Shangazi wanatishia kuniloga na wanashirikiana na polisi kunimaliza

Mali za bibi yakoo ni mali ya watoto wakee so kama mama ako hakupewa hapo mali ya urithi wewe hauna chako mzee kakomaee utafutee vyakoo..!
 
Yaani ni sawa na...

1.30,000×12=360,000 tsh.

2.40,000×12=480,000 tsh.

NB..Hapa haujapewa kwa mkupuo hapa hujakutana na wapangaji wasumbufu.

Ila ndiyo jamaa amekomalia hao wataweza hata kumfanya ndondocha ama wamtoe roho kabisa.
Kweli mkuu.
Pesa ndogo huua!
Taiz ya selo naona haijamuingia..
Ngoja wamuokotee nyayo zake wamfanye sasa ndondocha azilete kiulaini.
Zama za kujali mambo yako hizi
 
hivyo vijumba vya vyumba sita vimeua sana wakazi wa pwani. wataakua kweli ulipaswa kujipaga kifedha na kuganga ndio ukadao haki yako. sasa subili stroke
wajomba mashangazi wa kizaramo kindengereko wameondoa rafiki zangu wengi kuna mwingine chizz hadi md huu kisa kijumba cha ulithi
 
Aisee. Hii lazima itakuwa dar. Huyu alipaswa achapwe viboko hadharani ili iwe fundisho kwa wasubiri urithi kwa bibi zao. Pumbaavu sana
 
Nasikitika na kuumia katika maisha yangu sijawahi kulala kituo cha polisi wala kufika kituo cha polisi sababu mimi ni mtu mwema lakini cha ajabu nimelazwa kituo cha polisi siku 4 kwa mara ya kwanza bila ya kosa lolote nimetafunwa na mbu ,watemi manyapara wamenionea kwakuwa nililazwa selo la watukutu nimeumia kwakweli.

Shangazi zangu wakishirikiana na polisi wanataka kunimaliza na kunizulumu mali yangu.Shangazi zangu waliwapa rushwa polisi wanilaze ndani bila ya kosa lolote haki ipo wapi wajameni.

Ni Stori mdefu lakini bibi yangu alizaa watoto 4 ambapo wakike watatu na wa kiume mmoja.Mama yangu ni kati ya hao watoto wanne wa bibi yangu halali kwa uzuri bibi yangu amefariki na ameacha nyumba moja yenye vyumba sita.Siku 5 nyuma nilienda kudai urithi wa bibi yangu nikawataka shangazi zangu wanipe chumba kimoja niwe nachukua kodi kwasababu yule ni bibi yangu na mama yangu hayupo duniani hivyo nichukue haki ya mama na yangu kama mjukuu.

Wale shangazi wakaanza maneno na kukataa katakata na mimi nikawa mbishi iweje haki yangu waninyime ugomvi ukawa mkubwa nikatafuta kufuli nikaenda kufunga kwenye moja ya chumba .

Wale ndugu zangu walitishia kuniloga na walisema wazi wataniloga lakini sikutishika nikang'ang'ania haki yangu mali ya bibi yangu nataka chumba nipewe ili niweze kuyaendesha maisha yangu sasa nitaishi vipi ndipo walipoenda polisi na kuja kunikamata na kunilaza kituoni kwa siku nne na ushahidi ninao .Hii ni haki kulazwa kituoni bila kosa ? Sababu ya kusimamia haki yangu ?

Namshukuru mungu nimetoka ila nimeumia sana polisi kutumika kunikandamiza wakati hao shangazi zangu wanadai wataniloga na wananizulumu haki yangu.

Duniani ukiwa mnyonge utateseka sana na ndugu sio watu kabisa asikuambie mtu .kesi saizi ipo kwa mwenyekit lakini shangazi zangu hawataki kuelewa wana roho mbaya
Mali za urithi ni noma sana ztakuja kukutoa roho ww. Tafuta mali zako 2
 
Pole sana ndugu. Ila napenda kukushauri kwamba, ukomae tu kwa kupiga kazi ili siku moja na wewe upate vya kwako...kwa sasa kaa nao mbali hao watu, maana sio wazuri kwako.

Kugombania vitu kama hivyo, ni very risk ndugu yangu. Tena ukizingatia hapo hauna msaada wa mama....unaweza ukajikuta unalogwa kweli, na kuwa chizi totally.

Naomba ufahamu kwamba. Machizi wote mitaani, sio kwamba wamezaliwa na uchizi au walipata magonjwa ya akili tu. Bali wapo waliozaliwa wazima kabisa, ila kwa hizi hizi imani potofu, zikawafanya wawe machizi mitaani, na huku wakikosa msaada wa mtu wa kujitolea kuwanasua kutoka kwenye shida hile....mara nyingi ujikuta wakijifia tu wakiwa kwenye hali hiyo hiyo ya uchizi. So wapo walioharikiwa na maisha yao kwasababu kama hizo.

HII NDIO DUNIA MDOGO WANGU, KUWA CARE SANA.
 
Ila wewe jamaa wa ajabu saana,yaani unadai urithi wa bibi yako kwani wewe ni mtoto wa huyo bibi!?

Acha ujinga,unatia aibu kulalamika na kusema ni haki yako,uba haki gani hapo!?

Wenye haki ni watoto wa huyu bibi labda kama aliandika wosia na wewe upewe chumba!

Hv una miaka mingapi!?
 
Sijawahi wala kusikia mtu anadai urithi wa bibi yake tena mzaa mama, huweze dai mali ujombani.
 
ingekuwa mi ni huyo shangaz yako ningekufunga mwaka. una akili mgando sana shenz type
 
Duu wajukuu mnashida sana...

Unajiona upo sahihi kabisa kusema mali ya bibi yako unahaki nayo...

Kama wazazi wako hawajakuachia kitu ndiyo imetoka hiyo...

Mwenye haki na mali za bibi yako ni watoto zake tu na siyo wajukuu zake...


Cc: mahondaw
 
Kwani urithi wa wana wanawe unamaanisha nini kwenye bible?lol ni haki yake kudai urithi wa bibi
 
Back
Top Bottom