SHANGWE : Afisa elimu Iringa awapagawisha wanaCCM, atabiriwa kula shavu kubwa wizarani

C

Cliffhanger

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2018
Messages
412
Points
1,000
C

Cliffhanger

JF-Expert Member
Joined May 22, 2018
412 1,000
Naam ,baada ya yule mkuu bora kabisa wa mkoa kule mbeya ,kipenzi cha wana ccm bwana chalamila ambaye break ya kwanza baada ya kupewa dhamana ya kumuwakilisha Rais jijini mbeya alisema kipaumbele chake ni kumujondoa sugu kusema ya kwamba WANAOMPINGA MAGUFULI WATAPIGWA SINDANO ZA UKICHAA ,jamaa mwingine toka kanda hiyo ambaye ni afisa elimu naye ametoa kauli ya kishujaa iliyopokelewa vyema na wana ccm mtandaoni huku wengi wakimuomba muheshimiwa Rais ampe cheo wizarani ikibidi hata awe katibu wa wizara ya elimu

Mwanaharakati huyo wa kujitegemea na mzalendo toka iringa alisema....ANAYETOKA NA TAULO CHUMBANI KWA MAMA YAKO NDIYE BABA YAKO,HAIWEZEKANI WALIMU MLIPWE MSHAHARA NA SERIKALI YA CCM HALAFU MSHABIKIE UPINZANI,TUKIKUBAINI TUNAKUTAFUTIA HATA KESI YA UBAKAJI AU UHUJUMU UCHUMI UKAFIE GEREZANI

Ikumbukwe hata Rais Magufuli alishawahi kuwashangaa wakurugenzi wa wilaya na mikoa kwamba inakuwaje kwenye uchaguzi wanatangaza mpinzani kashinda wakati yeye ndiye anawapa mshahara na magari,ikumbukwe pia RPC wa Arusha aliwahakikishia CCM ushindi akwapigia na saluti na kuwasihi wasiwe na wasiwasi,HUO NDIYO UZALENDO TUNAOTAKA.View attachment 1180977
Ni mwendo wa kubatizana kwa moto kama hauchomwi sindano ya ukichaa basi utapewa hata kesi ya uhujumu uchumi
Kama kweli huyu ni mtumishi wa serikali ina maana kauli aliyoitoa ya "HAIWEZEKANI WALIMU MLIPWE MSHAHARA NA SERIKALI YA CCM HALAFU MSHABIKIE UPINZANI,TUKIKUBAINI TUNAKUTAFUTIA HATA KESI YA UBAKAJI AU UHUJUMU UCHUMI UKAFIE GEREZANI" ni msimamo wa serikali mpaka hapo mwenye mamlaka atakapokanusha.

Ofisi ya DPP na IGP inatakiwa itoe tamko kama ni kweli watanzania wanaoshabikia upinzani wanabambikiwa kesi za ubakaji na uhujumu uchumi ili wafie gerezani!
 

Forum statistics

Threads 1,336,416
Members 512,614
Posts 32,538,737
Top