Shamshi vua nahodha ni mkomavu na mpevu wa siasa za ndani na anajitambua

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,358
349
akiwa mchangiaji wa mwisho mheshimiwa ameigusa nchi kwa hoja kunjufu na zenye mashiko.....

Amelitaka bunge, serikali muungano, Mapinduzi na watanzania kufikiri beyond maeneo, umimi na zaidi waiangalie katiba kwa manufaa ya nchi leo na vizazi vijavyo....

Amehoji juu ya msuguano wa nani mkazi na siyomkazi wa znz, haki ya upiga kura, hofu na kutokuaminiana miongoni mwa wabara na visiwani...
Amekemea hulka ovu ya kuchagua kukosoa kile kitakachokunufaisha na kunyamazia kile kinachowakwaza wengine....kama kweli dhamira ni kuondoa dosari na kuleta imani basi si haki kuchagua yale ya kuwapendeza wa Znz ilhali kuna sheria ambazo Wazanzibara wengi wanateswa nazo na zimefumbiwa macho na Wanzanzibar!!!
Amehitimisha kwa kuomba uwepo mjadala kati ya wabunge wa visiwani na wawakilishi na kwamba yeye amejipanga kuwasilisha hoja ya proportionality voting ili kuua uhasimu wa kimajimbo pale zanzibar...amebainisha kuwa ni kati 500km-1km unapata jimbo la uchaguzi kule zanzibar lakini maelewano kila kukicha yanakosekana hivyo ameshauri kura ipigwe kwa rais...kura za uraisi zitatoa uwiano wa wawakilishi kwa mujibu wa matokeo hayo....


Amenionyesha upevu,ukomavu,uzalendo,utaifa na uongozi ulioshamiri dhamiri njema.....

Hongera sana mh. Waziri shamsi vuai nahodha.
 
Ninakubaliana naye pia kuwa ni vema JMT Constitution ilibebe hili...hii itapunguza pia rushwa lakini zaidi itazalisha Rais wa wananchi kwa sababu wagombea Ubunge wataamuliwa na Presidential votes
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom