Shambulio la Owerri: Zaidi ya wafungwa 1,800 watoroka jela Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861

Owerri prison

Polisi wanalaumu shambulio hilo lilifanywa na kundi linalotaka kujitenga la wenyeji wa Biafra, ambalo lilipigwa marufuku

Mamlaka ya kitaifa ya magereza nchini Nigeria imethibitisha kwamba zaidi ya wafungwa 1,800 wametoroka jela nchini humo kufuatia shambulio la watu waliojihami kwa bunduki, maafisa walisema.

Washambuliaji hao waliripotiwa kuvamia gereza hilo lilipo katika mji wa kusini mashariki wa Owerri kwa kutumia vilipuzi.

Wafungwa sita wameripotiwa kurejea huku wengine 35 wakikataa kutoroka.

Polisi wanalaumu shambulio hilo lilifanywa na kundi linalotaka kujitenga la wenyeji wa Biafra, ambalo lilipigwa marufuku. Kundi hili limeripotiwa kupinga madai hayo..
Mamlaka ya usimamizi wa magereza imethibitisha ni wafungwa 1,844 waliotoroka gerezani katika jimbo la Imo.

Watu waliokuwa wamejihami wa silaha nzito nzito walivamia kituo cha kuwazuilia wafungwa mjini Owerri mapema Jumatatu, baada ya kuwasili wakiwa wameabiri magari na mabasi, amaafisa walisema.

Msemaji wa polisi alisema washambuliaji hao walitumia maroketi, maguruneti na silaha zingine katika uvamizi huo.

Owerri attack

Magari yaliyochomeka yalionekana katika maeneo yaliyolipuliwa

Rais Muhammadu Buhari ametaja shambulio hilo kuwa "kitendo cha ugaidi". Ameelekeza vikosi vya usalama kuwakamata washambuliaji hao pamoja na wafungwa waliotoroka.

Msemaji wa vugu vugu la watu Biafra wanaotaka kujitenga liliambia shirika la habari la AFP kwmaba madai kuwa lilihusika na shambulio la Jumatatu ni "uwongo".

Jimbo la Imo kwa muda mrefu limekuwa eneo linalokuza makundi ya watu wanaotaka kujitenga ,huku uhusiano kati ya serikali kuu na wenyeji wa jamii ya Igbo ukiwa wa mvutano.

Tanhu mwezi Januari vituo kadhaa vya polisi na magari katika eneo la kusini mashariki mwa Nigeria yameshambuliwa na silaha kuibiwa. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulio hayo.
 
Rais Buhari ni kilaza mno. Tena ajabu ni kuwa alikuwa Jenerali jeshini na kawa rais mara ya pili
Ukilaza wake ni upi boss? Kumbuka bokoharam kwa Sasa wamerudishwa sana nyuma japo bado wanasumbua.

Tatizo la huko Biafra halijaanza leo, Buhari amerithi tu, kumbuka Nigeria ina matatizo mengi sana ya ndani kuanzia udini, ukabili,ugaidi,ufisadi na mengine mengi.

Buhari amejitahidi sana tofauti na mtangulizi wake.
 
Ukilaza wake ni upi boss? Kumbuka bokoharam kwa Sasa wamerudishwa sana nyuma japo bado wanasumbua.

Tatizo la huko Biafra halijaanza leo, Buhari amerithi tu, kumbuka Nigeria ina matatizo mengi sana ya ndani kuanzia udini, ukabili,ugaidi,ufisadi na mengine mengi.

Buhari amejitahidi sana tofauti na mtangulizi wake.
Boko Haram alikuwa na uwezo wa kuizuia. Tuachane hawa separatists ambao ni vigumu ila Boko Haram uwezo wa kupambana nao alikuwa nao kabisa, ila sasa political motives na priority hiyo hana.

Wanafunzi mia ngapi wanatekwa na wahuni wanaswaga msituni bila taarifa kujua walipo? Then wakishakombolewa bado hajui apambane nao vipi. Wana silaha gani wale kwamba vifaru na ndege, si ni RPG, double cabin na SMG na kama hizo. Magaidi wa kujitoa mhanga ndio wagumu ila hawa wenye kambi kabisa ni uzembe kuwadekeza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom