Shangazi kaja na mchumba kutoka kijijini...Mwenzenu nipo dillema!

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
Ni mwaka mmoja sasa umepita toka rafiki yangu kipenzi wa tokea primaly, sekondary mpaka chuo alipopata ajira ktk halmashauri fulani (sitaitaja jina) kama Afisa Utumishi. Takribani mwezi wa 6 sasa tangu rafiki yangu huyu anitake ushauri kwani amekua akisisitiziwa na ndugu zake wa pande zote wa upande wa baba na mama yake juu ya kuoa. Anamchumba wa kichaga aliyepo masomoni chuoni dsm mwaka wa 2 sasa akisomea mambo ya habari pale SJMC, Kifupi wanapendana na mimi pia nampenda shemeji yangu huyu kwa mapenzi ya dhati aliyonayo kwa rafiki yangu, siku zote nimekuwa nikiwatakia mema afikie lengo lao la kuishi pamoja(ndoa), majuzi kanipigia simu, kanipa taarifa kua shangazi yake mkubwa amekuja kutoka kijijini na binti ambaye amechaguliwa na ukoo kama mchumba/mke wake, shangazi yake amedai ujio wake ni kutimiza wajibu kama alivyoamuliwa na kikao cha ukoo pia akasema huko kijijini taratibu nyingine za ndoa zinaendelea. Jamaa kachanganyikiwa, ananiomba ushauri juu ya hili jambo, mimi nimeshindwa kumpa jibu coz sijui niegemee upande gani, shemeji yangu wa chuo namkubali, jamaa yangu sipendi agombane na ndugu zake pia.. Nimemwambia anipe muda then nitamjuza nin chakufanya.. Hapa alipo anasubiri ushauri wangu kwani tunaaminiana, tumeshirikiana, kusaidiana na kushauriana ktk mengi. Hapa nilipo nipo dillema ktk kutoa huo ushauri, jamani tusaidiane ktk hili, nini kifanyike hapo? Nimshaurije? Nawategemea sana ktk hili. Asanteni...
 
Suala la awe na nani ni la huyo jamaa yako,asimame kama mwanaume na awe na msimamo!
 
Suala la awe na nani ni la huyo jamaa yako,asimame kama mwanaume na awe na msimamo!
Mkuu msimamo gani? Kiafrika society/family ndio basic unity na mchumba watoka ndio mapenzi bora. Ktk hali hii kuchanganyikiwa lazima. Nipe ushauri mkuu!
 
dah,hizi mambo bado zipo eeh? tz nayo kubwa mno,inabidi zitengenezwe majimbo huru kama marekani sasa!
 
Hii dunia ukitaka kumfurahisha kila mtu utachanganyikiwa, mwambie achague kile anachofikiri kwamba ni kizuri kwake na kitampa furaha.

kama anashindwa kuamua, mwambie amwambie shangazi yake arudi na huyo dada kule alikotoka naye na yeye atawajulisha baadaye mipango yake.

Unanikumbusha mbali kidogo, mimi kuna brother yangu naye alitafutiwa mke na mahari ikawa imeshatolewa lakini jamaa alikataa na ilibidi mzee awe mpole na mahari ilirudi, sasa yeye anashindwa nini kuamua, cheo chenyewe afisa utumishi kama anashindwa kuamua mambo yake mwenyewe hao waajiriwa ataweza kuwaamulia mambo yao kweli.

Baadaye soma signature yangu hapo chini halafu umfowadie.
 
Aoe huyu aliyeletewa, mapenzi na kuzoeana kutaanza hukohuko kwenye ndoa.

Ilikuwa hivyo, tulipoanza kuhama makwetu na kwenda sehemu nyingine kutafuta maisha ndipo tukaanza na sisi 'kutafuta' wa kuoa. Achukue mke tu, simpo!
 
Ningemshauri Amege kwanza aona kama analipa! Maana totoz za Kijijini usipime hazijachakachuliwa sana.
 
hii nayo kali...amrudishe huyo binti na shangazi kijijini then nae aende kuwaoiga msasa...ikiwezekana aende na mchumba wake wa UDSM kujitambulisha rasmi.
 
afanye uamuzi kutokana na moyo wake unachotaka. Mwisho wa siku yeye ndo ataishi na mwanamke alomchagua c ukoo wala shangazi.

Meanwhile amwambie shangazi arudi na huyo binti!

Pia asimame kidete maana ana vita kali mbele yake.

Halafu haya mambo mengine uduwanzi sana, raha ya maisha ufanye maamuz mwenyewe uanguke au kufanyikiwa mwenyewe sio watu watoke wanakotoka kuja kuharibiana maisha na taratibu!
 
Huyo rafiki yako atambue kuwa mke yeyote atakayeoa hataishi na shangazi yake, mjomba, wazazi au watu wengine wa ukoo. Ni yeye atakayeishi naye. Yeye ndiye atakayekabili uzuri na ubaya wa huyo mke. Kwa hiyo ni LAZIMA afuate chaguo la moyo wake hata kama sio chaguo la wazazi au ukoo wake kwa kuwa hayo ndiyo maisha yake yote yaliyobaki. Watu wa ukoo watapinga sana lakini baadaye watasalimu amri. Tusiendekeze vimila VILIVYOKAUKA tayari.
 
Hii dunia ukitaka kumfurahisha kila mtu utachanganyikiwa, mwambie achague kile anachofikiri kwamba ni kizuri kwake na kitampa furaha.kama anashindwa kuamua, mwambie amwambie shangazi yake arudi na huyo dada kule alikotoka naye na yeye atawajulisha baadaye mipango yake.Unanikumbusha mbali kidogo, mimi kuna brother yangu naye alitafutiwa mke na mahari ikawa imeshatolewa lakini jamaa alikataa na ilibidi mzee awe mpole na mahari ilirudi, sasa yeye anashindwa nini kuamua, cheo chenyewe afisa utumishi kama anashindwa kuamua mambo yake mwenyewe hao waajiriwa ataweza kuwaamulia mambo yao kweli.Baadaye soma signature yangu hapo chini halafu umfowadie.
Mkuu nimekupata, nitamwelekeza ktk hili. Tatizo sipendi kuwa sehemu ya matatizo yake, nawasiwasi na ushauri/task aliyonipa then nashindwa kumkwepa kwa hili!
 
Aoe huyu aliyeletewa, mapenzi na kuzoeana kutaanza hukohuko kwenye ndoa. Ilikuwa hivyo, tulipoanza kuhama makwetu na kwenda sehemu nyingine kutafuta maisha ndipo tukaanza na sisi 'kutafuta' wa kuoa. Achukue mke tu, simpo!
Mmh! Vp huyu mchaga wake sasa? Ni mzuri wa tabia na sura, anajiheshimu na ni mstaarabu sana! Nahisi wataendana!
 
Back
Top Bottom