Kinachoendelea Loliondo: Shame on them! - Mwinyi, Mkapa, and Kikwete!

Wakuu zangu,

Jamani mbona naona watu mkifukuza mwizi wa nguo zenu mkiwa uchi?.. yaani hata sielewi kabisa Wadanganyika tumerogwa na nani?.. ndio maana niliuliza kwa nini sisi masikini mkashindwa kujibu! Wajanja wote waliingia mitini.. Kwa sababu hata sisi wenyewe hajujui..ndio haya....

Kwanza kabisa swala la Loliondo ni zito sana kama lingezungumzwa kwa staha lakini nimesoma mada nyingi humu na hoja zake zimejengwa kwa UDINI zaidi wala sio swala la rangi au kutetea maslahi ya Taifa..Hii ni akili mbovu kabisa na pengine naweza sema kuwa moja ya Umaskini wetu kwa sababu tumepokea dini hizi na tukawa watumwa wa imani hizi badala ya kuelewa mwongozo wa dini hizi na tukaacha mila na tamaduni zetu.

Wakuu zangu ikiwa swala ni ardhi, ardhi yetu INAUZWA.... hili ndilo somo kubwa na kwa mapana yake. Ni upumbavu mkubwa kukubali uwekezaji kutoka Ulaya lakini siii kutoa Arabuni kwa sababu ya mtazamo wa kidini au maendeleo ya watu na nchi hizo. Kuuza nchi yetu kwa wageni hakuna ongezeko la Elimu wala Utaalam, tutauza kwa fedha, na uroho wa fedha.. hivyo haijalishi kama ni mwarabu au mzungu anayekuja wekeza. Tatizo libakie tunakereka na KUUZWA kwa ardhi yetu.

Binafsi sikufurahia kuuzwa kwa mbuga zetu na nimewahi kulizungumzia hili toka zamani. Athari zake niliziandika wazi nje kabisa ya kumtazam mnunuzi kaa ni mtoto wa mfalme au ana undungu na Rostam.. Hata kama angeuziwa mzungu bado ningepinga kuuzwa kwa mbuga hiyo.

Tatizo kubwa la uuzaji wa mbuga zetu ni kwamba sasa hivi Ulaya na nchi zote zilizoendelea wanafungua Zoo za wanyama wetu kiasi kwamba zinapunguza pato la nchi yetu ktk Utalii. Na kibaya zaidi hawa wawekeshaji wamekuwa Walanguzi middlemen ktk biashara mabyo sisi wenyewe tungeweza kuifanya na kwa pato kubwa zaidi kwani hawa wawekeshaji ndio wao supplier wakubwa wa wanyama wetu ktk hizo Zoo. Ni ujinga mkubwa kuuza mbuga yetu kwa thamani ambayo mauzo ya Tembo wawili tu wanaweza kulipia kodi ya mwaka. na kutokana na NDOVYO TULIVYO tumeshindwa kuuza sisi wenyewe wanyama wetu tunawapa walanguzi.

Ndivyo tunavyofanya kwa mazao yetu iwe karafuu, kahawa, Pamba korosho na kadhalika.. Tunauza malighafi zetu kwa bei mchekea wakati mali hiyo hiyo ingewezekana kabisa kusafirishwa kwa consumer ikiwa finished product at the right price...
ndugu zangu, Wadanganyika wenzangu mweee acheni hizi habari za JK Muislaam na sijui Mkapa Mkristu haziwezi kutujenga hata kidogo..kumbuka tu kila unapoandika kuzungumzia dini nyingine unaipoteza hekima na pengine uumini wako. Unakuwa mtunzi wa Biblia au Kuran kwani maneno yote mnayozungumza hapa hayakuandikwa ndani ya vitabu hivyo..
 
Baada ya kuligusa suala la Meremeta nilidokeza kuwa ripoti tunayoifanyia kazi sasa ni ile ya kuelezea historia ya ufisadi wa makuwadi wa wizi wa kimataifa ulioanzia Loliondo na kugusa Ikulu yetu (chini ya Mwinyi) hadi suala Meremeta ambalo nalo liligusa utawala wa Mkapa, na suala la Dowans linalogusa utawala wa Rais Kikwete.

Lakini kabla hatujafika huko kote hatuna budi kusikitishwa na taifa letu kurudi nyuma tena karibu miaka 17 sasa kwenye kashfa ya Loliondo. Kama nilivyodokeza kwenye suala la Loliondo::connections watu wale wale waliokuja kama wawekezeji wamerudi tena na watarudi tena na kutufanya sisi tuwe watumwa katika nchi yetu.

Kampuni ya OBC ya UAE mdau wake mkubwa ni Brigadier wa jeshi la UAE na mtu wa karibu wa familia ya mtawala wa huko. Kwenye Dowans kampuni hewa ya Dowans (ambayo JK hakufuatilia kama vile hakufuatilia Richmond) nayo inamilikiwa na Generali wa jeshi hilo hilo la UAE na ambaye naye ana ukaribu na watu wa familia hiyo.

Kama vile tulio na wazimu katika vichwa vyetu tukawa tayari kupiga magoti mbele ya watu hawa hawa na kuwanyanyasa watu wetu ili tuwafurahishe makuwadi wa ufisadi wa kimataifa. Wamasai wa Loliondo leo hii wanaitwa wakimbizi katika nchi yao na malalamiko yao hayapewi kipaumbele wala kutiliwa maanani!

Na ni watu hawa hawa wa familia ile ile waliojaribu kuchukua eneo la Yaeda Chini na kusababisha njaa kwa watu wetu na watawala wetu wakawatetea; watu wa familia ile ile ya kina Zayed. Angalau kwenye kesi ya Bonde la Yaeda Chini tuliweza kupiga kelele na kuwatimua lakini Loliondo na Dowans hawako tayari kutuachilia.

Hawa watu wanatuahidi vitu gani hadi tuwe wanyonge na dhaifu mbele zao utadhani mbwa mbele ya chatu? Hawa majenerali wenye nyotanyota wanawaahidi nini watawala wetu na wanalainika mbele zao kama waliolishwa limbwata za kitanga?

Hadi inafika mahali waliochaguliwa na wananchi wanawatetea makuwadi wa ufisadi wa kimataifa ambao rekodi yao iko wazi ya jinsi gani wametumia vibali tulivyowapa vibaya, jinsi gani wameua wanyama wetu kiholela na kutorosha wanyama hai kwenda makwao kwa fahari ya watawala wa huko.

Kama vile watawala hawa hawa walivyoruhusu madini yetu kule Buhemba kuchotwa na mamluki wa kivita wa Afrika ya Kusini na kuendelea kutuimbia wimbo wa umaskini wetu huku tukijichekelesha mbele yao.

Nani alitulaani? Tuache kupiga kelele ili wauze hadi nepi za watoto wetu, na vitanda vya vikongwe vyetu vipigwe mnada? Tuache kuandika na kuhoji yanayotokea nchini mwetu kwa vile wao ni watawala? Tuache kuliamsha taifa kutoka katika usingizi wake kwa sababu tukifanya hivyo tunawaudhi wanaotembea na ving'ora na kutetemewa wakitembea?

Mnatupa uchaguzi rahisi; mnatupa uchaguzi ambao hatuwezi kuacha kuuchukua; ni uchaguzi usiohitaji shahada za Harvard wala utaalamu wa fizikia ya anga za mbali. Hatuwezi kufumba macho yetu na vinywa vyetu ili mtutawale mpendavyo.

Jifunze kuhusu original Loliondo Scandal ambayo inahisiwa kuhusishwa na kifo cha mwandishi mahiri wa uchunguzi Stan Katabalo hapa Bonyeza Hapa

Napenda kujua msimamo wa wabunge wafuatao kuhusu Loliondo:

Dr. Harrison Mwakyembe
Lucas Selelii
mama Anna Kilango
Mzee Yusuph Makamba
John Chiligati
Samwel Sitta (Spika)

NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.

Mkulu hapa umeniacha

sasa R.Oanahusika vipi na hiyo DB ndio nani David Banda?(jocking)

hebu tuweke wazi

halafu mbona siku hizi hakuna miziki au ndio ma prodyuza washachoka kukaa studio?
 
Mbona inajulikana kwa wote kuwa alisomeshwa na JKN? Na si yeye tu.

- Mkuu Sikonge, ahsante sana mkuu kumbe unalifahamu hili, unajua ni wananchi wachache sana wanaolijua hili,

- Mimi ninamfahamu jamaa wa uwt aliyekuwa akiwapelekea hela za poketi money shuleni kila mwisho wa mwezi toka Ikulu, ambaye Muungwana alimtumia sana kwenye kampeni za urais kupata info nyeti za kambi zingine,

- Huyu aliweza kujipenyeza na kuingia kambi yoyote ile, bila kufahamika kuwa ni mtu wa Muungwana, mpaka uchaguzi ulipokwisha ndipo akajulikana kuwa ndiye aliyewaponza kambi karibu zote, vinavyoelea siku zote huwa vimeundwa!

Respect.

FMEs!
 
FM and DSM:

Hile ni investment na wateja wake wanatoka au kutegemea kutoka pande zote za dunia na sio Arabuni pekee yake.

Trophy Hunting ni mchezo uliokomaa sana Marekani na nchi nyingi za Ulaya. Hivyo wawindaji kwa sehemu kubwa watakuwa wazungu.

Wawindaji huwa wanaongozwa na walinzi ambao mara nyingi ni ndugu zetu wa damu. Na kwa maneno ya mwindaji mmoja kutoka Denmark anasema kuwa ukitoa kitu kidogo, waongozaji watakuruhusu kuua wanyama zaidi ya wale uliopewa.

Je katika matatizo haya wa kulaumiwa ni nani?

Wakulaumiwa ni sisi wenyewe. Tutatoa lawama kwa huyu Brigadia, lakini huyu ni investor. Na mamilioni yake hakuyapata kutoka mbinguni. Aliyafanyika kazi sehemu nyingine kabla ya kuja Tanzania.

Wote wanastahili lawama. Hao wazungu wanaopenyeza rupia ili waue wanyama zaidi ya quota yao na hao waarabu wanaowinda bila kujali sheria za uwindaji. Kuvaa kofia ya uwekezaji kusiwape immunity. Pamoja na kuwalaamu ndugu zetu wanaowanywesha sumu vifaru ili wawanyofoe pembe zao lakini lazima tuwalaumu vile vile waarabu wa Yemen wanaoona fahari kuweka visu ndani ya pembe hizo na wachina wanaodhani pembe hizo zinaongezea nguvu za kiume. Wote walaumiwe, bila kujali rangi, dini, kabila au jinsia.

Amandla.......
 
Hayo ni mawazo yako binafsi na uzushi na kuwa mbabaishaji wa maneno wa hali ya juu. Mbona kuna mbuga nyingi sana zimechukuliwa na watu aina mbali mbali hususan wazungu, tena zina ukubwa maradufu zaidi ya hizo za Loliondo lakini huzisemi? Kwa nini ukweli unaoutaka kuulazimisha uwe wa upande mmoja tu? hizi ndio ''agenda za siri'' tunazozisema kila siku.

Kama unajua zipo mbuga zilichochukuliwa na watu mbalimbali "hasa wazungu" kwanini wewe usiziseme? Kwanini mimi ndio nimekuwa msemaji wa kila mbuga ilichochuliwa au unataka niziseme halafu uulize mbona kuna migodi nayo sisemi?

Hilo la Dowans linahusu nini? au Dowans wamefanya kosa lipi?

Ni walaghai, wameingia nchini under false pretense, na Dowans ndio hao hao wa Loliondo!

ngoja usikie mifedha watakayolipwa ndio mtajuwa kuwa fitina za kijinga siku zote hazisaidii bali zina hasara kubwa kama yale ya wale wa Malaysia, nna uhakika unawajuwa na mpaka leo tunawalipa kutokea puwani. Kwa hayo hayo mafitina ya mijitu kama wewe, mkenda kututia hasara Taifa zima.

shindwa! Wenye kulitia hasara taifa wamekaa kwenye viti vya enzi kama watawala wa ufalme wa ufisadi!

Loliondo, nini hasa walichokiiba? nini hasa walichochukuwa nje ya Sheria? nini hasa walichochukuwa wakapeleka nje ya Tanzania? zaidi ya wawekezaji wengine wa kwenye mbuga zingine?

wakati mwingine jaribu kufanya utafiti wewe mwenyewe usisubiri kupikita, kuwekewa mezani, na kulishwa; mwisho utataka umezeshwe pia.

Tena ukitazama kwa makini hawa wa Loliondo wamesaidia na kutowa misaada kuliko mwekezaji mwengine yeyote aliewekeza kwenye Mbuga za wanyama.

Endelea peke yako kuabudu katika madhabahu ya misaada!

Wacha hizo za kuleta, kwa sababu tu wawekezaji wa Loliondo ni... na Dowans ni... Utajaza mwenyewe!

wale wale!
 
naona umechanganya mambo kidogo, loliondo inamilikiwa na ndugu ya mfalme wa UAE, dowans inamilikiwa na Rostam pamoja na mjeshi wa Oman.
 
Na hao warabu walivamia au waliuziwa? nenda loliondo wewe ukaone mambo walioyofanya hao jamaa sio kuchonga tu. Hata ikulu watainunua kwa tamaa za watanzania. Kikwete mwenye hata hizo hela za kampeni unadhani kapata wapi? Jaribu kufatilia urafiki kati ya kikwete na Salim Ajeeb wa Oman ndio utajua ukweli.
 
ndio shame on them,

and shame on us who keep on carrying the stinky thing around for years..

POLITICIANS & DIAPERS BOTH NEED TO BE CHANGED, AND FOR THE SAME REASON
 
Wakuu zangu,
Jamani mbona naona watu mkifukuza mwizi wa nguo zenu mkiwa uchi?.. yaani hata sielewi kabisa Wadanganyika tumerogwa na nani?.. ndio maana niliuliza kwa nini sisi masikini mkashindwa kujibu! Wajanja wote waliingia mitini.. Kwa sababu hata sisi wenyewe hajujui..ndio haya.........

Ndo maana CCM wanaendelea kushinda na kuumiza wananchi nchini, kila kitu lazima kitiwe udini udini!, Ati badala ya kuulizana kwa nini ardhi ya wananchi iuzwe, watu wanataka kutoana macho, kila mmoja anamtetea mnunuzi anayehisi ni muumini ya dini aifuatayo yeye! Yaani watu hawajali nchi ikiuzwa ali mradi tu mnunuzi ni mtu wa dini yake. Nshawahi kusema kuwa mafisadi dini yao ni tofauti kabisa na dini nyingine, kwani wao wanaabudu pesa, na kabila lao ni pesa, wanapigia magoti pesa, na wanafutana kwa kuwa wote wanaungana kwenye hiyo nyumba yao ya ibada-Ufisadini!- Nyie wengine kaeni hapa mtoane macho wenzenu wanaendelea kuzizoa hizo pesa na kila leo wanabuni mbinu mpya.
 
Wakuu zangu,
Jamani mbona naona watu mkifukuza mwizi wa nguo zenu mkiwa uchi?.. yaani hata sielewi kabisa Wadanganyika tumerogwa na nani?.. ndio maana niliuliza kwa nini sisi masikini mkashindwa kujibu! Wajanja wote waliingia mitini.. Kwa sababu hata sisi wenyewe hajujui..ndio haya....

Wengine hatukujibu sana kwa sababu swali lenyewe lilikuwa limekosewa. Ukiuliza swali lililokosewa utapata majibu yaliyokosewa.

Kwanza kabisa swala la Loliondo ni zito sana kama lingezungumzwa kwa staha lakini nimesoma mada nyingi humu na hoja zake zimejengwa kwa UDINI zaidi wala sio swala la rangi au kutetea maslahi ya Taifa..

Sijui udini umeingiaje tena humu.

Hii ni akili mbovu kabisa na pengine naweza sema kuwa moja ya Umaskini wetu kwa sababu tumepokea dini hizi na tukawa watumwa wa imani hizi badala ya kuelewa mwongozo wa dini hizi na tukaacha mila na tamaduni zetu..

sijui udini umeingizwaje humu tena.

Wakuu zangu ikiwa swala ni ardhi, ardhi yetu INAUZWA.... hili ndilo somo kubwa na kwa mapana yake. Ni upumbavu mkubwa kukubali uwekezaji kutoka Ulaya lakini siii kutoa Arabuni kwa sababu ya mtazamo wa kidini au maendeleo ya watu na nchi hizo.

tatizo siyo ardhi tu, tatizo ni mchakato mzima wa uwekezaji na Loliondo ni mfano mzuri kwani ni ufisadi ulitangulia ufisadi mwingine mkubwa; Ndilo lilikuwa jaribio kubwa la kwanza la kuuza urithi wa watoto wetu kwa wageni. Sasa kama hao wageni wangekuwa ni wasomali, wamarekani, wachina au watu wengine ukweli kuwa ni kashfa unabakia pale pale.

Kuuza nchi yetu kwa wageni hakuna ongezeko la Elimu wala Utaalam, tutauza kwa fedha, na uroho wa fedha.. hivyo haijalishi kama ni mwarabu au mzungu anayekuja wekeza. Tatizo libakie tunakereka na KUUZWA kwa ardhi yetu.

Huo ndio ukweli; ndio maana tunapopigia kelele hatubakii kwenye Loliondo tu, tunaenda hadi Buhemba, Buzwagi, n.k Hivi vitu vitukere bila kuangalia aliyehusika ana toka wapi au ana dini gani.

Binafsi sikufurahia kuuzwa kwa mbuga zetu na nimewahi kulizungumzia hili toka zamani. Athari zake niliziandika wazi nje kabisa ya kumtazam mnunuzi kaa ni mtoto wa mfalme au ana undungu na Rostam..

Tatizo siyo sisi ni watawala ndio wanafanya hivyo; Ni wao wanaoangalia mwekezaji anatoka wapi na ni mtoto wa wanani na anahusiana na nani hapa Tanzania.

Hata kama angeuziwa mzungu bado ningepinga kuuzwa kwa mbuga hiyo.
tatizo kubwa la uuzaji wa mbuga zetu ni kwamba sasa hivi Ulaya na nchi zote zilizoendelea wanafungua Zoo za wanyama wetu kiasi kwamba zinapunguza pato la nchi yetu ktk Utalii. Na kibaya zaidi hawa wawekeshaji wamekuwa Walanguzi middlemen ktk biashara mabyo sisi wenyewe tungeweza kuifanya na kwa pato kubwa zaidi kwani hawa wawekeshaji ndio wao supplier wakubwa wa wanyama wetu ktk hizo Zoo. Ni ujinga mkubwa kuuza mbuga yetu kwa thamani ambayo mauzo ya Tembo wawili tu wanaweza kulipia kodi ya mwaka. na kutokana na NDOVYO TULIVYO tumeshindwa kuuza sisi wenyewe wanyama wetu tunawapa walanguzi.

true!

Ndivyo tunavyofanya kwa mazao yetu iwe karafuu, kahawa, Pamba korosho na kadhalika.. Tunauza malighafi zetu kwa bei mchekea wakati mali hiyo hiyo ingewezekana kabisa kusafirishwa kwa consumer ikiwa finished product at the right price...

kweli kabisa!

ndugu zangu, Wadanganyika wenzangu mweee acheni hizi habari za JK Muislaam na sijui Mkapa Mkristu haziwezi kutujenga hata kidogo..

It buffles my mind!

kumbuka tu kila unapoandika kuzungumzia dini nyingine unaipoteza hekima na pengine uumini wako. Unakuwa mtunzi wa Biblia au Kuran kwani maneno yote mnayozungumza hapa hayakuandikwa ndani ya vitabu hivyo..

hili la dini linanishinda upeo wangu kwenye mada hii. Kuwaendekeza wanaoleta udini kwenye mada hii ni kuwapa heshima isiyostahili.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nakuomba rudia kusoma hoja zilizopita, sijui kaa umeifuatilia sana mada hii..Swala la Loliondo limetumika zaidi kwa sababu wanunuzi ni Waarabu kama vile watu wanatazama nani toka nje anayefaa kupewa ardhi hiyo. Ni kweli kabisa ardhi yetu haikanza kuuzwa jana wala Liliondo inauzwa kila siku na hakuna mtu anayetazama upande wa pili au kukashifu policy nzima inayoruhusu..Sidhani kama tunatakiwa kumlaumu Mwinyi, Mkapa au JK ikiwa bunge letu linajua vizuri kwamba ardhi yetu inakodishiwa (kuuzwa) wawekezaji toka nje kwa masharti mbuzi kabisa..

Binafsi nilikuelewa toka mwanzo pamoja na kwamba wewe pia huzungumzi kitu unless kina harufu fulani nje ya picha kamili..Tuyaache hayo.
Sasa ukirudi ktk swala la ardhi huu ni urithi wetu naoste tunakubaliana kwamba hakuna mtu wala mkoloni anayetakiwa kupewa nguvu na ushujaa wa wapiganaji wetu waliodai Uhuru. Ukweli ni kwamba tunapokodisha ardhi inaondoa kabisa maana ya Uhuru na inafikia mtu kujiuliza kwa nini tulipigania Uhuru kwani ardhi ndio ilikuwa sababu ya kwanza..Tungeweza kabisa ku lease ardhi ile kwa wakoloni toka wakati ule bila kudai Uhuru na kama alivyozungumza Mugabe leo hii ktk mahojiano na Christian Amanpour kwamba ni mali ya wananchi..Lakini leo hii inaonyesha wazi kwamba Uhuru wetu ni kuwa na sura ya Mmatumbi Ikulu.

Mkuu wangu JF ya leo sii ile ya jana wlaa mwaka jana, Udini umeingia sana kiasi kwamba kila mtu huyu anapimwa kwa dini yake..wapo hata washikaji wangu wa karibu wamechukua majina ya bandia ili mradi tu inapofikia maswala ya dini huyatumia majina hayo bila kujua kwamba uandishi wao unawaacha Uhchi wa nyama..Kwa hiyo unapohoji Udini umeiongia vipi pasipo kusoma maelezo ya baadhi wanazi wasiojua wala kufuata ibada za dini zao inashangaza sana hasa kwa mtu kama wewe..In fact mimi nimefikia Ukingo wa kuendelea mna mapambano hapa JF.. naona ni kupoteza muda na wakati wangu muhimu sana kwani maendeleo ya Mtanzania yamekuwa kama tunaitafuta pepo..Kila mmoja wetu atakufa yeye atazikwa yeye na atahukumiwa yeye kwa yale alofanya!..
Kifupi nadhani imefikia mahala nijitazame mimi mwenyewe naweza vipi kuipata pepo (utajiri) kwa nadharia inayojieleza kuwa maendeleo ya nchi huanza na mtu mmoja mmoja!
 
Bob, inakuwaje tena?

yaani hawa wanaoleta upuuzi wao unawaruhusu njia Mkuu. hizi pepo mku tunazitafuta kila kukicha.....na wakti huo huo tukiendeleza mapambano kama kawa.....uzuri ukishajua udhaifu wa mtu fulani hiyo ni silaha kubwa katika kujenga hoja zako dhidi ya mtu huyo....don't give up....tumetoka mbali.....

Jeshini tunaingia pamoja lakini wengine hatuna vyeo walivyonavyo wengine.....kazi na iendelee
 
Ogah,
Hapana mkuu wangu ukiendeleza sana mapambano watakuja sema unaamini - Ukija Kufa ktk mapambano unapewa ufunguo wa mbinguni (a key to Heaven)!..
Unajua hakuna kitu kibaya dunaini kama mnapojaribu kushindana na mwenye nguvu ikiwa hamna UMOJA baina yenu. Hivi leo Wadanganyika tumepoteza maana ya ADUI zetu kuwa ni Afya, Ujinga na Umaskini. badala yake demokrasia imetuletea UJINGA mwingine kiasi kwamba inasherehesha nadharia ya nchi za magharibi.
Unajua kulingana na report ya CIA inajieleza wazi kabisa kwamba njia pekee ya kuzi control nchi maskini ni kuvunja UMOJA wao..na ajabu wanafanikiwa sana wakati sisi sote tunaelewa fika kuwa UMOJA ndio NGUVU yetu..
Sasa ikiwa tunashindwa kujipanga tukaunda UMOJA chini ya misingi ya Utanzania badala yake tunaweka tofauti zetu ambazo ndizo hasa somo kubwa la CIA ktk kusambaratisha tunafika kweli..Leo hii swala la Loliondo limechukua sura ya Uarabu na Uzungu, kesho utasikia Uislaam na Ukristu mara Uchagga na kadhalika basi ili mradi tunakwepa hali halisi..Kila Ufisadi hutafrisika kama vile ugonjwa wa HIV lazima iwe ni swala la Umalaya na kuulaaniwa wakati mojority wanaendelea kutotumia condom kama kinga.
Hivyo inafikia mahala najiuliza what a f....... nitaitafuta pepo ki vyangu vyangu!
 
