SHAME; Mbunge wa Kilolo akimbia kuwekwa kitimoto na wananchi wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHAME; Mbunge wa Kilolo akimbia kuwekwa kitimoto na wananchi wake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 27, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mwakilishi wa mkurugenzi wa Kilolo John Kiteve akijibu maswali katika mdahalo huo ambao ulipaswa pia kuhudhuria na mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla
  Na Francis Godwin,Blog

  MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla amekwepa kushiriki mdahalo wa kimaendeleo katika Kati yake na wananchi wa jimbo hilo leo .

  Katika mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Upendo Ruaha mbuyuni mbunge Profesa Msolla ambaye pia amepata kuwa waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia mbali ya kupewa taarifa na waandaaji wa midahalo hiyo ambao ni azaki za kiraia Tanzania ,mbunge huyo alipaswa kufika katika ukumbi huo kuanzia majira ya saa tatu asubuhi ila hadi saa Saba mchana mbunge huyo wala katibu wake hawakuweza kutokea ukumbini na kupelekea mdahalo huo kuchelewa kuanza .

  Mratibu wa midahalo hiyo mkoa wa Iringa Raphael Mtitu alisema kuwa mbunge huyo alipewa taarifa kwa wakati juu ya uwepo wa midahalo hiyo japo alisema kuwa anasikitishwa na hatua ya mbunge kutofika na kuwa ni mbunge wa kwanza toka kuanza kwa midahalo hiyo kushindwa kufika huku akidai kuwa kutofika kwake bado hakujazuia mdahalo huo kuendelea .

  Mtitu alisema mbunge alipaswa kufika katika mdahalo huo Kwani ni mdahalo ambao unahusisha wapiga kura na mbunge na kutoa nafasi ya wananchi kuweza kutumia nafasi hiyo kujadili maendeleo ya jimbo hilo.

  Pia alisema baada ya mdahalo huo kufanyika katika jimbo hilo la Kilolo mdahalo utakaofuata utafanyika katika jimbo la Ismani kwa kumkutanisha mbunge wa Jimbo hilo Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mdahalo wa mwisho utafanyika katika jimbo la Kalenga kwa kumkutanisha mbunge Dkt Wiliam Mgimwa ambaye ni waziri wa fedha na uchumi na wapiga kura wake .

  Hata hivyo amewaomba wabunge hao kufika katika mdahalo hiyo Kwani ni midahalo yenye sura ya kimaendeleo zaidi na kuwa hatua ya wabunge kukwepa kufika katika midahalo hiyo ni kutowatendea haki wapiga kura wake.

  Wakati huo huo wananchi walioshiriki katika mdahalo huo walieleza kusikitishwa na hatua ya mbunge wao Prof.Msolla kushindwa kufika katika mdahalo huo na kudai kuwa kufanya hivyo ni saw a na usaliti Kwao na kudai kuwa mtendaji wa kata hiyo na mtendaji wa kijiji walionekana wakipita mitaani kuzuia wananchi kutofika huku wakitaka kuzuia midahalo hiyo usifanyike bila mafanikio .

  Katika moja Kati ya maswali yao wananchi wa Ruaha mbunyuni wameeleza kusitikiswa na baadhi ya waganga wa tiba za jadi ambao wamekuwa wakivamia nyumba za idaba na makazi ya watu wakidai wanatoa uchawi alisema mwinjilisti wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) usharika wa Ruaha Bahati Lyena


  SOSI; Fransis Godwin Blog.
   
Loading...