Shambulio la ubalozi wa Marekani Tanzania na kijana wa Kizanzibar na niliyoyakuta Zanzibar

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,096
2,000
Inawezekana Watanzania tumeshasahau kama binadamu tulivyoumbwa lakini imenibidi baada tu ya hivi punde kusoma story inayoelezea kijana aliyesababisha kujulikana kwa Osama Bin Laden huko Abbotab Pakistan na mwisho kuuwawa.

Pili naomba msinielewe vibaya hasa ndugu zangu mlioko hapa Jamii forum hasa wale wa Zanzibar. Ugaidi haujalishi nchi, kabila wala dini kwani huko Marekani magaidi wanaofanya mauaji hata Wakiristu wezangu wanashiriki

Nilipofika kwa mara ya kwanza Zanzibar 2004 nilifikia Dunga Ubago (Makazi ya familia za wanajeshi) kwani ndipo mjomba alikuwa anaishi na familia yake.
Siku moja jioni tukienda kwenye konde lake (shamba) mjomba alinipa story ya kusisimua baada ya kufika jirani na nyumba fulani za makazi. Mjomba alinieleza kuwa katika moja ya magaidi walioshiriki kulipua ubalozi wa Marekani Dar Es Salaam mmoja wa walipuaji alitoka katika kaya hii na alikamatiwa nje ya nchi akitoroka na sasa yuko Guatanamo Bay nchini Cuba kama mfungwa ila kila mwaka familia huenda kumsalimia kwa gharama za serikali ya Marekani. Niliitazama Ile nyumba kwa mbali nikishuhudia migari kibao maarufu Kama chai maharage ambayo kipindi hicho ilikuwa maarufu kwa kusafirisha abiria.
Baada ya siku kadhaa rafiki yangu mwingine Mzanzibar alinipa story hiyohiyo na kuhitimisha kuhakiki hiyo habari kuwa ni kweli.

Nikiwa nimepata kazi ya Hotel Bwejuu nilianza kuishi Meli sita njia ya kuelekea Kizimbani baadae nikahamia Mtaa wa mwembe Mchomeke Meli sita hiyohiyo. Baada ya kuwa mwenyeji nilianza jukumu la kuwatafuta vijana kutoka kijijini kwetu bara waliolowea Zanzibar nikijaribu kuwaulizia viongozi wa umoja wa vijana wa Kisukuma waliokuwa maeneo ya Uroa na ilikuwa kazi ngumu kwani wengi walikuwa wameshabadiri majina kwa kusilimu na mmoja tu niliyebahatika kumfahamu baada ya kukutana nae akitoka kukata nyasi kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa. Alinipeleka kwa tajiri yake kunitambulisha na mimi nikampeleka ninapoishi na kutambulisha kwa girlfriend wangu niliyekuwa nafanya kazi nae za hotel.......
Kufahamiana na huyu ndugu kulinifanya niishi vizuri sana na kujisikia niko Kama nyumbani kwetu maana kila nikitoka kazini nilikuta ameniletea maziwa, matunda n.k.

Siku ambayo sitaisahau ni siku nilipomkuta amenisubiri kwa muda mrefu kwangu na baada ya kusalimiana na kuongea ndipo akafunguka jambo ambalo hadi leo nikisoma tu habari zinazohusu ugaidi nakumbuka na nishukru mungu kuwa alifanya busara kuja kwangu kunidokeza.

Jamaa yangu huyu nilikuta ameleta sanduku lake likiwa na nguo nyingi na vitu vingine akinisihi kipindi cha likizo niwapelekee ndugu zake bara isipokuwa yeye na wezake wameshaandaliwa kwenda nje ya nchi na agent aliyeko Zanzibar kwenda Afghanistan kwa ahadi ya malipo makubwa ila kazi walikuwa hawaijui. Nilimuuliza munaondoka lini na umemuaga tajiri yako akasema hapana ila tutakutana sehemu ya pamoja na kuondoka kwa pamoja!!! Bila kupoteza muda nilimuita girlfriend wangu kujumuika katika maongezi haya ambapo awali yalikuwa ya wawili tu na mimi akili ilinituma hawa watu wanaenda kupewa mafunzo hatari ya kigaidi.
Maongezi yangu ya kwanza nikamwambia afute mara moja suala la kusafiri na nikampata maelezo ya kina yenye vitisho kama kwamba na mimi nishawahi kushiriki hilo jambo, nakumbuka kipindi anatoka kijijini kuja Zanzibar huyu ndugu alihitimu tu darasa la saba kijijini kwetu........