Nyerere may have been almost immune to personal corruption, but he created one of the most indelibly corrupt societies in the 'third world'. A few days after Nyerere's burial, an international report confirmed that Tanzania was still one of the world's 25 poorest nations and the seventh most corrupt.

Shame!
 
Haya mwingine huyooo, Nyerere ametokea wapi ktk mada hii! yaani tafran tupu...
 
Nyerere may have been almost immune to personal corruption, but he created one of the most indelibly corrupt societies in the 'third world'. A few days after Nyerere's burial, an international report confirmed that Tanzania was still one of the world's 25 poorest nations and the seventh most corrupt.

Shame!
The world is still full of sin although Jesus came to save us from our sins; the blame should be on Jesus, no? Some kind of logic indeed.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nakuomba rudia kusoma hoja zilizopita, sijui kaa umeifuatilia sana mada hii..Swala la Loliondo limetumika zaidi kwa sababu wanunuzi ni Waarabu kama vile watu wanatazama nani toka nje anayefaa kupewa ardhi hiyo. Ni kweli kabisa ardhi yetu haikanza kuuzwa jana wala Liliondo inauzwa kila siku na hakuna mtu anayetazama upande wa pili au kukashifu policy nzima inayoruhusu..Sidhani kama tunatakiwa kumlaumu Mwinyi, Mkapa au JK ikiwa bunge letu linajua vizuri kwamba ardhi yetu inakodishiwa (kuuzwa) wawekezaji toka nje kwa masharti mbuzi kabisa..

tunawalaumu hao marais kwa sababu hao wawekezaji uchwara walipokuja mara ya kwanza - Loliondo 1 hawakwenda Bungeni bali Ikulu; waliporudi tena kwenye Loliondo - 2 hawakwenda Bungeni bali Ikulu, na mwaka huu alipokuja tena mwana wa Zayed hakwenda Bungeni bali Ikulu! Ikulu ndio mlango wao rahisi kabisa na ndio wamekuwa wakiutumia. Kama Ikulu wakitaka kubadilisha sera wanaweza!

Binafsi nilikuelewa toka mwanzo pamoja na kwamba wewe pia huzungumzi kitu unless kina harufu fulani nje ya picha kamili..Tuyaache hayo.

Tutaweza vipi kuyaacha kirahisi hivyo wakati umetoa madai mazito ambayo hata kuthibitisha nina uhakika huwezi. Kwamba sizungumzii "kitu" unless kina harufu fulani "nje ya picha kamili" ni madai yasiyo na msingi, hayana ukweli, na hata ukitumia karne kutafuta ushahidi huwezi kupata. Nazungumzia vitu kwa jinsi vilivyo bila ya kuangalia kitu kingine zaidi ya kile kilichopo. Wenye kazi ni wale wenye kutafsiri.

Sasa ukirudi ktk swala la ardhi huu ni urithi wetu naoste tunakubaliana kwamba hakuna mtu wala mkoloni anayetakiwa kupewa nguvu na ushujaa wa wapiganaji wetu waliodai Uhuru. Ukweli ni kwamba tunapokodisha ardhi inaondoa kabisa maana ya Uhuru na inafikia mtu kujiuliza kwa nini tulipigania Uhuru kwani ardhi ndio ilikuwa sababu ya kwanza..
T

Kwetu sisi hatukupigania uhuru na ardhi kuwa ya kwanza tu bali tuliongozwa na ulazima wa kutambua na kudai heshima na utu wetu kama binadamu. Ukoloni unaondoa kwanza uhuru, utu, na ubinadamu wetu. Na hilo hutekelezwa kwa kutunyang'anya ardhi. Hivyo, kuna ukweli hapo.

unge
weza kabisa ku lease ardhi ile kwa wakoloni toka wakati ule bila kudai Uhuru na kama alivyozungumza Mugabe leo hii ktk mahojiano na Christian Amanpour kwamba ni mali ya wananchi..Lakini leo hii inaonyesha wazi kwamba Uhuru wetu ni kuwa na sura ya Mmatumbi Ikulu.

Na hilo ni tatizo la kweli. Tukiwakataa watu weusi kwa vitendo vyao vya kikoloni tunaambiwa tunawadharau, lakini wanapokuja wazungu na wageni wengine kufanya vitendo hivyo hivyo tunatakiwa kuwashukuru!

Mkuu wangu JF ya leo sii ile ya jana wlaa mwaka jana, Udini umeingia sana kiasi kwamba kila mtu huyu anapimwa kwa dini yake..wapo hata washikaji wangu wa karibu wamechukua majina ya bandia ili mradi tu inapofikia maswala ya dini huyatumia majina hayo bila kujua kwamba uandishi wao unawaacha Uhchi wa nyama..Kwa hiyo unapohoji Udini umeiongia vipi pasipo kusoma maelezo ya baadhi wanazi wasiojua wala kufuata ibada za dini zao inashangaza sana hasa kwa mtu kama wewe..In fact mimi nimefikia Ukingo wa kuendelea mna mapambano hapa JF.. naona ni kupoteza muda na wakati wangu muhimu sana kwani maendeleo ya Mtanzania yamekuwa kama tunaitafuta pepo..Kila mmoja wetu atakufa yeye atazikwa yeye na atahukumiwa yeye kwa yale alofanya!..
Kifupi nadhani imefikia mahala nijitazame mimi mwenyewe naweza vipi kuipata pepo (utajiri) kwa nadharia inayojieleza kuwa maendeleo ya nchi huanza na mtu mmoja mmoja!

Ni kweli ndio maana naingia siku hizi kwa mapozi na kwa nukta na vituo.
 
...................Ni kweli ndio maana naingia siku hizi kwa mapozi na kwa nukta na vituo.

Hivi mnataka kuniambia kuwa hamjui kuwa uchaguzi......just around the corner?..........

Vijana itabidi tuwarudishe Trinidad & Tobago............
 
Mzee Mwanakijiji,

Mkuu wangu JF ya leo sii ile ya jana wlaa mwaka jana, Udini umeingia sana kiasi kwamba kila mtu huyu anapimwa kwa dini yake..wapo hata washikaji wangu wa karibu wamechukua majina ya bandia ili mradi tu inapofikia maswala ya dini huyatumia majina hayo bila kujua kwamba uandishi wao unawaacha Uhchi wa nyama..Kwa hiyo unapohoji Udini umeiongia vipi pasipo kusoma maelezo ya baadhi wanazi wasiojua wala kufuata ibada za dini zao inashangaza sana hasa kwa mtu kama wewe..In fact mimi nimefikia Ukingo wa kuendelea mna mapambano hapa JF.. naona ni kupoteza muda na wakati wangu muhimu sana kwani maendeleo ya Mtanzania yamekuwa kama tunaitafuta pepo..Kila mmoja wetu atakufa yeye atazikwa yeye na atahukumiwa yeye kwa yale alofanya!..
Kifupi nadhani imefikia mahala nijitazame mimi mwenyewe naweza vipi kuipata pepo (utajiri) kwa nadharia inayojieleza kuwa maendeleo ya nchi huanza na mtu mmoja mmoja!

Mkandara

usiache mapambano, endelea tu, hiki ni kijiwe muhimu sana. kupitia hoja na majadiliano ambayo wachangiaji (wewe ukiwa mmoja wapo) wanachangia. Kupitia kwenye kijiwe hiki watu kama mimi tuliokuwa mbumbumbu wa maswala ya siasa tumehabarishwa mengi tu yanayoendelea nchini kwetu, tumekuwa tukiona dots tu hapa na pale lakini hapa JF panatusaidia ku connect the dots na kupata picha halisi ya kinachoendelea siku hadi siku.

ni kupitia hizi hizi hoja za kidini zinazoshamiri hapa JF tumeelewa kiasi gani udini una ingilia siasa na maendeleo ya Tanzania,
 
Back
Top Bottom