Shambulio la shule Nigeria: Mamia ya wavulana waliotekwa 'waachiwa huru'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Mamia ya wavulana waliotekwa wiki iliyopita kutoka shule ya bweni kaskazini -magharibi mwa Nigeria wameachiliwa huru, mamlaka katika eneo hilo zimeambia BBC.

Msemaji wa gavana wa jimbo la Katsina amesema wavulana 344 wameachiliwa huru na kwamba wako katika hali nzuri.

Hata hivyo, ripoti zingine zinaashiria kuwa baadhi yao wamesalia mikononi mwa watekaji wao.

'Jinsi nilivyotoroka watekaji' - mwanafunzi Nigeria
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na na wanamgambo la Boko Haram, ambalo awali lilitoa video ikiwaonyesha baadhi ya wavulana hao.

Katika taarifa yake, msemaji, Abdul Labaran, amesema wavulana hao walikuwa wakipelekwa katika mji mkuu wa mkoa wa Katsina, na hivi karibuni wataungana na familia zao.

Amesema video iliyotolewa na na Boko Haram ilikuwa ya kweli, lakini ujumbe unaonekana kutoka kwa kiongozi wa kikundi hicho Abubakar Shekau, ulikuwa wa kuiga.

Hapo awali mamlaka zilitoa idadi ndogo kuliko ile yiliyotolewa na wenyeji kama jumla ya vijana waliotekwa nyara na hadi sasa haijulikani ikiwa wote wako salama.

Gavana wa jimbo hilo Aminu Bello Masari alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema, "tumepata wavulana wengi. Sio wote," huku chanzo cha usalama kililiambia shirika la habari la AFP wengine walibaki na watekaji wao.

Bwana Labaran alisema hakuna hata mmoja wa wavulana waliotekwa nyara aliuawa, huku maoni yake yakikinzana nay ale ya mvulana aliyeonyeshwa kwenye video hiyo ambaye alisema kuwa wengine waliuawa na ndege za kivita za Nigeria

Haijulikani jinsi kuachiliwa huru kwa wavulana hao kulitokea lakini habari hiyo imethibitishwa kwa BBC Hausa na afisa mwingine wa serikali ya jimbo hilo.
 
Possibly walioachiwa ni wenye dini yao hao waliobaki bado wakishikiliwa wataamua sasa wazikane imani zao walizozipenda wabaki salama au wakatae kuzikana shingo zao zing'olewe.

Yeah,Mungu anasaidiwa kazi!
 
Hii scene haieleweki kabisa
Watanzania ni watu wenye akili timamu sana kulinganisha na wengi katika Afrika.

Huu uzi tangu ulipowekwa juzi utaona hakuna mwenye hamu kuusoma.Ndo maana wachangiaji ni wachache mno.Yapo mengi yakushughulika nayo sio upuuzi wa Nigeria.

Watoto wamerudi, walikuwa wapi?

Jeshi limewapata na hawakuumia. Walifanyaje na walimkamata nani kati ya waliowashikilia hao watoto. Mbona jeshi halitoi taarifa ya operesheni muhimu kama hii habari zake zilizochukua nafasi za kimataifa. Ujinga mtupu.
 
Hao watoto wameachiliwa bila kuumizwa huenda sababu watekaji walitaka pesa na huenda serikali ya Nigeria imelipa pesa japo haiwezi kukiri hadharani.
 
Hao watoto wameachiliwa bila kuumizwa huenda sababu watekaji walitaka pesa na huenda serikali ya Nigeria imelipa pesa japo haiwezi kukiri hadharani.
Katika mkasa huu watekaji lazima wawe ni sehemu ya jeshi la Nigeria kwa sababu Nigeria hakuna misitu ya kuficha watoto wote hao hata kwa siku moja.

Ndio maana hakuna taarifa iliyotolewa ya operesheni ya kuwaokoa ilivyoanza na kumalizia.Utaona kuwa ni upuuzi na kupoteza muda wa walimwengu kuzungumzia masuala ya kikundi hewa cha Bokoharam.

Kama wamelipa si mantiki kumlipa mtu anayeitwa Shekau bila kumkamata hapo hapo au baadae.Yeyote aliyeumwa kupokea pesa lazima aoneshe anapopeleka na waliomtuma.Katika dunia ya sasa haya mambo hayawezi kutokea tena bila kuwa ni mtandao kijeshi lenyewe.Na ndipo tunaposema Nigeria hakuna raisi wa maana na serikali ni ya kijanja janja sana.
 
Watanzania ni watu wenye akili timamu sana kulinganisha na wengi katika Afrika.

Huu uzi tangu ulipowekwa juzi utaona hakuna mwenye hamu kuusoma.Ndo maana wachangiaji ni wachache mno.Yapo mengi yakushughulika nayo sio upuuzi wa Nigeria.

Watoto wamerudi, walikuwa wapi?

Jeshi limewapata na hawakuumia. Walifanyaje na walimkamata nani kati ya waliowashikilia hao watoto. Mbona jeshi halitoi taarifa ya operesheni muhimu kama hii habari zake zilizochukua nafasi za kimataifa. Ujinga mtupu.
Wewe siku zote ni mtetezi wa hivi vikundi vyenye mirengo ya kidini. Boko haram ni wahalifu na wapaswa kusakwa.
 
Hii inaitwa tengengeneza tatizo halafu unalitatua mwenyewe sababu ukifuatilia Maelezo hayashawishi kuonesha namna gan walipambana kuwaokoa zaid Watoto wamepatkan ila jins walovyopatikana n siri yao AL SHABAB ISIS BOKO HARAM TALEBAN AL QAEDA hii n mirad kama miradi mingine ya kuingiza pesa isipokuwa wao hawapo BRELA TRA na wala hawana namba ya mlopa kodi TIN katika nchi zao
 
Afrika bado sana. Ina maana serikali ya nigeria, umoja wa kijeshi wa Afrika Magharibi, na umoja wa africa wote wameshindwa kupambana na kuwadhibiti hao boko haram? Inashangaza sana.

Ukiona hivyo ujue Boko Haram ni deal kuna watu ndani ya Serikali na Mataifa ya nje wanafaidika nayo.
 
Wewe jamaa ni kilaza wa standard gauge.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile
Bila kufafanua unachokusudia ni kama hujasema la maana na hueleweki. Mpira utarudi kwako kwamba huna akili ya kujadiliana na watu wenye uono wa mambo ya kidunia. Rudi kwenye zile nyuzi uzipendazo zenye watu wa aina yako.
 
Ni kweli nakubaliana na wewe, unahitaji ukarabati uwezo wako wa kujenga hoja ili ufikie level za kuwa objective.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli nakubaliana na wewe, unahitaji ukarabati uwezo wako wa kujenga hoja ili ufikie level za kuwa objective.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Ungeanza wewe kutoa mfano kwa kuonesha wanajamii unaposema mtu ni kilaza wapi amejifafanua hivyo.Bila kufanya hivyo wewe utakuwa ni zaidi.
Mimi nakupa mfano wa ukilaza wako pale unapoamini Bokoharam wameteka watoto 800 halafu wakawaachia huru bila madhara.Wapi umeona kitu kama hicho kikitokea mbali na Nigeria ambako kuna watu wengi wa mfano wako wanaoamini vitu hewa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom