Shangazi: Tume ina majaji 4 lakini wote kama hawajui sheria na hukumu ipo kuwa Maandamano huwa hayahitaji kibali

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,563
2,000
NEC ina makamishna 4 majaji na nina hakika wanaelewa kuwa Mahakama ya Rufaani ilitoa HUKUMU kwamba wananchi hawahitaji KIBALI kutoka popote ili kuandamana PEACEFULLY. Polisi ijuilishwe tu lakini kazi yake si kutoa KIBALI! #FactCheck TUME isipate #ElectionFever https://t.co/mAScpweFMb

IMG_20200904_111908.jpg
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,226
2,000
Tuna majaji wa majina ambao kiuhalisia uwezo wao ni afadhali hakimu wa mahakama ya mwanzo mwenye weledi.

Majaji wetu wanaharibiwa weledi wao na ukada wao kwa CCM.

Kuna wajinga wengi tu unasikia eti ili uandamane unahitaji kibali cha Polisi! Unashangaa kama hawa watu huwa wanasoma sheria au ni tutusa wa kutenda lakini waliobeba vyeti vya usomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,986
2,000
Majaji wa ukweli walikuwa akina Nyalali, Mzavas, Rugakingira, Korosso, Mroso, Kisanga nk.

Hao hawakujua cha rais wala cha nani, wao walikuwa wanakufa na kitabu tu kinasemaje, Nyerere alipoona hivyo akaanzisha sheria ya kuweka watu kizuizini bila kufikishwa mahakamani enzi hizo maarufu kama (Detention Without Trial).

Nyerere alichoka kwani alikuwa akimburuza mtu mahakamani kwa hizi tuhuma za kipuuzi majaji walikuwa wakiwaachilia huru kiulaini kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi madhubuti.

Kwenye vyesi vya uhujumu uchumi mwaka 1984-1985 watuhumiwa waliachiliwa huru kwa kile majaji walichodai kuwa "Sheria ya uhujumu uchumi ilikuwa batili".
Wale ndio walikuwa majaji lkn hawa wa leo ni wachumia tumbo tu na makanjanja wa kisheria.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom