Shamsi Vuai Nahodha :'Acheni siasa za ukubwa wa majimbo'

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amewataka wabunge kuacha kushabikia ukubwa wa majimbo kuacha kasumba hiyo kwani haina maana yoyote kwa maendeleo.

Nahodha alisema kipimo kizuri kwa wabunge ni kuangalia utumishi wao uliotukuka, lakini si katika kupingana kwa kuangalia idadi ya watu waliopiga kura.

Alisema hayo alipojadili Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akifungua Bunge hilo mapema mwishoni mwa mwaka jana.

Katika kujadili hotuba hiyo, Waziri huyo alionekana kujibu kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupitia Chadema ambaye aliwahi kutoa kauli ya masuala ya uchache wa wapiga kura huko Zanzibar.

Nahodha alisema kama kipimo cha ubunge kinatokana na ukubwa wa majimbo, ni wazi kuwa wanaoongoza majimbo makubwa wangekuwa viongozi wa kambi za upinzani bungeni.

Katika mkutano wa bunge kuliibuka malumbano juu ya idadi ndogo ya wapiga kura katika majimbo ya Zanzibar ambao walielezwa kuwa idadi ya wananchi waliowachagua ni ndogo mno ukilinganisha na wale wa Bara.

"Katika michango ya wabunge kwenye hotuba ya rais, kumeibuka jambo moja ambalo nataka kulisema, nalo ni hisia za kudharau wabunge kutoka katika majimbo yenye uwakilishi wa idadi ndogo ya watu, huo si uungwana hata kidogo na suala hilo lisipoangaliwa linaweza kuharibu muundo na sura ya bunge," alisema Nahodha.

Waziri huyo aliyekuwa Waziri Kiongozi wa alimtolea mfano mbunge wa Jimbo la Ubungo na kumtaja kuwa angeweza kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

"Kama hoja ni ukubwa wa majimbo na idadi ya wapiga kura, basi mbunge wa Ubungo John Mnyika angeweza kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ama angekuwa Mwenyekiti wa Chama chake kwa kuwa na wapiga kura zaidi ya 450,000," alisema Nahodha.

Alisema kuwa ni vema Wabunge wa Bunge la Muungano wakawa na umoja ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila mmoja wao amefika katika bunge hilo kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania bila ya kuangalia ukubwa na idadi ya wapiga kura waliowachagua.
 
Back
Top Bottom