Shambulio la marekani tumejifunza nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shambulio la marekani tumejifunza nini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 25, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MASHAMBULIZI YA MAREKANI SOMALIA TUMEJIFUNZA NINI

  Ndugu

  Tumeona siku za karibuni Jeshi la marekani kwa kutumia ndege zake zilifanikiwa kumuuwa gaidi mmoja raia wa Kenya waliyekuwa wanamtafuta sana toka balozi zao zilipolipuliwa jijini dar es salaam na nairobi .

  Nimeshangaa kwanini serikali ya Kenya haikuingia yenyewe ndani ya Somalia kwenda kumtafuta gaidi huyo kama walikuwa wanajua alipo na taarifa za uwepo wake katika eneo hilo , badala yake wameruhusu jeshi la marekani kushambulia eneo hilo na kufanikiwa kumuuwa gaidi huyo

  Nachouliza nchi yetu ya tanzania tumejiandaa vipi na vitendo hivi vya jeshi la marekani kuingilia mipaka ya nchi zingine kwa matakwa yao wenyewe , serikali ya Kenya haijatoa tamko lolote la maana kwa nchi ya marekani wala umoja wan chi za afrika nao umekaa kimya tu kuhusu shambulio hilo pamoja na kwamba wamezoea kufanya mashambulizi siku za nyuma .

  Binafsi sipendi harakati za kigaidi mahala popote lakini pia sipendi kuona nchi zinavyovamia nchi zingine kwenye kuuwa watuhumiwa haswa kwa njia hizo zilizotumika kesho kutwa tunaweza kusikia wameenda kupiga mwanza kutafuta magaidi

  Na ndio kwanza wanatafuta nafasi ya kuanzisha kituo chao cha kijeshi kwa nchi za afrika , naamini huko mbeleni kutakuwa na matishio makubwa zaidi ya hili kwa nchi hiyo kuamua kuvamia nchi zingine
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Nenda mbali zaidi ya kutokupenda.

  Do something about it to show your seriousness!

  Innocent pals are killed.
   
 3. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Shy mbona Tanzania ilivamia Uganda>...what do you say abou that?
   
 4. A

  Alvin Member

  #4
  Sep 26, 2009
  Joined: Sep 7, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa unajua mimi hapo ndipo ninapokushangaa maana kwana umesema kwamba unashangaa serikali ya kenya haikuingia yenyewe kumsaka gaidi huyo sasa unataka marekani nao wakae kimya kama kenya ili apange mbinu zingine shida ya sisi africa hatujishughulishi sasa mtu yuko kenya lakini gaidi mpaka auliwe na mtu kutoka marekani jamani hii nini hasa
   
 5. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kweli dada Kelly Tulivamia Uganda mbona hatukusema nini? Tulikwenda kumpiga nduli pale Kagera au ilikuwa gear ya kuingilia tu, mpaka leo Tanzania haikukaa sawa, acha we ufisadi ulianzia mbali kweli
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mimi napongeza wamarekani kwa kazi nzuri ya kupambana na ugaidi, kwanza hata wangeweka kambi yao TZ ni poa tu kwa sababu sisi tumeshindwa hata kutafuta mabomu ya mbagala je al qaeda tutawaweza? ambao wanawasumbua hata marekani wenyewe?

  Kuhusu issue ya somalia, kwanza kenya hawakujua kwamba nabhan yupo somalia kutokana na weakness ktk intel yao sasa wangeingia vipi huko while hawajui kama adui yupo.
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kinyume cha haki za utawala wa nchi. Lakini kwa kuwa marekani ndio polisi wa Duniya basi ndio anapeta
   
 8. m

  mbarbaig Senior Member

  #8
  Sep 27, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yule gaidi kauwawa Somalia na ndio alikimbilia...ujue kuwa anahusika pia kushambulia interest za marekani...apart from ndege ya israel an hotel za mombasa ku target wamarekani na israel...Somalia wahalifu wote wanakimbilia huko..kabla hawajasumbua wengine they have to be neutralized
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  :(
  Mkuu inaelekea uelewa wako wa haya masual ya kufuatilia magaidi yana walakin.
  Kwanza huwezi kulinganisha Kenya au Tanzania kwa uwezo wa kuwafuatilia hao magaidi na Marekani.
  Kama si Marekani tusingewajua waliotehga mabomu ubalozi wa Marekani Kenya na Tanzania.Hii ni kwa sababu ugaidi huu asili yake ni mtandao ambao wala hatungeweza kuufuatilia.Uwezo wa vitengo vyetu vya ulinzi unaeleweka vyema.
  Leo ni miaka 11 toka kulipuliwa mabomu balozi za Marekani Dar es salaam na Nairobi.Leo umma wa kitanzania bado uko gizani juu ya mlolongo mzima wa jambo hili.
  Hatuwezi kujifananisha na Marekani katika bajeti kufanya investigation,surveillance na hatimaye kufanya surgical execution ya kuua hawa magaidi.
  Kwa upande wangu mimi nawapongeza Marekani kwa hilo.Tukumbuke kuwa katika milipuko ya DSM na Nairobi karubu wote waloi uwawa ni ndugu zetu.
  Hivyo basi kama magaidi hao watakuwepo hapa kwetu na wanajificha tukipata msaada wa aina yoyote kuna ubaya gani
  Vile vile kumbuka hivi karibuni kulikuwepo na mazoezi ya kijeshi kati ya nchi zetu za Afrika Mashariki katika kujiweka sawa na tishio la magaidi.
   
Loading...