Shamsi Atetea Maslahi Ya Zanzibar Au Bara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamsi Atetea Maslahi Ya Zanzibar Au Bara?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Aug 8, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  [h=1]Shamsi Atetea Maslahi Ya Zanzibar Au Bara?[/h] Written by Mrfroasty (Ufundi) // 06/08/2011


  [​IMG]
  Mbunge ataka paspoti kuingia Zanzibar
  JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti Maalum
  na Salehe Mohamed na Danson Kaijage, Dodoma
  MBUNGE wa viti maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (CUF), ameitaka serikali kurejesha utaratibu wa watu kutoka Tanzania Bara kuingia visiwani Zanzibar kwa paspoti ili kupunguza wimbi la ujambazi na mauaji linazidi kuongezea siku hadi siku.
  Katika swali lake la nyongeza, Abama alitaka kujua kama serikali itakuwa tayari kurejesha mfumo wa zamani wa kuingia katika visiwa hivyo kwa kutumia paspoti ili kudhibiti vitendo vya ujambazi vinavyoongezeka.
  Akijibu swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha, alisema kwa hali ilivyo hivi sasa hakuna sababu kwa Watanzania kuingia visiwani Zanzibar kwa kutumia pasipoti kwa kuwa visiwa hivyo ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano.
  Nahodha alisema si kweli kuwa matukio ya ujambazi yamekuwa yakiongezeka Zanzibar kama alivyodai Abama bali hali ya ujambazi visiwani humo imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka.
  Alisema Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka wazi kuwa kila Mtanzania ana haki ya kutembea eneo lolote lile ndani ya jamuhuri bila kukwazwa hivyo kurejesha utamaduni wa pasipoti ni kumkwaza
  "Kwa hali ilivyo hivi sasa Zanzibar sioni sababu ya kuanzisha utaratibu wa pasipoti,kama tunataka kudhibiti matukio ya uhalifu ni vema tukaendelea na utaratibu wa ulinzi shirikishi," alisema Waziri Nahodha.
  Katika swali lake la msingi, Abama alitaka kujua serikali inatoa kauli gani juu ya vitendo vya ujambazi na mauaji ili kuhakikisha havitokei tena kwenye visiwa na Waziri Nahodha alimjibu akisisitiza kuwa si kweli kuwa matukio hayo yanaongezeka na kuwa yaliyopo ni ya kawaida ikilinganishwa na miji mingine ya Tanzania.
  Alisema takwimu zilizopo zinaonyesha matukio ya mauaji na ujambazi Zanzibar yamekuwa yakipungua mwaka hadi mwaka.
  Waziri Nahodha alitoa mfano kuwa mwaka 2008 matukio ya mauaji yalikuwa 15 na ya ujambazi yalikuwa 15, mwaka 2009 matukio ya mauaji yalikuwa 22 ya ujambazi yalikuwa 6, mwama 2010 matukio ya mauaji yalikuwa 15 na ya ujambazi lilikuwa tukio moja na mwaka 2011 matukio ya mauaji yalikuwa matano wakati tukio la ujambazi lilikuwa moja
   
Loading...