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Dar zipo Mkuu,kuna wazawa wenzio waumia

Pole sana wazawa wenye hisa za ACACIA. Lakini kwa wengine ACACIA ni kampuni la kibeberu, acha hisa zao ziporomoke, kampuni lifilisike, lifungwe, lidaiwe, life. Kama alivyosema Magufuli akiwa Singida leo, ACACIA wakafie mbele!

By the way, wanavyosema ACACIA inachangia pato la taifa, hivi najiuliza, unachangiaje GDP kama mapato yako yote yanapelekwa nje ya nchi? Tena sio yanapelekwa nje, ni kwamba yanabaki nje. Ndege inatua mgodini inachukua dhahabu, malipo yanakuwa yashafanywa.

Tume ya Osoro imesema, na ACACIA wamekiri, kwamba makontena ya makinikia yanakuwa yashalipiwa na wateja huko huko Ulaya kabla hayajaondoka nchini, hivyo mteja yuko Ulaya; wana hisa wako London; benki ya ACACIA iko London. Pesa huku inakuja kufanya nini? Haikanyagi. Inaingiaje kwenye hesabu za GDP ya Tanzania?
 
Pole sana wazawa wenye hisa za ACACIA. Lakini kwa wengine ACACIA ni kampuni la kibeberu, acha hisa zao ziporomoke, kampuni lifilisike, lifungwe, lidaiwe, life. Kama alivyosema Magufuli akiwa Singida leo, ACACIA wakafie mbele!

By the way, wanavyosema ACACIA inachangia pato la taifa, hivi najiuliza, unachangiaje GDP kama mapato yako yote yanapelekwa nje ya nchi? Tena sio yanapelekwa nje, ni kwamba yanabaki nje. Ndege inatua mgodini inachukua dhahabu, malipo yanakuwa yashafanywa.

Tume ya Osoro imesema, na ACACIA wamekiri, kwamba makontena ya makinikia yanakuwa yashalipiwa na wateja huko huko Ulaya kabla hayajaondoka nchini, hivyo mteja yuko Ulaya; wana hisa wako London; benki ya ACACIA iko London. Pesa huku inakuja kufanya nini? Haikanyagi. Inaingiaje kwenye hesabu za GDP ya Tanzania?
Inaingia kwenye GNP

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Inaingia kwenye GNP

Same difference.

Take one divide by the population you get the other.

Pesa ambayo imelipwa na mteja New York kwenda benki ya ACACIA London, wakalipwa wanahisa London, haijagusa mzunguko wa pesa Tanzania, inaingia vipi kwenye GNP ya Tanzania?
 
Naanza kuona kwa nini Tundu Lissu yuko ndani...huenda kuna vitu vinafanyika na wengi hatuwezi kuona. Kwenye majukwaa ya kisiasa na kile kilicho nyuma ni mambo mawili tofauti. Huenda Tundu Lissu anashinda/kukesha sehemu wakipeana mbinu za kijasusi zaidi namna ya kudeal na mzungu. I am just thinking, si lazima niwe sahihi!!
Wakati ripoti zinatayarishwa, kuna watu walidukuliwa simu zao na kufuatiliwa nyendo zao wakati wakiifuatilia tume zote mbili
 
Wao wanadai miaka yote wamechimba kwa hasara, tunawasaidia wasiendelee kupata hasara !
 
To put the size of the bill in perspective, Acacia, which is majority owned by Barrick Gold Corp., had total revenues of $1.05 billion last year and has reported sales of a total of $7.7 billion since 2009.

The $40 billion tax bill is more than twice what all top five global gold miners (including Barrick) combined have paid in taxes since 2000!” Hunter Hillcoat, an analyst at Investec Plc, wrote in a note to investors Tuesday.

At least two senior employees have been detained for questioning by Tanzanian authorities this month, while other employees have been interviewed by the police. On Friday, Acacia said the dispute had depleted its cash balance to $176 million from $318 million a year earlier and that it will have to shutter its flagship Bulyanhulu mine at the end of this quarter if the situation is not resolved.
Ni shida yao, wajipange kupambana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo tunayomfanyia Barrick kwa sasa dunia nzima ya wawekezaji it's a talk of town.
Watu wanaangalia jinsi tunavyomkomesha Barrick , tunavyoharrass wafanyakazi wake, tunavyoua thamani yake kwenye soko la hisa with just 'Sukuma land allegations'

Halafu kesho tuwafuate wawekezaji sijui na nyimbo gani,tuwaambie waje wawekeze?
Lazima wajiulize, kama tumeweza kuutendea hivi mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu?
Humu jf kuna vijitu vijinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu data nyingi za wazungu ziko wazi ukizitafuta utapata sasa hapa kwetu ripoti tumeambiwa ni ya rais!! hata anayetuhumiwa hajapewa huu si ujinga wa kiwango cha lami aka uzazwa!
Ripoti za acacia wanadai wanapata hasara miaka yote waliokuwepo hapa katika migodi yote ! Au hukumsikia CAG !?
 
Back
Top Bottom