Shamimu Mwasha na mumewe wakutwa na kesi ya kujibu katika tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Kuanza kujitetea Septemba 3

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mafisadi imesema kwamba mfanyabiashara Abdu Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41), wana kesi ya kujibu.

shamim.jpg

Kadhalika, mahakama hiyo imesema wanafamilia hao wataanza kujitetea kesho (Septemba 3).

Uamuzi huo umetolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza mashahidi wanane na vielelezo sita vya Jamhuri. Hata hivyo, washtakiwa waliieleza mahakama kwamba wanatarajia kuita shahidi mmoja pamoja na wenyewe, utetezi utakuwa na mashahidi watatu.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Veronica Matikila na Wakili wa Serikali Constantine Kakula.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei Mosi, mwaka huu, wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

IPPMedia
 
Majuto, maumivu, woga, mashaka na huzuni hivi vyote ndio vimetawala moyo wake kipindi hiki, Mungu atatenda haki sawaswa na matendo yao.
 
Dawa za kulevya zinaingia humohumo kwenye uhujumu uchumi,kwa akili ya kawaida tu ninavyoelewa...
Kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa zinaweza ingia popote kirahisi mno kuliko mtu anavyotaraji...na ndo maana zimekua nyingi sikuhizi maana ukikwiba pesa na unafanya shughuli basi utakua unatakatisha pesa ulizoiba kupitia hiyo shughuli au ukifanya tendon lolote linalozuia serikali kutopata mapato yake kwa namna yeyote ile either wizi,rushwa,Tax evasion nk...basi hapo unahujumu uchumi pia...yaani ni shida umakini unahitajika sana
 
Mange alipomuita Mrs Sembe tulidhani ni wivu wa maisha, sasa mambo yapo hadharani barazani.
Shamim Mwasha alikuwa one of the active blogger. Kama aliingia kwenye sembe muda mrefu atakuwa ameharibu wengi huyu.

Nakumbuka alianzia Dar Hotwire kisha akaanzisha bloggs zake. Ukimuangalia huwezi kufikiria kama atakuwa mharibifu kiwango hiki.

Anyways hizi ni tuhuma ngoja tufuatilie labda anaweza kujitetea vizuri
 
Mbona mimi nilikuaga simjui huyu mwanamke? Mnasema alikua mke wa Mengi wa IPP??
 
Shamim Mwasha alikuwa one of the active blogger. Kama aliingia kwenye sembe muda mrefu atakuwa ameharibu wengi huyu.

Nakumbuka alianzia Dar Hotwire kisha akaanzisha bloggs zake. Ukimuangalia huwezi kufikiria kama atakuwa mharibifu kiwango hiki.

Anyways hizi ni tuhuma ngoja tufuatilie labda anaweza kujitetea vizuri
Tuhuma? Jana hukumu imetoka na wamehukumiwa na mumewe.
 
Back
Top Bottom