TAENDELEA BAADAE
 
CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,552
2,000
mmmh hapa ukisoma mistari basi kuna utata.
kwanza: nikijaribu kuwaulizia viongozi wa umoja wa vijana wa Kisukuma waliokuwa maeneo ya Uroa. Yaani uende dar na uulize vijana wa usukumani au watu kutoka usukumani. ( inawezekana na ukawapata wengi sana )
penye utata: nakumbuka kipindi anatoka kijijini kuja Zanzibar huyu ndugu alihitimu tu darasa la saba kijijini kwetu........ yaani ulibahatika kukutana na mtu mliekuwa kijiji kimoja ( inawezekana ila sio kirahisi ki hivyo, mimi nimewahi kuishi uganda nikiwa nimetoka dar maeneo ya upanga. hapo ugana niliwakuta watanzania wengi ila sio wa maeneneo niliyotoa. niliwahi kuishi kenya na hata hapo kenya niikutana na watu wengi wa TZ ila hakuna niiekutananae na akatokea maeneo niiyokuwa naishi) sikatai kukutana na mtu wa kijijini kwenu ia cha kushangaza mtu huyohuyo anakuwa kwenye story unayotaka kuileta. kuna ile TV series inaitwa LOST no ilikuwa na mpangilio wa story yako.

Yaani na mpaka alielipua ubalozi wa marekani yupo kwenye stori yako.....

anyway endelea......
 
Vijana weeeeeeeengi toka kijijini kwetu nikiwemo mimi tulienda Zanzibar kwa nyakati tofauti kusaka maisha wengine hadi leo wako huko. Waliokuwa wanarudi walitujulisha Ukifika Zanzibar nenda Uroa kwa mzee fulani utakuta wasukuma kibao wakifanya kazi za kulima na kusimamia mashamba na walikuwa na umoja wao wa kusaidiana endapo mmoja atapata matatizo. Nenda Dunga kaulize hii story na kama ni agent au imekugusa tafuta njia nyingine ya kupotosha
 
Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,096
2,000
Ulipima bhupepo angu mwanangwa...
Ukweli siku zote huwa unauma, kuna Watanzania wengi wanafahamu mambo mengi lkn wanayafunika tu ili kuepusha kusumbuliwa, usukumani wanaofanya mauaji ya vikongwe wanajulikana ila huwezi kuwataja maana tayari utakuwa katika hatari na familia yako. Ugaidi upo kwenye jamii yetu ila hofu imetanda. Msanii Roma si kwamba hawajui waliomteka lkn analinda makubaliano yao kwa ajili ya maisha yake. Hayo mimi niliyaona na kama binadamu ni lazima niyakumbushie hata kama upande wa pili utachukia. Kuna padri alipigwa risasi ya kichwa huo si ugaidi!? Tuvumiliane hapa ni jamii forum ni moderator tu ndiye anaweza kuona hii habari haifai kuwepo hapa basi
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,192
2,000
mmmh hapa ukisoma mistari basi kuna utata.
kwanza: nikijaribu kuwaulizia viongozi wa umoja wa vijana wa Kisukuma waliokuwa maeneo ya Uroa. Yaani uende dar na uulize vijana wa usukumani au watu kutoka usukumani. ( inawezekana na ukawapata wengi sana )
penye utata: nakumbuka kipindi anatoka kijijini kuja Zanzibar huyu ndugu alihitimu tu darasa la saba kijijini kwetu........ yaani ulibahatika kukutana na mtu mliekuwa kijiji kimoja ( inawezekana ila sio kirahisi ki hivyo, mimi nimewahi kuishi uganda nikiwa nimetoka dar maeneo ya upanga. hapo ugana niliwakuta watanzania wengi ila sio wa maeneneo niliyotoa. niliwahi kuishi kenya na hata hapo kenya niikutana na watu wengi wa TZ ila hakuna niiekutananae na akatokea maeneo niiyokuwa naishi) sikatai kukutana na mtu wa kijijini kwenu ia cha kushangaza mtu huyohuyo anakuwa kwenye story unayotaka kuileta. kuna ile TV series inaitwa LOST no ilikuwa na mpangilio wa story yako.

Yaani na mpaka alielipua ubalozi wa marekani yupo kwenye stori yako.....

anyway endelea......
Usishanga mkuu kule Zanzibar kuna vijana wengi sana wa Kisukuma na kazi zao ndiyo hizo house boy/shamba boy na kutunza ng'ombe.
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,036
2,000
Kwa hiyo Zanzibar kunamyanya ya kusafirisha watu ili wajekuwa magaidi siyo? Basi hata kibiti nako,amboni,na kule mwanza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom