Shambulio la Marekani dhidi ya Jenerali wa Iran lilikiuka sheria za kimataifa

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
776
2,404
Shambulio la Marekani ambalo lilimuua Jenerali Qasem Soleimani lilikiuka sheria za kimataifa, wataalamu wa Umoja wa mataifa wamesema.

Soleimani alikufa pamoja na watu wengine tisa katika shambulio la anga karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq mwezi Januari.

Muwakilishi wa kitengo maalum cha Umoja wa mataifa kinachoangazia mauaji ya kiholela, Agnes Callamard, anasema Marekani haijatoa ushaidi wa kutosha kuhalalisha shambulizi hilo.

Marekani ilimshutumu kwa kuchochea ugaidi.

Wiki iliyopita, Iran ilitoa waranti ya kukamatwa kwa rais wa Marekani Donald Trump na watu wengine 35 kwa shutuma za mauaji na ugaidi.

Qasem Soleimani alikuwa nani?
Tangu mwaka 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kitengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.

Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati Mashariki ya kati kupitia vikosi vya Kikurdi, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.

Jina lake lilianza kuwa maarufu alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ushirikiano wa karibu na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja ulamaa huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.

Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.

Jenerali Qasem Soleimani hakuwa anajulikana na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.

Umashuhuri wake uliimarika hatua ambayo ilifanya maafisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.

Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.

Bwana Trump alimuelezea Soleimani kuwa gaidi namba moja duniani kote.

Alidai uongozi wa jenerali uliwalenga Wamarekani na kuwajeruhi pamoja na kuwaua mamia ya raia na watumishi wa Marekani miaka 20 iliyopita na jenerali huyo alifanya shambulio la roketi nchini Iraq mwezi Desemba na kumuua mkandarasi ambaye alikuwa raia wa Marekani.

Soleimani alikufaje?
Jenerali aliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad akiwa katika ndege inayotokea Syria mapema Januari 3.

Alikuwa anaondoka uwanja wa ndege akiwa pamoja na maafisa wa juu pamoja na wanambo wa Shia ambao walikuwa wanaungwa mkono na Iran wakati kundi hilo liliposhambuliwa na ndege isiyo na rubani ya Marekani.

Miongoni mwa watu ambao waliuawa pamoja na Soleimani alikuwa Abu Mahdi al-Muhandis, naibu kamanda wa kundi la kijeshi lenye umaarufu mkubwa na mwamvuli wa jeshi la Shia.

Bwana Trump alisema, alitoa amri ya shambulio hilo la anga ili 'kusitisha vita' kati ya Marekani na Iran.

"Soleimani alikuwa amepanga mpango mbaya wa shambulio dhidi ya wanadiplomasia wa Marekani na wanajeshi wake, lakini aliuawa kabla ya kutimiza mipango" .

Siku tano baadae, Iran ilishambulia ngome mbili za jeshi la Iraqi zilizowahodhi wanajeshi wa Marekani. Na hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeuawa lakini zaidi ya watu 100 waliathirika na majeraha ya ubongo.

Ripoti ya wataalamu wa UN inasemaje?
Agnes Callamard amewasilisha ripoti yake siku ya Alhamisi katika baraza la Umoja wa mataifa kitengo cha haki za binadamu huko Geneva.

Ripoti yake inasema Marekani haijatoa ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa Soleimani alikuwa amepanga shambulio la siri dhidi ya maslahi ya Marekani hasa nchini Iraq, kufanya hatua za haraka kuwa muhimu kuchukuliwa.

"Meja Jenerali Soleimani alikuwa kiongozi wa mikakati ya jeshi la Iran na matukio nchini Syria na Iraq. Lakini tishio la Marekani kuondoa maisha yake kabisa lilikuwa kinyume na sheria."

Marekani imepokeaje ripoti hii?
"Ripoti hii inaminya haki za binadamu na kuwapa mwanya magaidi kufanya wanachotaka na kwa mara nyingine hatua hii inathibitisha tena kwa nini Marekani ilikuwa sahihi kuondoka katika baraza la umoja wa mataifa linaloangazia haki za binadamu mwaka 2018,alisema msemaji wa mambo ya nje wa Marekani Morgan Ortagus.


===
My take

Swala la ubaguzi ni kubwa sana dunia. na hii sio kwa watu weusi tu.
embu fikiria hao wairan walilipua ndege ya marekani wakalipua ndege ya abiria wa nchini kwao. wakalipua kambi ya jeshi la marekani nchini Iraq lakini hatujawahi kusikia umoja wa mataifa ukisema iran inamakosa kisheria.

