Shambulio SYL Hotel, Mogadishu: Baada ya Al Shabaab kuteka hotel kwa saa 7. Watu 10 wauawa wakiwemo Wapiganaji watano wa Al Shabaab na Raia wawili

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Wanamgambo wa Alshaabab nchini Somalia wamekiri kuhusika na shambulio linaloendela katika hoteli ya kifahari mjini Mogadishu SYL nchini Somalia. Taarifa zinasema kuwa makundi ya wanajeshi wanaonekana kwenye barabara inayoelekea katika kasri ya rais.

Taarifa za hivi punde ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa makumi kadhaa ya watu waliokuwemo ndani ya hoteli ya SYL wanaripotiwa kuokolewa, na washambuliaji wawili wameuawa na vikosi vya usalama vya Somalia, huku wengine watatu wakiwa bado wanaendesha mashambulio ndani ya hoteli.

Serikali ya Somalia bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulio hili.

Kituo cha redio cha Dalsalam mjini Mogadishu kimesema kenye ukurasa wake wa twitter kuwa wabunge wawili kwa jina Mahgan pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Somalia Abdulkadir Ali Omar wamejeruhiwa katika shambulio lilitokea katika hoteli ya SYL:

UPDATE
Majeshi ya Ulinzi na Usalama yamefanikiwa kulizima shambulio la Kigaidi ambalo Wanamgambo wa Al Shabaab wamekiri kuhusika nalo katika Hoteli ya Kifahari ya SYL iliyopo Mogadishu baada ya saa saba za mapigano

Msemaji wa Serikali, Ismail Mukhtar kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, Watu 10 wameuawa katika shambulio hilo ambapo Wanamgambo wa Al Shabaab watano waliovamia hoteli hiyo wameuawa na Watu wengine watano wakiwemo raia wa kawaida wawili

Aidha, Watu takriban 82 wameokolewa na wengine wengi wamejeruhiwa huku Polisi ikitahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na shambulio hilo katika hoteli hiyo iliyopo karibu na makazi ya Rais na inayotumiwa zaidi na Viongozi Waandamizi wa Serikali


****

Suspected Al Shabaab fighters storm Mogadishu's SYL hotel near the Presidential palace.

Fierce exchange of gunfire heard inside the hotel - Witnesses.

Heavy gun battle between Al Shabaab attackers & security forces ongoing inside SYL hotel in Mogadishu.

The hotel is a popular destination for Somalia ministers, MPs & military officials. Casualties unknown yet. SYL has been the subject of AS attacks many times before

Several Al Shabaab gunmen wearing Somali military uniform entered the SYL hotel and began shooting.

Senior govt officials were inside the hotel during the attack. Some of them escaped by jumping from the wall and others missing. No VBIED involved

Mogadishu's SYL hotel under siege. Al Shabaab gunmen have taken positions, firing grenades and bullets from the upper floors of the hotel. Security reinforcements deployed to the scene. Casualties reported from inside the hotel, number still not known.
 
Back
Top Bottom