Shangilia za CCM kwa CUF kunaonyesha CCM bado ina uwezo wa kuvuruga wapinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shangilia za CCM kwa CUF kunaonyesha CCM bado ina uwezo wa kuvuruga wapinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Feb 9, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Haitulii akilini kwangu kabisa! Wabunge CCM kushangilia CUF? Halafu CUF kinajiita chama cha upinzani? Bila kubebwa na njama za CCM kutoa tafsiri mpya ya kukubali hoja ya tafsiri mpya ya kanunu CUF wangekuwa wanatamba leo hii?

  jamani hebu tuwe wakweli na tufikiri angalau kidogo basi. Hivi kweli CCM inaweza kuchangamkia na kufurahia masuala ya upinzani kwa ajili manufaa ya upinzani na siyo manufaa yake?. Hii inawezekana kweli? Yaani CCM sasa hivi inakuwa-concerned sana hali katika upinzani hivyo inachukua hatua na kufanya maamuzi kuhusu kuboresha masuala yao?

  Mtu anaye-believe nonsense ya namna hii akapimwe akili. Daima CCM, kama vilivyo vyama vingi tu Barani Afrika, inataka kubakia madaraka daima dumu, na mambo yakiwa magumu, basi inakuwa hata tayari kuingia uswahiba na chama kingine kuunda serikali ya umoja ili iendelee kukaa madarakani, kwani inajua katika serikali hiyo ya umoja yenyewe ndiyo mwenye maamuzi makuu.

  Hivyo ndugu zangu, shangilia zote za CCM Bungeni jana kwa CUF ni kielelezo tosha kwamba inajua inachokipanga, CCM siyo wajinga. Mwisho wa siku CUF ndiyo itaonekana wajinga, kama siyo wasaliti.

  CCM wanajua fika kwamba Chadema ingebakia ndiyo kambi rasmi ya upinzani, CCM ingeanza kutafuta njia ya kutokea. Sasa hivi inaona angalau siri zao na ufisadi wao utafunikwa.

  Long live Tanzania!
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata mie nilishangaa sana jana! Bila shaka kama ulivyosema CCM ndiyo itakayonufaika na yaliyotokea jana.
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,421
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Sasa wew mtu akimshangilia mchumba wake wewe waona ajabu!!!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0  Imenikumbusha mwaka 2005 baada ya uchaguzi. Mambo yalikuwa hivihivi, kinyume chake. CUF walikuwa mwiba kwa CCM, huku Chadema walionekana maswahiba ingawa walikuwa na wabunge 5 tu hivi. Wakati wa uchaguzi wa kutafuta Mbunge kutoka upinzani kwa ajili ya Bunge la Afrika, waliogombea ni Fatma Maghimbi (CUF) na Phares Kabuye (RIP) wa (TLP). Kabla ya kura wengi tulijua kuwa atakayechaguliwa ni Kabuye kwani Wabunge wa CCM (ambao ndiyo wengi) wasingempa wa CUF -- chama adui yao wakati ule!

  CCM Bwana!!!! Wee acha tu. Kuna siku upepo wa kisiasa ukibadilika tena CUF watajikuta siyo blue-eyed boy wa CCM. Wakisha kuwafyonza kama kipande cha chungwa basi hukitupilia mbali. CCM huwa hawana uswahiba wa kudumu, bali ni masilahi ya kudumu.
   
 5. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ndugu yangu Counterpunch, ni ukweli kabisa kuwa siyo barani Africa tu bali dunia nzima chama tawala chochote hakiwezi kuwa na urafiki na chama cha upinzani, unless kuna kitu wanakitaka/wanategemea kutoka kwa chama hicho cha upinzani.

  Hiyo inawezekana tu kama vyama hivyo vinashirikiana kuunda serikali wala si vinginevyo. Vyama vingine vya NCCR, UDP, TLP vinashingiria bila kujua.

  CUF wanashirikiana kuund serikali na CCM. Mheshiwa Seif ni makamu rais wa Zanzibar. Ni vipi vyama vya upinzani watakaa pamoja kujadili mambo ya namna ya kupambana na watawala na mtu mmojawapo yupo kitka kikao hicho??? Huo ni upopo tu!!
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na kwa nini walete chokochoko hii wakati huu ambapo Chadema ndiyo chama kikubwa cha uipinzani, na siyo wakati uliopita? Mwenye kujibu swali hili vizuri naweza kukubali yaliyotokea Bungeni jana ni sahihi.
   
 7. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hasira zinazidi kupanda
   
 8. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Kitu cha Mhimu Chadema wasimamie wanachokiamini, pia wawaelimishe wananchi nini kinachofanywa na wapinzani feki kama CUF, NCCR, TLP, halafu 2015 wananchi wataamua.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

  [​IMG]


  22.JPG

  525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

  Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

  Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

  Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

  Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

  Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

  Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

  Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

  Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

  Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

  (1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

  (2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

  (3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

  Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani imefika muda sasa, wazanzibari wakae kwao na bunge lao na watanganyika tuwe na letu... ilituweze kuongea mambo yetu wenyewe kwa mustakabali wetu...:twitch:
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  You have to learn politics

  Mlipenda wenyewe mgawanyiko, mngeweza kuzuia hali hii kutokea OK

  Ukibagua usishangae kubaguliwa ok!
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Na haka ka"Muungano" tukafanye nini?
  Tumpelekee mwenyewe mwalimu Musoma?
   
Loading...