Lakini mmarekani kumlipua jenerali wa iran imekuwa ni kosa kwenye sheria za umoja wa mataifa

na wakati huo ukiangalia zaidi umoja wa mataifa unaangazia zaidi kuuwawa jenerali na wairan na wakati huyo jenerali wakati anauwawa alikuwa na wenzake tisa. Ni kama hao wengine walikuwa sio watu.

Na je huyo jenerali yeye alikuwa anathamani gani kuliko binadamu wengine ambao wanakufa kila siku na umoja wa unakaa kimya.
 
... zile kejeli na matusi ya nguoni kutoka Tehran yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu Soleman alipuliwe; kumbe ndiye alikuwa mater mind wa mitusi ile.
 
... zile kejeli na matusi ya nguoni kutoka Tehran yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu Soleman alipuliwe; kumbe ndiye alikuwa mater mind wa mitusi ile.
Zile kelele za US toka wapigwe vile vikombora wameufyata kumbe yale makontena ndio yalikua yanazingua
 
Ure take

Ndege yamarekani ipi ilioripuliwa ?!

Si ndio hapo mkuu, Iran haijawahi kulipua ndege yoyote ya Marekani inayo beba abiria.

Ninacho kumbuka mimi mwaka 1988 Marekani ndio wali wahi kutungua ndege ya abiria ya Iran na kuua abiria wote 300, baadae US akaomba msamaha kwa Iran wakidai ndege ilitunguliwa kimakosa.
 
Zile kelele za US toka wapigwe vile vikombora wameufyata kumbe yale makontena ndio yalikua yanazingua
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png

Madhara yaliyo sababishwa na makombora ya Iran kwenye makambi ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq yaliwakata ngebe akina Trump, Pompeo na majenerali wa jeshi la Marekani - baada ya tukio hilo la kutisha siku hizi USA haichukulii Iran poa hata kidogo.

Shuhuda wa shambulio la Iran ambaye ni raia wa Uholanzi smbaye alikuwa anaishi karibu na kambi ya jeshi la Merikani alisema kwamba sonic boom ya makambora ya Iran yalikuwa na sauti ya kutisha sana sana,yalipo hit designated targets mlipuko na shock wave vilikuwa extra ordinary, kaongezea kusema kwamba katika maisha yake hajawahi kushuhudia milipuko yenye kufikia kiwango hicho. Mimi sikushangazwa na comments za shuhuda huyo baada ya kupata taarifa kwamba wanajeshi 100 wa Kimerikani walio kuwa wamejichimbia kwenye mahandaki kama panya buku walikimbizwa kwenda kutibiwa kwenye Hospitali za Kuwait,Ujerumani na USA - hii inadhilisha kwamba mashambulizi ya makombora ya Iran hayakuwa ya kawaida kuanzia kwenye nguvu za mlipuko,madhala na ulengaji shabaha ambao ni dead accurate - it came as a shock to Trump,Pompeo and US Military top brass - hawatarudia tena kuwachukulia wa Iran kimzaa zaa.
 
Marekani anaendelea kula kipigo, Juzi kuna kamanda wao kauwawa Afghanistan, wanasema eti watalipiza kisasi
... zile kejeli na matusi ya nguoni kutoka Tehran yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu Soleman alipuliwe; kumbe ndiye alikuwa mater mind wa mitusi ile.
 
Marekani anaendelea kula kipigo, Juzi kuna kamanda wao kauwawa Afghanistan, wanasema eti watalipiza kisasi
... tunazungumzia habari za the highest figure; the general of the army; kuuliwa kama kuku wewe unatuletea habari za koplo kujeruhiwa uwanja wa mapigano.
 
Si ndio hapo mkuu, Iran haijawahi kulipua ndege yoyote ya Marekani inayo beba abiria.

Ninacho kumbuka mimi mwaka 1988 Marekani ndio wali wahi kutungua ndege ya abiria ya Iran na kuua abiria wote 300, baadae US akaomba msamaha kwa Iran wakidai ndege ilitunguliwa kimakosa.
Ujinga kabisa, yaani unatungua raia wangu halafu unakuja na vijimaneno shenzi kabisa . .yaani nitakunyoosha unyooke
 
Back
Top Bottom